Vatican yapendekeza Jumuiya ya Mtakatifu Pio X kuanzisha mazungumzo ya kitaalimungu
Na Salvatore Cernuzio – Vatican.
Mkutano wa "mchangamfu" na "wa dhati", uliofanyika kwa "idhini" ya Papa Leo XIV, uliooneshwa na pendekezo la kuanzisha "mazungumzo maalumu ya kitaalimungu" na kuhitimishwa kwa pendekezo wazi: kwamba Jumuiya ya Mtakatifu Pio X isimamishe uamuzi kuhusu kuwekwa wakfu wa kiaskofu uliotangazwa kwa sababu hii "ingemaanisha kuvunjika kwa uamuzi wa ushirika wa kikanisa (mgawanyiko) na matokeo mabaya kwa Jumuiya kwa ujumla." Alhamisi tarehe 12 Februari 2026 mazungumzo yalifanyika kati ya Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, Kardinali Víctor Manuel Fernández, na Padre Davide Pagliarani, Mkuu wa Shirika la Udugu wa Mtakatifu Pio X(SSPX) umoja wa mapadre unaojulikana zaidi kama Walefebvrian, uliopewa jina la Askofu Marcel Lefebvre, ambaye alianzisha chama hicho miaka ya 1970 kupinga mageuzi ya Mtaguso wa II wa Vatican. Unaweza kusoma maandishi kamili: LEGGI QUI IL TESTO INTEGRALE DEL COMUNICATO DEL DICASTERO PER LA DOTTRINA DELLA FEDE
Mkutano na Kardinali wa Argentina ulitangazwa mnamo tarehe 4 Februari kama matokeo ya kwanza halisi ya "mawasiliano" kati ya Vatican na Jumuiya ya Mapadre ya Mtakatifu Pio X(SSPX) yaliyolenga "kuepuka kutokubaliana au suluhisho la upande mmoja kwa masuala yaliyojitokeza." Hatua hii ya mwisho ilisisitizwa katika taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican iliyochapishwa mnamo tarehe 3 Februari 2026, siku moja baada ya tangazo la Jumuiya la kuwekwa wakfu kwa maaskofu wajao. Pagliarani mwenyewe, wakati wa sherehe iliyofanyika katika seminari ya SSPX huko Flavigny-sur-Ozerain, Ufaransa, alitangaza kwamba atawakabidhi Maaskofu wawili wa Jumuiya hiyo, Mhispania Alfonso de Gallareta na Mswiss Bernard Fellay, jukumu la "kuendelea na kuwekwa wakfu kwa Maaskofu wapya" mnamo Julai 1, bila idhini ya Papa.
Kitendo hiki kingeiga kile cha mnamo tarehe 30 Juni 1988, wakati Askofu Mkuu Lefebvre alipowapatia wakfu Maaskofu wanne, na hivyo kulazimika kutengwa na Kanisa. Wawili kati ya hao wanne walikuwa Fellay na de Gallareta. Taarifa ya Mkuu wa Shirika kuanzia mwanzoni mwa Februari ilirejea barua iliyotumwa Vatican ikielezea "hitaji maalum la Jumuiya la kuhakikisha mwendelezo wa huduma ya Maaskofu wake," na kusisitiza kwamba hakuna jibu lililofika bado kutoka Roma. Hata hivyo, Alhamisi Februari 12, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na Mkuu wa SSPX walikutana katika Jumba la Ofisi Takatifu. Maelezo ya mkutano yameripotiwa katika taarifa iliyosainiwa na Kardinali Víctor Manuel Fernández, ambayo inasema kwamba "baada ya kufafanua baadhi ya mambo yaliyowasilishwa na SSPX katika barua mbalimbali, zilizotumwa hasa kati ya 2017 na 2019, miongoni mwa mengine, swali la mapenzi ya Mungu kuhusu dini nyingi, mkuu alipendekeza njia ya mazungumzo ya kitaalimungu, yenye mbinu maalum sana, kuhusu masuala ambayo bado hayajafafanuliwa vya kutosha."
Mada hizi ni pamoja na: "Tofauti kati ya tendo la imani na 'unyenyekevu wa kidini wa akili na utashi,'" na "viwango tofauti vya uzingatiaji vinavyohitajika na maandishi mbalimbali ya Mtaguso wa Kwanza la Kiekumeni wa Vatican na tafsiri yake." Wakati huo huo, ilipendekezwa "kushughulikia mfululizo wa masuala yaliyoorodheshwa na SSPX katika barua ya tarehe 17 Januari 2019." Kwa mujibu wa taarifa, "Mchakato huu ungelenga kuangazia, katika mada zilizojadiliwa, mahitaji ya chini kabisa ya ushirika kamili na Kanisa Katoliki na, kwa hivyo, kuelezea hadhi ya kisheria ya Udugu, pamoja na mambo mengine yatakayochunguzwa zaidi."
Kiti Kitakatifu pia kilirudia kwamba "daraja la kuwekwa wakfu wa maaskofu bila agizo la Baba Mtakatifu, ambaye ana mamlaka ya juu ya kawaida, ambayo ni kamili, ya ulimwengu wote, ya haraka, na ya moja kwa moja, ingemaanisha kuvunjika kwa ushirika wa Kanisa (utengano), na matokeo mabaya kwa Udugu kwa ujumla." Kwa hivyo, "uwezekano wa kufanya mazungumzo haya unamaanisha kwamba Udugu unasimamisha uamuzi kuhusu kuwekwa wakfu, uliotangazwa wa maaskofu." Mkuu wa Shirika la Udugu wa Mtakatifu Pio XI(SSPX)"atawasilisha pendekezo hilo kwa Baraza lake na kutoa jibu lake kwa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, "Ikiwa kuna jibu chanya, hatua, kwa hatua, na taratibu zitakazofuatwa zitakubaliwa pande zote mbili," hati hiyo inasisitiza. Mwishoni mwa mkutano, ombi la maombi linafanywa "kwa Kanisa lote" ili kusindikiza safari hii, hasa katika nyakati zijazo, pamoja na maombi kwa Roho Mtakatifu, mbunifu mkuu wa ushirika wa kweli wa kikanisa unaotamaniwa na Kristo."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Bonyeza hapa tu: Just click here.