Ratzinger na Kanisa linalokaribisha wakati likiacha uhuru
ANDREA TORNIELLI
"Kupitia mateso, alijifunza kumwacha aende zake mwenyewe, bila vikwazo. Alijifunza kuvumilia ukweli kwamba njia yake ilikuwa tofauti kabisa" na ile aliyoifikiria. Haya ni maneno kuhusu mama wa Mtakatifu Agostino, yaliyosemwa wakati wa kuwekwa wakfu kwa Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Monica katika wilaya ya Neuparlach ya Munich na Askofu Mkuu wa wakati huo Joseph Ratzinger. Ilikuwa tarehe 29 Novemba 1981, siku nne tu baada ya kutangazwa kwa uteuzi wake kama Mwenyekiti wa Baraza la kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Hii tena ni picha ya Ratzinger iliyo mbali sana na ile inayooneshwa na wale wanaotumia vifungu vilivyochaguliwa kutoka katika majisterio ya Benedikto XVI kujaribu kumtofautisha na ile ya warithi wake. Mahubiri haya yamechapishwa kwa mara ya kwanza kwa Kiitaliano katika Kitabu cha maandishi teule ya Ratzinger, "La fede del futuro" yaani “Imani ya wa wakati Ujao” (Cantagalli Editore, yaliyotafsiriwa na Pietro Luca Azzaro), yakiwa na utangulizi wa Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican.
Katika mahubiri yake, Askofu Mkuu wa Munich wa wakati huo anawasilisha umbo la mama yake Agostino kama uzoefu hai wa kile ambacho Kanisa lilivyo katika kiini chake cha ndani kabisa. "Ndani yake," Ratzinger anaandika, akimrejea Mtakatifu wa Hippo, "aliiona Kanisa kama mtu, Kanisa kibinafsi, ili kwake lisingekuwa tu kifaa, ambacho mtu anahisi kitu cha mbali sana, miundo ambayo haieleweki kwa kiasi fulani. Katika mwanamke huyu,kwa kile ambacho Kanisa lilivyo, kilikuwa kibinafsi." Kardinali , alikumbuka, kuwa gostino aliandika kuhusu mama yake kuwa: "Hakunipa uhai huu tu wa kimwili, lakini alinipa nafasi moyoni mwangu, alinipa nafasi maishani mwangu ambayo ningeweza kuwa mwanaume." Binadamu, Ratzinger alisema, "wanahitaji nafasi ya uhusiano ya uaminifu, ya upendo; na maana inayowaruhusu kutembea kuelekea wakati ujao." Lakini "nafasi hii ya kuishi" haina uhusiano wowote na miundo ya kikanisa au jamii zinazotegemea utambulisho wa watu wakamilifu wanaojitenga na ulimwengu, wakiulaani siku hadi siku. Hakika, inaonyesha vyema uso wa Kanisa linalokaribisha, linaloheshimu uhuru wa kila mtu na wakati wa kila mtu.
Kama vile Monica alivyofanya na mwanawe, akizingatia "kumwacha huru" kuwa "muhimu kwa ajili ya uundaji wa nafasi hii ya kuishi." Huru kufanya makosa, huru kufuata tamaa zake za kimwili... Monica "alijua jinsi ya kusubiri. Alijua jinsi ya kukubali mgogoro kati ya vizazi. Kupitia mateso, alijifunza kumruhusu atembee njia yake mwenyewe, bila vikwazo. Alijifunza kuvumilia ukweli kwamba njia yake ilikuwa tofauti kabisa na ile ambayo yeye, kwa imani, alikuwa amepanga kwa ajili yake; na bado alijifunza kumpenda, kuwa kando yake, kutomwacha, huku akimruhusu uhuru wa nafsi yake. Katika uwazi na matarajio haya, ambayo yalimruhusu uhuru wa kuwa yeye mwenyewe, sio kwa kumlazimisha imani, bali kwa kuwa pale kwa ajili yake kama mtu, kama mama, hivi ndivyo alivyompelekea imani.” Haya ni maneno ya kuelimisha kwa wazazi, kwa waelimishaji, na kwa ujumla zaidi kwa yeyote anayetangaza Injili. Kanisa kama "nafasi ya uzima, ya uhuru, ya matumaini."
Papa wa baadaye alitoa maoni: "Ninaamini kwamba leo kuna tuhuma nyingi na chuki dhidi ya Kanisa… kwa sababu tunapata Kanisa kidogo sana kama mtu, kidogo sana kama mtu. Tunasikia kumhusu kama muundo, ofisi, na kifaa pekee. Lakini Kanisa linaweza tu kudumu, na tunaweza kuota mizizi ndani yake, na linaweza kuwa nchi yetu, ikiwa tu litaendelea kudumu ndani ya watu. Nafasi hii, nafasi zote—hata vyumba ambavyo tunatumia muda wetu wa mapumziko na kukutana—vinapaswa kuwa nafasi zinazotusaidia kuwa Kanisa ana kwa ana kwa kila mmoja; nafasi ambayo ni nafasi ya kuishi kwetu, mama, mtu anayetupatia mahali pa kuaminiana na uwezekano wa kuishi. Kanisa ambalo ni "hospitali ya kambini, inayokusindikiza, ambapo upendo huponya majeraha ya ndani kabisa na unajisikia uko nyumbani.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here