Tafuta

2026.01.09 Kampeni ya Vyombo vya Habari Kimataifa kuhusu Akili Unde. 2026.01.09 Kampeni ya Vyombo vya Habari Kimataifa kuhusu Akili Unde. 

Vyombo vya habari vya kimataifa vinadai uwazi kutoka makampuni makubwa ya AI

"Ukweli ndani na ukweli nje:"Ni Kauli mbiu ya Kampeni ya kimataifa inayotaka uaminifu wa taarifa kuwekwa katikati ya maamuzi ya makampuni makubwa ya Akili Unde(AI).Watu wengi zaidi wanatumia zana za AI kupata habari,lakini mara nyingi hizi hupotoshwa au kutengwa kutoka katika vyanzo vya asili.Kwa hiyo vyombo vya habari vinayataka makampuni makubwa ya mapinduzi ya kidijitali kuchukua hatua ya uwajibikaji.

Alessandro Gisotti

Ni wakati wa makampuni makubwa ya AI(big companies),Akili Unde kushirikiana na vyombo vya habari kuhusu suala la uwazi wa vyanzo na matumizi ya maudhui ya taarifa. Hili ndilo ambalo vyama vikubwa vya habari duniani vinalitaka katika kampeni inayoitwa "Ukweli ndani, Ukweli Nje." Mpango huu unaungwa mkono na Umoja wa Vyombo vya Utangazaji vya Ulaya(EBU), (ambapo Radio Vatican ni mwanachama mwanzilishi wake), Chama cha Wachapishaji Habari Duniani(WAN-IFRA), na Shirikisho la Kimataifa la Wachapishaji wa Mara kwa Mara(FIPP). Kampeni hiyo ilichochewa hasa na ripoti ya BBC na EBU "Uadilifu wa Habari katika Wasaidizi wa Akili Unde(AI.)" Utafiti huu, uliochapishwa mnamo Juni 2025, ulionesha jinsi ambavyo zana za AI, bila kujali kijiografia, lugha, au jukwaa, zinavyorekebisha kimfumo, huondoa muktadha, au kudhibiti habari kutoka katika vyanzo vya kuaminika kama vile tovuti za vyombo vya habari.

 Zana za AI bado si chanzo cha habari kinachoaminika

Kwa mujibu Liz Corbin, Mkurugenzi wa Habari wa EBU, alisema, “Ingawa zina nguvu na matumaini, Akili Ude” bado si chanzo cha habari na taarifa kinachoaminika, na tasnia ya Akili Unde(AI)haishughulikii suala hili kama kipaumbele." Kwa hivyo,  ndiyo maana ya wito wa kujiunga na kampeni ya "Ukweli ndani, Ukweli nje," ili kushughulikia haraka suala la uwazi wa chanzo. Uaminifu wa uandishi wa habari uko hatarini, alisema Vincent Peyregne, mkuu wa Chama cha Wachapishaji wa Habari Duniani. "Ikiwa zana zinazoendeshwa na Akili Unde(AI), zinakusanya ukweli uliochapishwa na vyanzo vya habari vyenye mamlaka, basi zinapaswa kurudisha ukweli kwenye chapisho. Lakini leo," analalamika Peyregne, "hili halifanyiki." Watangazaji wa kampeni hiyo wanasema kwamba watu wengi zaidi wanatumia majukwaa ya AI kama njia ya kupata habari.

Na zana hizi zinapobadilisha, kurekebisha, au hata kughushi taarifa, matokeo yake ni mmomonyoko mkubwa wa uaminifu katika vyombo vya habari, jambo ambalo si muhimu kwa utendaji kazi nzuri za mfumo wa kidemokrasia. Hii ndiyo sababu, inarudiwa, suala hilo lazimalishughulikiwe haraka, hasa ikizingatiwa kwamba matumizi ya AI kupata taarifa yataongezeka tu katika miaka ijayo, hasa miongoni mwa vizazi vijavyo.

Kanuni Tano za Uwazi wa Taarifa za AI

Kampeni ya "Ukweli Ndani, Ukweli Nje" ni sehemu ya mpango mpana wa Uadilifu wa Habari katika Enzi ya Akili Unde(AI,) ambao unafafanua kanuni tano za msingi zinazolenga makubwa ya AI:

1) "Hakuna Ridhaa, Hakuna Maudhui." Maudhui ya uandishi wa habari yanaweza kutumika katika mifumo ya AI pekee kwa idhini ya mchapishaji wa awali.

2) "Sifa Sahihi." Thamani ya uandishi wa habari unaoaminika lazima itambuliwe wakati maudhui yanatumiwa na wengine.

3) "Usahihi, sifa, na asili." Chanzo asili cha maudhui yoyote yanayozalishwa na AI lazima kionekane wazi na kiweze kuthibitishwa.

4) "Wingi na utofauti." Mifumo ya Akili Unde lazima ioneshe utofauti wa mfumo ikolojia wa habari duniani.

5) "Uwazi na mazungumzo." Kampuni za teknolojia lazima zishirikiane na mashirika ya vyombo vya habari ili kukuza viwango vya pamoja vya usalama, usahihi, na uwazi. Kuanzia kanuni hizi, lengo ni kufanya kazi pamoja kwa ajili ya taarifa za kweli na za kuaminika. Kwa upande wa Liz Corbin wa EBU, "Sio suala la  kunyoosheana vidole, bali kuhusu kushiriki katika mazungumzo yenye kujenga. Umma una haki ya kupata uandishi wa habari bora na wa kuaminika, bila kujali teknolojia inayotumika."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

 

09 Januari 2026, 15:48