Chiclayo,Kard.Czerny:Kuwa karibu na mgonjwa hupelekea uongofu wa moyo
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo fungamani ya Binadamu, aliongoza misa Takatifu katika Madhabahu ya mama Yetu wa Amani huko Chiclay nchini Peru katika fursa ya Maadhimisho ya Siku ya XXXIV ya Wagonjwa Duniani, tarehe 11 Februari 2026, sanjari na Siku kuu ya Bikira Maria wa Lourdes. Baba Mtakatifu Leo XIV alimtuma mwakilishi wake katika Siku hii muhimu. Kwa kutazama hali ya siku hii, Kardinali alisisitiza juu ya kuwa karibu sana na wale wanaoteseka na magonjwa kwamba husababisha uongofu wa moyo, huunda jumuiya na ni udhihirisho halisi wa upendo kwa Mungu.
Upendo si wazo unaweza kutoa uzima, afya na wokovu
Akisoma tena Ujumbe wa Papa Leo XIV kuhusiana na tukio hilo wenye mada, "Huruma ya Msamaria: Kupenda kwa Kuvumilia Maumivu ya Mwingine," Kardinali, Czerny mzaliwa nchi ambayo Papa alihudumia kama askofu, alisisitiza kwamba aina hii ya upendo haiwezi kupunguzwa kuwa wazo tu, matunda ya tafakari za kitaalimungu au kijamii." Bali tunaweza kuzungumza kuhusu upendo huu, kuanzia tu uzoefu wetu binafsi na imani, na pia kupitia kumbukumbu angavu ya matukio ambayo tumeshuhudia upendo huu ukifanya kazi. Kardinali aidha alirejea watu wa kibiblia waliokumbukwa katika liturujia ya siku, wakiwa wameungana, kwa upendo ule ule ambao unaweza kutoa uzima, afya, na wokovu,"na ambao tunapaswa kushukuru.
Upendo ni uongofu na Maria ni msukumo na mwalimu wao
Upendo ni mchakato wa uongofu, kwa maana halisi ya neno. Unahusisha kutazama kwa macho ya Mungu,kutoridhika na kutangaza unabii mbaya au kutangaza utambuzi wa kusikitisha, lakini badala yake kuwa tayari kubadilisha mwelekeo, kuegemea kwa matumaini, tena na tena, kwa wengine. Mtazamo huu pia unafaa kama gundi la kijamii, kwani huunda jumuiya, alisisitza Mtawa wa Kijesuit. Na, kwa kumbukumbu ya Mama Yetu wa Lourdes, Kardinali Czerny aliakisi kile kinachotokea ndani ya mipaka ya hifadhi hiyo ya Ufaransa, iliyojaa maumivu na matumaini ya wokovu wa wanaume na wanawake wengi. Katika utofauti wa huduma zao, zilizounganishwa na mahitaji ya kila mgonjwa, kwa pamoja wanaweza kutoa zaidi ya vile mtu anavyoweza kutarajia kutoka kwa kila mmoja wao peke yake. Maria ndiye msukumo na mwalimu wao.
Zaidi ya Ubinafsi ni upendo wetu kwa Mungu
Kuweza kushirikiana na wengine kwa manufaa ya wote, na hasa walio katika mazingira magumu zaidi: hii ndiyo zawadi ambayo Kardinali Czerny aliwaalika kuomba. “Kwa kutoa kile ambacho kila mmoja wetu anaweza na kushinda jaribu la kutokuwa na imani au, wakati mwingine, ubinafsi wa kiburi unaotutenga na kaka na dada zetu katika dhamira ya kuwatunza wale wanaohitaji zaidi." Kwa kuhitimisha aliwaeleza kuwa “Msisahau kamwe, kwamba upendo wetu kwa wengine daima ni usemi halisi wa upendo wetu kwa Mungu na kwamba, kinyume chake, hatuwezi kusema au kufikiria kwamba tunampenda Mungu bila kutembea katika njia ya upendo.”
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here