Tafuta

Basilika ya  Mtakatifu Maria Mkuu. Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu.  (@Vatican Media)

Papa amteua Alí Herrera kuwa Makamu wa Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu!

Tangu mwaka 2024,Askofu wa Colombia alikuwa Katibu wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto ambaye atachukua nafasi ya Kuwa Makamu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu(Santa Maria maggiore),Roma.

Vatican News

Papa Leo XIV tarehe 15 Januari 2026, alimteua Askofu Luis Manuel Alí Herrera, ambaye hadi uteuzi alikuwa katibu wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto, kuwa Makamu  Mkuu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu(Santa Maria Maggiore).

Awali alikuwa Askofu msaidizi mstaafu wa Bogotá nchini Colombia, na mwanasaikolojia anayejulikana kwa kujitolea kwake katika ulinzi wa watoto, Herrera ambaye aliteuliwa kuwa katibu wa Tume ya Ulinzi wa Watoto na Watu Wazima Walio katika Mazingira hatarishi mnamo Machi 2024. Ataendelea na wadhifa huu baada ya uteuzi wake kuwa Makamu Mkuu tarehe 15 Januari 2026.

Katika Kanisa Kuu la Liberia, yaani la Mtakatifu Maria Mkuu,  Askofu Alí ​​​​Herrera atashirikiana na Kardinali Rolandas Makrickas, Mkuu wa Kanisa Kuu hilo.

Makamu mpya wa Basilika ya Mt.Maria Mkuu

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

 

15 Januari 2026, 17:01