Siku ya Radio Duniani,podikasti ya Radio Vatican kuhusu AI
Vatican News
"Akili Unde ni chombo, si sauti." Kichwa cha toleo la 2026 la Siku ya Radio Duniani, lililoadhimishwa Februari 13 siku moja baada ya maadhimisho ya miaka 95 ya kuanzishwa kwa Radio Vatican, kilishuhudia vyombo vya habari vya Kiti Kitakatifu kilipendekeza na kukuza mpango maalum katika lugha saba, huku vipindi saba vya radio vikibadilishwa kuwa podikasti zenye mada zilizowekwa kwa mustakabali wa radio, utumishi wa umma, uvumbuzi, na uhusiano kati ya vyombo vya habari, jamii, na akili unde.
Matangazo ya lugha ya Kiitaliano, yaliyoandaliwa na Andrea De Angelis, yaliwashirikisha wageni Andrea Borgnino, Mkuu wa maudhui wa RaiPlaySound na mtangazaji wa Radio3, na Ivana Faccioli, Mkurugenzi wa habari wa RTL 102.5, Alessandro Gisotti, Naibu Mkurugenzi wa uhariri wa Vyombo vya Habati Vatican na rais wa EBU Radio News Group, na Massimiliano Menichetti, Naibu Mkurugenzi wa uhariri wa Vyombo Vya Habari vya Vatican na Mhusika wa Radio Vatican - Vatican News.
Kusikiliza podikasti katika Siku ya Radio Ulimwenguni
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here