Tafuta

 Dorothy Day,kama mlei alijumuisha utendaji mkali wa upendo kiinjili.Alikuwa imara na mwenye kupenda changamoto,na imani yake ilifungamana na migongano ya wakati wake. Dorothy Day,kama mlei alijumuisha utendaji mkali wa upendo kiinjili.Alikuwa imara na mwenye kupenda changamoto,na imani yake ilifungamana na migongano ya wakati wake. 

Maisha na maneno ya Dorothy Day yalionesha mfano uliojikita katika tumaini hai

Historia nzima ya Dorothy Day,mwanamke wa Marekani aliyejitolea maisha yake yote kwa ajili ya haki ya kijamii na haki za watu,hasa maskini,wafanyakazi walionyonywa, waliotengwa na jamii,aliyetangazwa kuwa Mtumishi wa Mungu mnamo mwaka 2000 ni ushuhuda wa kile ambacho mtume Mtakatifu Yakobo tayari alidai katika Barua yake kwamba:“Nioneshe imani yako bila matendo,nami nitakuonesha imani yangu kwa matendo yangu”(2:18).

Na Ritanna Armeni na Angella Rwezaula - Vatican

Mtu anaponukuliwa katika hotuba kwa umma siyo kwa bahati mbaya. Wakati hotuba imetolewa na Papa, nukuu za watu ni za muhimu na kwa malengo stahiki. Katika Katekesi za  Jubilei kwa siku za hivi karibuni,  Papa Leo XIV, aliamua kuchagua kumbukumbu ya Dorothy, aliyemwelezea kama “mtu mdogo lakini wa maana sana kwa wanawake wa Marekani, kwani alikuwa na moto ndani yake.” Hili lilikuwa chaguo muhimu la Papa Leo XIV  lililodhihirisha nia ya wazi na ya makusudi kufanya hivyo. Dorothy (1897- 1980) alikuwa mwandishi wa habari, na mwanaharakati Mkatoliki. Alikuwa pia mwanzilishi, wa chama cha wafanyakazi wakatoliki kilichoanzishwa mwaka 1933, kwa kushirikiana na Peter Maurin, kwa lengo la kuwasaidia watu wasio na makazi na maskini huko New York nchini Marekani. Chama hicho kilienea kwa kasi katika majiji ya Marekani, Canada, na Uingereza.

Utendaji wa upendo Kiinjili

Zaidi ya hayo, Dorothy, kama mlei alijumuisha utendaji mkali wa upendo kiinjili. Alikuwa imara na mwenye kupenda changamoto, ambaye imani yake ilifungamana na migongano ya wakati wake, mkosoaji wa kijamii na mshiriki wa masuala ya kisiasa, na kujitoa kuwasaidia waliotengwa kwa kutafakari kwa kina utu wa mwanadamu. Alikuwa mwanaharakati aliyejitoa kwa dhati katika vita mbili kuu za dunia, na bila kuchoka alikosoa jamii iliyokuwa imetawaliwa na ubinafsi na ushindani. Ni ngumu kukwepa maoni kwa kumnukuu, Papa Leo XIV alitaka kuonesha mwelekeo. Papa alisisitiza kuwa katika kulijenga Kanisa, mchango wa Walei kwa namna yoyote siyo mbadala. Badala yake unaweza kuwa sehemu ya kufanya maamuzi, kama ilivyokuwa kwenye mchango wa Dorothy.

Injili iingie katika jamii, Ijenge na kubadilisha matendo ya kila siku

 

Papa Leo  alihimiza kuwa Injili haipaswi kuishia katika kutoa faraja, badala yake iingie katika jamii, ijenge na kubadilisha, lazima iingizwe kwenye matendo ya kila siku. Dorothy aliamua kuishi maisha yake hadi mwisho katika nyumba ya ukarimu wa wafanyakazi wakatatoliki. Maisha na maneno yake yalionesha mfano wake uliojikita katika tumaini hai, ushiriki wa kijamii na huduma kwa maskini, ambayo inabaki kuwa kitovu kwa kanisa la leo. Dorothy Day ”, alisema Papa Leo XIV, inaonesha msimamo. Aliona kuwa mwenendo wa maendeleo wa nchi yake, haukutoa nafasi sawa kwa kila mtu; alielewa kuwa ndoto hii ilikuwa kitu kisichofikiwa kwa walio wengi, ndiyo maana kama Mkristo aliamua kujihusisha na wafanyakazi, wahamiaji na wale walioumizwa na hali mbaya ya uchumi.”

Amani siyo ya kufikirika bali ni zoezi la kila siku

Kwa kuhitimisha, Papa Leo XIV alisema kuwa Amani siyo jambo la kufikirika, bali ni zoezi la kila siku. Dorothy alichukua jukumu hili kwa ujasiri hasa katika kipindi cha miaka ya giza ya “Nazism”, wakati wote wa vita vya pili vya dunia, na baadaye katikati ya vita baridi. Katika kipindi kilichogubikwa na vita, migogoro ya kimataifa, ongezeko la kukosekana usawa, mgawanyiko wa kisiasa, mfano wake haotoi tu unga’o bali huelekeza kwenye njia thabiti, inayodai na thabiti kufuata.”

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

20 Januari 2026, 11:19