Tafuta

Askofu mkuu Giorgio Lingua Balozi wa Vatican nchini Israeli na Mwakilishi wa Kitume wa Vatican Mjini Yerusalemu na Palestina. Askofu mkuu Giorgio Lingua Balozi wa Vatican nchini Israeli na Mwakilishi wa Kitume wa Vatican Mjini Yerusalemu na Palestina.  (Župa Krašić)

Askofu Mkuu Giorgio Lingua Balozi wa Vatican Nchini Israeli, Mwakilishi wa Kitume Yerusalemu na Palestina

Askofu mkuu Lingua alizaliwa tarehe 23 Machi 1960 huko Fossano, Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 10 Novemba 1984 akapewa Daraja takatifu ya Upadre. Baba Mtakatifu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu mkuu na hatimaye kuwekwa wakfu tarehe 9 Oktoba 2010 na Kardinali Tarcisio Pietro Evasio Bertone aliyekuwa Katibu mkuu wa Vatican wakati ule. Kimsingi Askofu mkuu Lingua alianza huduma ya kidiplomasia mjini Vatican mwaka 1992.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 22 Januari 2026 amemteua Askofu mkuu Giorgio Lingua kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Israeli na Mwakilishi wa Kitume Mjini Yerusalemu na Palestina. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Lingua alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Croatia. Amewahi pia kuwa Balozi wa Vatican nchini: Cuba, Iraq na Yordan ambako ameshuhudia mateso na mahangaiko ya Wakristo kutokana na nyanyaso na dhuluma za kidini na kiimani, lakini wakati wote amejitahidi kuwa ni rejea ya matumaini kwa wale waliopondeka na kuvunjika moyo.  Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Lingua alizaliwa tarehe 23 Machi 1960 huko Fossano, Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 10 Novemba 1984 akapewa Daraja takatifu ya Upadre.

Papa Leo XIV akizungumza na viongozi wa Serikali ya Israeli
Papa Leo XIV akizungumza na viongozi wa Serikali ya Israeli   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu mkuu na hatimaye kuwekwa wakfu tarehe 9 Oktoba 2010 na Kardinali Tarcisio Pietro Evasio Bertone aliyekuwa Katibu mkuu wa Vatican wakati ule. Kimsingi Askofu mkuu Lingua alianza huduma ya kidiplomasia mjini Vatican kunako mwaka 1992. Tangu wakati huo ametekeleza utume wake sehemu mbalimbali za dunia kama vile: Pwani ya Pembe, Marekani, Serbia na Italia. Amewahi pia kufanya kazi katika Sekretarieti Kuu ya Vatican kwenye Idara ya mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican na alijikita zaidi katika masuala yaliyokuwa yanazihusu nchi za Amerika ya Kusini na Caribbeani.

Uteuzi Israeli
01 Februari 2026, 16:26