Tafuta

2026.02.13 Sr Nina Krapić,Papa Leo XIV. 2026.02.13 Sr Nina Krapić,Papa Leo XIV. 

Sr Nina Krapić Naibu Mkurugenzi Mpya wa Ofisi ya Habari ya Vatican!

Papa Leo XIV amemteua Mtawa huyo wa Krozia,ambaye hapo awali alikuwa afisa wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano,anachukua nafasi ya Cristiane Murray,ambaye anaacha wadhifa wake aliochukua tangu Julai 2019.

Vatican News

Papa Leo XIV amemteua Naibu Mkugenzi wa Ofisi ya Habari ya Kiti Kitakatifu Sr Nina Benedikta Krapić M.V.Z., ambaye anachukua nafasi ya Cristiane Murray, aliyejiuzulu kutoka wadhifa alikuwa nao, tangu Julai 2019 na Sr Nina alipokelewa na Baba Mtakatifu, asubuhi tarehe 13 Februari 2026. Hili lilitangazwa katika jarida la Ofisi ya Habari ya Vatican.

Mtawa huyo wa Kroatia hadi sasa alikuwa Afisa wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, atachukua wadhifa wake mpya kuanzia tarehe 1 Machi 2026.  Sr Krapić alizaliwa Rijeka, Kroatia, mnamo tarehe 7 Juni  1989. Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Rijeka akiwa na shahada ya Sheria mnamo 2015, akibobea katika Mahusiano ya Umma katika Chuo Kikuu cha Zagreb mnamo 2023.

Alifunga nadhiri za Milele katika Shirika la Watawa wa Upendo la Mtakatifu Vincent wa Paulo mnamo tarehe 13 Agosti 2023. Amefanya kazi kama mwandishi wa habari na kama mshauri wa kisheria kwa wanawake waathiriwa wa nyanyaso za majumbani na watu wengine waliotengwa. Aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Caritas Jimbo Kuu la Rijeka. Tangu 2023, amekuwa Afisa wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na mwanafunzi wa udaktari katika Sayansi Jamii katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian Roma.

"Ninamshukuru sana Cristiane Murray," alisema Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Dk. Paolo Ruffini, "kwa kujitolea na taaluma ambayo ameitumia kutekeleza huduma yake. Kwa roho hiyo hiyo, ninamtakia Sr Nina Benedikta Krapić matashi yangu mema ya mafanikio, nikitegemea sifa zake nzuri za kitaaluma na kibinadamu."

Naibu Ofisi ya Habari Vatican

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here.

13 Februari 2026, 12:11