Tafuta

2026.02.20:Kard.Grech na Askofu Arrieta,rais mwenza na mratibu wa Tume ya Sheria ya Kanisa la Mashariki,pamoja na wajumbe wengine wa chombo kipya. 2026.02.20:Kard.Grech na Askofu Arrieta,rais mwenza na mratibu wa Tume ya Sheria ya Kanisa la Mashariki,pamoja na wajumbe wengine wa chombo kipya. 

Sinodi yaanzisha tume mpya kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki

Sekretarieti Kuu ya Sinodi imeunda Tume mpya iliyopewa jukumu la kuhamasisha mawazo ya marekebisho ya Kanuni za Sheriza za Makanisa ya Mashariki kwa kuzingatia safari ya Kisinodi.Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Sekretarieti hiyo,Kardinali Mario Grech,“Tume hiyo ni matokeo ya ombi lililotolewa na viongozi kadhaa wa Makanisa ya Sui Iuris.”

Vatican News

Sekretarieti Kuu ya Sinodi imeunda chombo kipya kitakachojitolea kwa ajili ya kutengeneza mapendekezo ya marekebisho ya Kanuni za Makanisa ya Mashariki(CCEO) katika muktadha wa safari ya kisinodi. Kwa kupewa jina la “Tume ya Kanoni ya Mashariki, ilikutana kwa mara ya kwanza mnamo  tarehe 20 Februari 2026 katika  Makao Makuu ya Sekretarieti Kuu Sinodi, mjini Vatican.

Tume inajibu maombi kadhaa

Tume hii mpya inajengwa juu ya kazi ya Tume ya Kanoni ambayo iliundwa mnamo Desemba 2023. Tume hiyo tayari ilikuwa imewasilisha mapendekezo kadhaa kwa ajili ya mageuzi ya Kanuni za Makanisa ya Mashariki(CCEO,) ingawa lengo lake kuu lilikuwa Sheria ya Kanoni ya Kanisa la Kilatini. Tume ya Kanoni ya Mashariki ya 2026 pia inajibu maombi kadhaa yaliyotolewa na viongozi wa Makanisa ya (sui iuris) Kisheria. 

Haya ni Makanisa 24 yanayojitegemea ndani ya Kanisa Katoliki ambayo yana ushirika kamili na Baba Mtakatifu, lakini yanadumisha tamaduni, liturujia, sheria, na utawala wao Maalum.. Kwa lengo la kukuza ushirikiano wa kati ya muungano wa Kipapa ili kuhudumia Makanisa mahalia, Tume mpya imeundwa na wataalamu wa sheria za Kanisa la Mashariki ambao wamechaguliwa kutoka kwa washauri wa Baraza la Kipapa la Maandiko ya Sheria na Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki.

Ilikuwa sahihi kuanzisha Tume Maalum

Kardinali Mario Grech, Katibu Mkuu Sekretarieti ya Sinodi, alielezea kwamba “ilionekana kuwa sahihi kuanzisha Tume Maalum ambayo inaweza kufanya kazi kwa karibu na Kikundi cha Utafiti, kufungu cha 1 kuhusu Vipengele Fulani vya Mahusiano Kati ya Makanisa Katoliki ya Mashariki na Kanisa la Kilatini" huku "ikizingatia umaalum wa Sheria ya Kanisa la Mashariki."

Kikundi hiki cha Utafiti ni mojawapo ya kumi zilizoanzishwa na Papa Francisko mwaka 2024, kufuatia Kikao cha Kwanza cha Mkutano Mkuu wa Kawaida wa XVI wa Sinodi ya Maaskofu. Wakati wa mkutano huo, mada kadhaa muhimu kuhusu maisha na utume wa Kanisa katika muktadha wa Sinodi ziliibuka. Katika roho ya Sinodi “inayotambulisha awamu hii ya utekelezaji,” Kardinali Grech aliwaalika “Makanisa ya (sui iuris,)Kisheria,  mikutano ya Maaskofu, Vyuo vikuu vya Kikatoliki, Taasisi, na watu binafsi wanaopenda kuwasilisha michango yao kwa Sekretarieti Kuu ya Sinodi ifikapo  tarehe 15 Aprili 2026.”

Mamlaka

Kwa muda mfupi, Tume hii mpya imepewa jukumu la kuandaa “rasimu ya maandishi ya Kanuni ili kutekeleza mapendekezo ya kisheria yaliyotolewa wakati wa safari ya Kisinodi ya 2021-2024, hasa yale yaliyoorodheshwa katika Ripoti ya Mhutasari (2023) na katika Hati ya Mwisho (2024).” Katibu wa Baraza la Kipapa la Maandiko ya Sheria, ambalo ni chombo kinachohusika cha Baraza la Kipapa, ataratibu kazi ya Tume hiyo ikiwa ni pamoja na kusasisha sheria ya sasa ya Mashariki.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

 

24 Februari 2026, 10:23