Tafuta

Amani huanza na utu:Wito wa kimataifa wa kukomesha biashara haramu ya binadamu ndiyo kauli mbiu ya 2026. Amani huanza na utu:Wito wa kimataifa wa kukomesha biashara haramu ya binadamu ndiyo kauli mbiu ya 2026. 

Siku ya Maombi Duniani na Tafakari Dhidi ya Biashara Haramu wa Binadamu 2026

Mtandao wa Kimataifa wa kupambana na biashara haramu ya binadamu Talitha Kum unavyoeleza kuwa Siku ya kupambana dhidi ya Biashara ya Binadamu tarehe 8 Februari inaambatana na ukumbusho wa kiliturujia wa Mtakatifu Josephine Bakhita,Mtawa wa Sudan ambaye alitekwa nyara na kutumwa akiwa na umri mdogo na baadaye akawa ishara ya ulimwengu ya kujitolea kwa Kanisa katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya binadamu.Siku hiyo ilianzishwa na Papa Francisko kunako 2015.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Amani huanza na utu:Wito wa kimataifa wa kukomesha biashara haramu ya binadamu, ndiyo kauli mbiu ya  Toleo la XII inayoongoza  Siku ya Maombi dhidi ya Biashara haramu ya binadamu kwa mwaka 2026 sanjari na Kumbukizi ya Mtakatifu Josephine Bakhita, Mtawa wa Sudan ambaye alitekwa nyara na kutumwa akiwa na umri mdogo na baadaye akawa ishara ya ulimwengu ya kujitolea kwa Kanisa katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya binadamu. Siku hii ilianzishwa na Papa Francisko kunako mwaka 2015. Papa Leo XIV anatukumbusha umuhimu wa kuheshimu moja ya kanuni za msingi za mtu binafsi: utu wa binadamu, unaoeleweka kama nguzo muhimu ya kujenga amani halisi.

Kundi la washiriki wa Siku ya Kimataifa dhidi ya Biashara haramu
Kundi la washiriki wa Siku ya Kimataifa dhidi ya Biashara haramu   (@Vatican Media)

Hata hivyo, Ujumbe kutoka Mtandao wa Kimataifa wa kupambana na biashara haramu ya binadamu wa Talitha Kum, ulikuwepo katika Katekesi ya Baba Mtakatrfu Leo XIV Jumatano tarehe 4 Februari 2026, kabla ya Siku hii ya XII  ya Maombi Duniani na Tafakari dhidi ya Biashara  Haramu wa Binadamu, iliyopangwa kufanyika mnamo Februari 8. "Kuja hapa kutoka kila bara, kukusanyika mbele ya Papa kusikiliza maneno yake, ambayo tangu siku ya kwanza yametualika kuishi kwa amani na sisi wenyewe, katika nchi yetu, katika jamii yetu, ilikuwa wakati mtakatifu." Alisema hayo Sr Abby Avelino, Mratibu wa Talitha Kum, Mtandao wa Kimataifa unaoendelezwa na Watawa wa Kike na Kiume dhidi ya jambo la aibu la biashara haramu ya binadamu, akizungumza kwa niaba ya ujumbe wa watu 20, karibu wanawake wote, waliokuwepo katika Katekesi hiyo.

"Kutoka kwa Papa Leo XIV," alieleza, "tulipokea kutiwa moyo kuendelea na mapambano dhidi ya janga la biashara haramu ya binadamu, tukijua kwamba amani haitawezekana isipokuwa tuheshimu utu wa binadamu." Hwa wanatoka Pakistan, Burundi, Lebanon, Japan, Italia, Ecuador, Brazili, Botswana, Australia, Ukraine, na Venezuela na wako mjini Roma kushiriki katika mipango iliyopangwa hadi Dominika  ijayo, tarehe 8  Februari 2026, katika Siku ya 12 ya Maombi Duniani na Tafakari dhidi ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu na ukumbusho wa kiliturujia wa Mtakatifu Josephine Bakhita. Mtawa huyo wa Sudan, aliyetangazwa kuwa Mtakatifu mnamo tarehe 21 Oktoba 2000, na Papa Yohane Paulo  II,  alipata uzoefu wa utumwa tangu akiwa na umri wa miaka saba na kwa hivyo anachukuliwa kuwa ishara ya ulimwengu wote ya kujitolea kwa Kanisa kupambana na janga hili.

Papa akiwabariki washiriki wa Tukio la Kimataifa dhidi ya Biashara haramu ya Binadamu
Papa akiwabariki washiriki wa Tukio la Kimataifa dhidi ya Biashara haramu ya Binadamu   (@Vatican Media)

Sr Avelino, alisisitiza kwamba lengo ni "kukuza jamii yenye heshima na amani, kulinda sio tu waathiriwa na manusura wa usafirishaji haramu wa binadamu, lakini zaidi ya yote wale watu walio katika mazingira magumu walionaswa katika uhalifu huu," anaongeza kwamba "unyonyaji wa watu kimsingi huharibu misingi ya amani na haki." Na "kwa hivyo, tunataka kuwakomboa takriban watu milioni 27, wengi wao wakiwa wanawake, watoto, wahamiaji waliolazimishwa kukimbia, na waathiriwa wa usafirishaji haramu." Kwa mujibu wa mtandao wa kimataifa wa kupambana na biashara haramu ya binadamu ‘Talitha Kum’ unavyosema kwamba “kupitia sala, tafakari, na ushiriki, tunaboresha dhamira yetu na kuimarisha umoja wetu katika mapambano ya kurejesha thamani ya mtu.”

Siku ya Kimataifaha ya kupambana na biashara dhidi ya binadamu

Safari itaanza na mkesha wa maombi mnamo tarehe 5 Februari 2026 saa 11:30 jioni masaa ya Ulaya katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria huko Trastevere, jijini Roma, ambapo Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu, Mons. Jozef Barlaš, atatoa tafakari. Jumuiya zilizojitolea kijamii zitakusanyika katika mji mkuu, na kuunda wakati wa pamoja na usemi mpana wa ukweli mwingi unaohusiana na biashara haramu ya binadamu.

Mnamo tarehe 6 Februari 2026,  saa 5:00 asubuhi  masaa ya Ulaya Mtandano huu wa Kimataifa, utafanya hija ya Maombi kupitia mtandaoni. Wakati wa tukio hilo la Kimataifa, lenye lengo la maombi na kuongeza uelewa dhidi ya biashara haramu ya binadamu, washiriki kutoka Ulaya, Afrika, Amerika, Asia, na Australia wataungana pamoja na ahadi ya kujitolea "kuwa sauti kwa ajili ya kaka na dada zetu, ambao wamedhalilishwa katika utu wao. Sote tuombe," (Papa Francisko, Sala ya Malaika wa Bwana, Februari 8, 2015).

Tupinge biashara haramu ya binadamu
Tupinge biashara haramu ya binadamu

Katika tukio hilo, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Bindamu, Kardinali Michael Czerny, S.J., atatoa tafakari kuhusu utu wa binadamu na wazo la kuwa karibu na waathiriwa wa biashara haramu ya binadamu. Maadhimisho ya Misa yatafanyika tarehe 8 Februari 2026 saa 1:00 jioni katika Basilika ya Mtakatifu Petro, mjini Vatican na baadaye kushiriki sala ya Malaika wa Bwana pamoja na Papa Leo XIV katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.

Kwa kutembelea maeneo rasmi na kurasa za mitandao ya kijamii zilizotengwa kwa ajili ya Siku ya Kimataifa majukwaa ya (Facebook na Instagram), unaweza kupakua mwongozo wa mkesha wa Februari 5 na kupata taarifa zaidi kuhusu siku ya maombi hayo tarehe 8 Februari 2026. Kwa kuunga mkono sherehe hii, tungependa kuwataja watangazaji wakuu, ikiwa ni pamoja na mtandao wa kimataifa wa kupambana na biashara haramu ya binadamu Talitha Kum, Umoja wa Kimataifa wa Mama Wakuu wa Mashirika ya Kitawa ya Kike  (UISG), na Umoja wa Wakuu wa Mashirika ya Kitawa ya Kiume (USG).

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here

05 Februari 2026, 10:09