Tafuta

2026.02.08 Kardinali  Pietro Parolin katika Madhabahu ya Monte Berico huko Vicenza. 2026.02.08 Kardinali Pietro Parolin katika Madhabahu ya Monte Berico huko Vicenza. 

Kard.Parolin:Maria anatufundisha kuponya kutokana na hisia ya ubora inayotutenganisha

Katibu Mkuu wa Vatican aliongoza Misa takatifu alasiri,Februari 8,katika Madhabahu ya Bikira Maria huko Monte Berico,Vicenza ili kuzindua Mwaka wa Jubilei ya Mama Maria,miaka 600 tangu alipotokea kwa mara ya kwanza katika mlima huo.Kardinali alihimiza kugundua upya shule halisi ya ubinadamu ambayo,kwa kumtazama Maria,huponya mji kutokana na uadui wa kijamii ambao,kama tauni,huua mwili na roho.

Alvise Sperandio - Vicenza na Angella Rwezaula – Vatican.

Miaka mia sita iliyopita, ambapo ilikuwa mnamo tarehe 7 Machi 1426, Bikira Maria alitokea mkulima  moja Vincenza Pasini kwenye Monte Berico, ambacho ni kilima kinachoelekea  jiji la Vicenza.  Na wakati janga la Tauni ikiendelea wakati huo na kuifanya  jiji lipige magoti, iliisha. Tangu wakati huo, waamini hupanda kilima, si tu katika tarehe 8 Septemba  ya  kila mwaka katika siku ya Kuzaliwa kwa Maria, bali wamekuwa wakifanya hija yao kwenye madhabahu iliyojengwa hapo, na kuwekwa wakfu kwa Bikira wa Huruma ambayo inasimamiwa na Ndugu wa Shirika la Watumishi wa Maria. Kwa njia hiyo,  Dominika tarehe 8 Februari 2026 wakati wa Maadhimisho ya Misa Takatifu, Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, mzaliwa wa Schiavon, katika Jimbo hilo la Vicenza, alifungua Mwaka wa Jubilei hiyo.

Bikira Maria anatuonesha njia ya kushiriki na mshikamano

Mamia ya waamini walikuwepo kanisani, wengine nusu elfu nje, mbele ya skrini kubwa iliyowekwa kwenye Uwanja wa Vittoria. Maaskofu wanne walimzunguka Kardinali kwenye madhabahu: Padre Giuliano Brugnotto, Paroko wa Vicenza; Askofu Mstaafu Beniamino Pizziol wa Vicenza na Askofu Mstaafu Adriano Tessarollo wa Chioggia; na Askofu Claudio Dalla Zuanna wa Jimbo la Beira nchini Msumbiji. Mapadre Kadhaa, takriban watu mia moja wenye mamlaka na wanasiasa, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Veneto, Alberto Stefani, Mkuu wa Wilaya, Andrea Nardin, na Meya wa mji mkuu huo, Giacomo Possamai na watu wengi wa kawaida.

Madhabahu ya Monte Berico, Vincenza
Madhabahu ya Monte Berico, Vincenza

Katika mahubiri Kardinali alitoa wito kuwa "Maria anatualika tumruhusu Mungu azungumze katika Kristo. Anatualika tuwe na mtazamo wa ukimya wa ndani unaomaanisha uwezo wa kusikiliza sauti ya Bwana. Ni kwa njia hiyo tu Vicenza, eneo la Veneto, na wale wote wanaokuja hapa kama mahujaji Mwaka huu wa Jubilei wataweza kufungua 'milango mingi iliyofungwa' na kuruhusu historia nyingi zilizovunjika na zisizokamilika kuanza upya, na kutoa nafasi kwa usawa huo mkubwa unaoponya hisia ya ubora unaotutenganisha."

Kongamano la Kimataifa la Maria

Waamini walikusanyika katika Madhabahu  kuanzia wakati wa chakula cha mchana, wengi wakifika kwa miguu, wakipanda chini ya varanda zinazopepea kutoka jiji chini ya Mlima Berico. Ibada ilianza saa 9:00 alasiri, ikitanguliwa na Kongamano la Kimataifa la Maria, likiongozwa na kauli mbiu:"Maria, Mama wa Huruma kati ya Ucha Mungu wa Watu na Kuzaliwa Upya kwa Jumuiya." Kardinali Parolin aliyekaribishwa na Askofu Brugnotto wa Vicenza alianza kusema: "Maria atuoneshe njia ya kushiriki na mshikamano. Tumepanda kilima hiki ili kuhisi uwepo wa mama wa Maria na kukubali mwaliko wake wa kusikiliza sauti ya Mwanawe Yesu. Kwake tunawasilisha matamanio ya haki na amani yanayotokana na watu wetu wa Vicenza na kutoka kwa wengine wengi."

Kardinali Parolin katika Madhabahu ya Monte Berico, Vincenza
Kardinali Parolin katika Madhabahu ya Monte Berico, Vincenza

Kardinali Parolin: Shukrani kwa Maria, uponyaji kamili

Katika mahubiri yake, Kardinali Parolin alikumbuka historia ya miaka mia sita ya Madhabahu hayo  kuwa ni "historia ya matumaini, maisha, mabadiliko, na kuzaliwa upya." Akisisitiza kwamba "Mama wa Yesu ndiye mwanzo wa Kanisa la waliofufuka," aliongeza kwamba "msingi wa kile Vicenza na Veneto walichopitia wakati huo na wanachoitwa kupitia leo" ni kifungo "ambacho Mungu alitaka kuanzisha kati ya kiumbe wa kwanza aliyefufuka na ubinadamu katika safari yake kupitia wakati na historia." Katibu Mkuu wa Vatican alikumbuka kwamba "kumruhusu Mungu kuzungumza katika Kristo kupitia Mama yake Mtakatifu sana ,  kuliipatia uhuru kutokana na tauni: uhuru wa kufikiria na kufanya kila kitu ambacho tauni ilizuia, uhuru wa kuishi maisha ya kila siku kuanzia kifo. Ilikuwa uponyaji kamili, wa miili na roho."

Shule ya ubinadamu, kuponya mji kutokana na uadui wa kijamii

Hata leo, maneno ya kibinadamu yanatamani kuwafanya miili na roho kuwa watumwa, na hata leo "tumeitwa kumruhusu Mungu azungumze katika Kristo ili historia ya uhuru iweze kuandikwa katika wakati uliopo, ambapo kila mtu anaona jina lake na nafasi yake katika jamii ikiheshimiwa, ikikuzwa, na kukubalika. Kiukweli, hii pekee ndiyo inayoweza kutoa mustakabali ambapo kuna nafasi kwa kila mtu na si kwa baadhi tu." Kardinali Parolin alisisitiza kwamba "tunapomruhusu Mungu azungumze katika Kristo, jana kama leo, kila mtu hugundua upya haki ya kuzungumza na haki ya uraia, kwa sababu wote hurejeshwa kwenye wito wao wa asili na wa pamoja wa kuwa mashahidi wa ukweli. Hii husababisha uponyaji wa kuishi pamoja, ambao kutokana na kuwa 'ujumbe usiowezekana' kwa wengi unakuwa ufunguo wa kufikia mustakabali wa wote." Hata leo, Kardinali Parolinalisema, lazima tugundue upya "shule hiyo halisi ya ubinadamu ambayo, ikimtazama Maria, huponya mji kutokana na uadui wa kijamii unaoua, kama tauni, mwili na roho, ikimtenga kila mtu katika hofu na ndoto zao mbaya."

Kardinali Parolin Tumaini kwa Ukraine na Olimpiki ni fursa ya udugu."

Kando ya sherehe hiyo, Kardinali Parolin, akichochewa na waandishi wa habari, na alikumbuka uhusiano wake binafsi na Mlima Berico: "Mama yetu amekuwa akinisindikiza kila wakati, katika nyakati nzuri na mbaya, katika maisha yangu yote, ambayo, licha ya matatizo yote, yamefanyika nje ya Jimbo  kama Askofu, Balozi wa Vatican, na Kadinali. "Nimejitolea sana mahali hapa salama, ambapo mimi hurudi kila wakati kwa furaha." Akitazama matukio ya sasa na hali ya kimataifa ya kijiografia, Katibu Mkuu  alisema: “Wito wa diplomasia ya Vatican na Vatican ni kufanya kazi katika huduma ya amani, kuanzia na mamlaka kuu ya Papa na kujitolea kila siku kuzuia, kupatanisha, na kutafuta kutatua migogoro mara tu, kwa bahati mbaya, itakapotokea." Kuhusu kuanza tena kwa mazungumzo nchini Ukraine, aliendelea: "Bado tunatumaini kwamba tunaweza kufikia mwisho wa vita.

Kardinali Parolin alishiriki hafla ya ufunguzi wa Olimpiki Milano-Cortina
Kardinali Parolin alishiriki hafla ya ufunguzi wa Olimpiki Milano-Cortina

Majaribio mengi yamefanywa, karibu itakuwa tamaa, lakini tunataka kuthibitisha tena matumaini yetu. Ukweli kwamba mazungumzo yanafanyika tayari ni muhimu sana. Hitimisho bado halijaonekana." Maoni ya mwisho, hatimaye, kuhusu Olimpiki ya Majira ya Baridi iliyoanza huko Milano-Cortina: Jumamosi tarehe 17 Februari 2026 ambapo Kardinali pia aliudhuria hafla ya ufunguzi wa Michezo katika mji mkuu wa Lombardia, kwa mara ya kwanza kihistoria ambayo Katibu wa Vatican kuudhuria. Akikumbuka ujumbe wa Papa Leo XIV, Kardinali Parolin alisisitiza "thamani ya michezo kama ujumbe wa amani na maelewano, kama fursa ya udugu" na akarudia wito wa "kuheshimu makubaliano ya amani ya Olimpiki ambayo huzingatiwa kiutamaduni."

KARD.PAROLIN -VINCENZA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here.

09 Februari 2026, 09:55