Tafuta

Sr Simona Brambilla Sr Simona Brambilla  

Papa amemteua Sr Brambilla na kuwathibitisha wajumbe wa Baraza la Kipapa la Maaskofu

Sr Simona Brambilla, M.C.,Mwenyekiti wa Baraza la Kpapa la Mashirika ya Wakfu na Vyama vya Kitume ameteuliwa na Papa,Februari 14 na kuthibitisha wajumbe wa Taasisi za Curia Romana katika Baraza la Kipapa la Maaskofu.

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV Jumamosi tarehe 14 Februari 2026 amemetuwa mjumbe mpya kwa ajili ya  Baraza la Kipapa la Maaskofu, Sr Simona Brambilla, M.C., ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Wakfu na Vyama vya Kitume. Sista Brambilla, ambaye atatimiza miaka sitini na moja Machi 27, amekuwa Mkuu Mwenyekiti wa  Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maisha ya Wakfu na Vyama vya Maisha ya Kitume tangu mnamo Januari 2025. Yeye anakuwa Mtawa wa pili katika ujumbe huo, akiwa pamoja na  Sr Raffaella Petrini, rais wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya Serikali ya Jiji la Vatican na Gavana wa Mji wa Vatican, lakini  vile vile katika ujumbe huo kuna  Mlei mwanamke,  Bi Maria Lia Zervino, rais wa zamani wa Umoja wa Mashirika ya Wanawake Wakatoliki Duniani, (WUCWO), aliyeteuliwa na Papa Francisko kama wajumbe wa Baraza la Maaskofu mnamo Julai 2022 na kuthibitishwa tena tarehe 14 Februari na Papa Leo XIV. Kwa pamoja, wanaitwa kushiriki katika mchakato wa kuwachagua wachungaji wapya maskofu  wa majimbo Katoliki duniani.

Kwa njia hiyo wengine waliothibitishwa kutoka Taasisi za Curia Romana kuwa wajumbe wa Baraza hilo la Maaskofu ni: Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican; Kardinali Kurt Koch, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Kikristo; Kardinali João Braz de Aviz, Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Maisha ya Wakfu na Vyama vya Kitume; Askofu Mkuu Sérgio da Rocha, wa Jimbo Kuu la São Salvador da Bahia (Brazili); Askofu Mkuu Blase Joseph Cupich, wa Jimbo Kuu la Chicago(Marekani); Askofu Mkuu Joseph William Tobin, C.SS.R., wa Jimbo Kuu la Newark(Marekani); Askofu Mkuu Juan José Omella Omella, wa Jimbo Kuu la Barcelona (Hispania), Askofu  Anders Arborelius, O.C.D., wa Jimbo la Stockholm (Sweden); Askofu Mkuu Jose F. Advincula, wa Jimbo Kuu la Manila (Ufilippino); Askofu Mkuu Augusto Paolo Lojudice, wa Jimbo Kuu la Siena-Colle ya Val d’Elsa-Montalcino na Askofu wa Montepulciano-Chiusi-Pienza (Italia); Askofu Mkuu Jean-Marc Aveline, wa Jimbo Kuu la Marseille(Ufaransa); Askofu Oscar Cantoni, wa Jimbo la Como (Italia); Askofu Mkuu Grzegorz Ryś, wa  jimbo Kuu Kraków (Poland); Askofu Mkuu José Cobo Cano, wa Jimbo Kuu la Madrid (Hispania); Kardinali José Tolentino de Mendonça, Mwenyekiti wa Baraza la kipapa la Utamaduni na Elimu; Kardinali Mario Grech, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu; Kardinali Arthur Roche, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Nidhamu na Sakramenti za Kanisa; Kardinali Lazzaro You Heung-sik, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makleri; Kardinali Claudio Gugerotti, Mwenyekiti wa Baraza la kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki;

Kardinali Víctor Manuel Fernández, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mafundisho Tanzu ya Kanisa; Askofu Mkuu Paul Emil Tscherrig, Balozi wa Vatican, Kardinali Rolandas Makrickas, Mkuu wa Basilika ya Kipapa ya Mtakatifu Maria Mkuu; Askofu Mkuu Dražen Kutleša, wa Jimbo Kuu la Zagreb (Kroatia); Askofu Mkuu Jorge Ignacio García Cuerva, wa Jimbo Kuu la  Buenos Aires (Argentina); Askofu Felix Genn, Mstaafu wa Jumbo la Münster (Germania); Askofu Paul Desmond Tighe, Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu; Askofu José Antonio Satué Huerto, wa Jimbo la  Málaga (Hispania;  Padre Donato Ogliari, O.S.B., Abati wa Manasteri ya Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

14 Februari 2026, 12:37