Tafuta

Wamisionari waliokufa wakitoa ushuhuda kwa Yesu. Wamisionari waliokufa wakitoa ushuhuda kwa Yesu. 

Wamisionari na Wahudumu wa Kichungaji Walioawa mwaka 2025

Sauti za kimya za wamisionari na wachungaji waliouawa ni tumaini lililojaa hali ya kutokufa kwani ushahidi wao unaishi kama unabii na ushindi wa mema juu ya uovu.Shirika la habari Kipapa la Habari za Kimisionari Fides lilitoa ripoti yake ya kila mwaka na ambayo inayoaelezea wamisionari wa Kikatoliki na mapadre waliouawa ulimwengunu kote mwaka 2025 kwa ajili ya ushuhuda wa imani yao kwa Kristo.

Na Sr  Christine Masivo, CPS – Vatican.

Ripoti kutoka Shirika la Kipapa la habari  za kimisionari  Fides,  ilitoa taarifa  kuwa hata tumaini la wamisionari na wahudumu wa uchungaji wanaokufa ni "tumaini lililojaa kutokufa, kwa sababu ushuhuda wao unabaki kama unabii wa ushindi wa mema dhidi ya maovu." Hii ni moja ya misemo ambayo Papa Leo XIV alichagua kuanzisha ripoti ya kawaida iliyochapishwa mwishoni mwa mwaka ya Shirika hili la kimisionari Fides kuhusu wamisionari Wakatoliki na wahumu wa kichungaji waliouawa ulimwenguni kote . Inaonyesha chanzo tu cha tumaini la Kikristo, ahadi ya maisha ambayo hayafi kamwe.

Waliouawa waslishuhuda Kristo katika shughuli za kawaida

Taarifa chache kuhusu wasifu wao na mazingira ya vifo vyao zinaonesha tena mwaka huu kwamba wamisionari waliouawa hawakuwa katika mwanga wa matukio ya kusisimua. Walimshuhudia Kristo katikati ya shughuli za maisha ya kila siku, hata walipofanya kazi katika mazingira yaliyojaa vurugu na migogoro, na huduma za kijamii. Walikufa katika majukumu ya kawaida. Kwa mujibu wa Shirika hili, wamisionari 17 waliuawa duniani kote mwaka 2025, wakiwemo mapadre, watawa, waseminaristi na wahudumu walei. Afrika ilirekodi idadi kubwa zaidi ya vifo, ambapo wamisionari kumi waliuawa, wakiwemo mapadre sita, waseminari wawili, na makatekista wawili.

Nchi za Amerika, Asia na Afrika 

Nchi za Amerika zilirekodi vifo vinne, vilivyohusisha mapadre wawili na watawa wawili. Asia ilichangia vifo vya watu wawili, Padre mmoja na Mlei mmoja, huku Ulaya ikirekodi Padre mmoja aliyeuawa katika mwaka huo 2025. Barani Afrika, watano kati ya kumi walitoka Nigeria, wawili Burkina Faso na mmoja Sierra Leone, Kenya na Sudan. Watawa wawili waliuawa Amerika, huko Haiti, Padre mmoja huko Mexico na Padre mmoja wa asili ya Kihindi huko Amerika. Huko Asia, Padre mmoja aliuawa huko Myanmar na mwingine Ufilipino na huko Ulaya, Padre aliuawa huko Poland. Miongoni mwa waliouawa ni Emmanuel Alabi, mseminaristi kutoka Nigeria aliuawa baada ya kutekwa nyara wakati wa shambulio kwenye Seminari  Ndogo huko Ivianokpodi, Nchini Haiti Sr. Evabette Onezaire na Sr Jeanne Voltaire waliuawa huku kukiwa na vurugu zinazoendelea zinazohusishwa na magenge yenye silaha. Huko Mayanmar, Donald Martin Padre wa kwanza wa eneo hilo kuuawa wakati wa mzozo wa wenyewe kwa wenyewe unaoendelea na mwili wake kuokotwa na washiriki wa Jumuiya ya Parokia yake.

Wamisionari na Mpadre 626 wameuawa kuanza 2000 hadi 2025

Kulingana na  Shirika la Fides, kuanzia mwaka 2000 hadi 2025, jumla ya wamisionari wa Kikatoliki na mapadre 626 waliuawa ulimwenguni kote. Vifo hivi ni ushuhuda endelevu na mbegu zitakazoota na kuzaa matunda kupitia kwao, zikibadilisha mioyo kuokoa wote.

“Kaka na dada hawa wanaweza kuonekana kama wameshindwa, lakini leo tunaona kwamba sivyo ilivyo. Sasa, kama wakati huo, mbegu ya sadaka zao, ambayo inaonekana kufa, inachipuka na kuzaa matunda, kwa sababu kupitia kwao Mungu anaendelea kufanya maajabu, kubadilisha mioyo na kuwaokoa wanadamu" (Papa Francisko, Desemba 26, 2023, sikukuu ya kiliturujia ya Mtakatifu Stefano).

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

03 Januari 2026, 11:31