Tafuta

2026.01.27 Kongamano kuhusu Mtakatifu Rose wa Lima katika Chuo Kikuu cha Gregorian. 2026.01.27 Kongamano kuhusu Mtakatifu Rose wa Lima katika Chuo Kikuu cha Gregorian. 

Kard.Tagle:Mtakatifu Rose wa Lima alihamasisha harakati mpya za kimisionari

Katika Kongamano kwenye Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriani Januari 27,liliakisi sifa na sanamu ya Mtakatifu Rose wa Lima,nchini Peru,kabla ya Sanamu hiyo kupelekwa katika Bustani za Vatican,Jumamosi tarehe 31 Januari 2026.

Edoardo Giribaldi na Angella Rwezaula – Vatican.

Kongamano lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian, tarehe 27 Januari 2026 lilikiakisi sanamu ya Mtakatifu wa Peru, Rose wa Lima (1586-1617). Hafla hiyo iliandaliwa na Ubalozi wa Peru unawakilisha Nchi yake mjini Vatican, kwa ushirikiano na Chuo Kikuu Katoliki cha Kipapa nchini  Peru (PUCP).

Mmisionari anayewahamasisha vijana

Akifungua tukio hilo, Kardinali Luis Antonio Gokim Tagle, Mwenyekiti Mwenza wa  Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, alitoa tafakari kuhusu Mtakatifu Rose, Msimamizi wa Peru na mmoja wa walinzi wa  Ufilipino katika nchi ya Kardinali huyo.

Habari za utakatifu wake zimevuka bahari na vizazi, na kuwa "mfano" na "kimbilio la kiroho" kwa watu kila mahali, hata Asia ya Kusini-mashariki. Kama Kardinali alivyoeleza, moja ya sehemu sita za mbele za Kanisa Kuu la Manila, imetengwa kwa ajili ya mtakatifu huyo. Pia alishiriki kumbukumbu ya kibinafsi kutoka wakati wake akihudumu katika parokia iliyotengwa kwa ajili ya Mtakatifu, ambaye ibada yake ilienea kwa Ufilipino kupitia wamisionari wa Kidominika wa Hispania.

La locandina dell'evento

Tangu Papa Clement X alipomtangaza kuwa Mtakatifu mwaka 1671, Kardinali Tagle alisisitiza kwamba Mtakatifu Rose anabaki kuwa "mmisionari wa milele." Hasa, anatumika kama msukumo kwa kizazi cha leo, ambacho huelekea kuongozwa zaidi na mifano kuliko mafundisho rasmi. Kardinali Tagle alielezea matumaini kwamba tukio hilo la kitaaluma linaweza kuwa mbegu ya "harakati mpya ya kimisionari."

"Yungiyungi kati ya miiba"

Katika salamu zake kwa wale waliokuwepo, Sista Raffaella Petrini, Rais wa Utawala wa  Jiji la Vatican, alimtaja Mtakatifu Rose wa Lima kama mtu ambaye ni mchanga milele, mwenye uwezo wa kuamsha upendo na huruma, akieneza mvuto wa "mfano" wake na "umaarufu" wake katika wakati na nafasi.

Una statua di Santa Rosa da Lima

Mnamo  tarehe 31 Januari 2026, sanamu hiyo itaakisi mtindo huu wa utakatifu, ambapo sanamu ya Mtakatifu Rose itazinduliwa katika Bustani za Vatican, kwa uwepo wa  Papa Leo XIV. Imetengenezwa kwa nyenzo zilizopatikana kutoka Peru. Kazi hizo zinaonesha wakati ambapo Mtakatifu, akimtafakari Bikira wa Rozari, alionekana  akiwa na Yesu, ambaye alimpatia pete na maua. Ishara ya sanamu hiyo, ambayo inajumuisha nanga na taji la Rozari, inasisitiza safari ya kidunia ya Mtakatifu Rose na inawasilisha uso "unaong'aa na wenye tabasamu" wa mtu aliyechagua kumfuata Kristo.

Askofu Carlos Enrique García Camader, Rais wa Baraza la  Maaskofu wa Peru, hakuweza kuhudhuria ana kwa ana kutokana na ziara ya Kichungaji ya  Maaskofu wa Peru ya  Visita Ad Limina huko Roma. Badala yake, alituma ujumbe wa video akiakisi  jukumu la Mtakatifu Rose katika historia ya Kanisa na kama mlinzi Msimamizi wa Amerika Kusini. Alielezea matumaini kwamba, kama Mtakatifu Rose, "utafutaji wa ukweli" ungeambatana na "upendo na huduma."

Padre  Mark Andrew Lewis, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian, aliunganisha umbo la Mtakatifu Rose na Papa Francisko. Mnamo 2017, wakati wa miaka mia nne ya kifo cha mtakatifu, Baba Mtakatifu alikumbuka upendo wake kwa uumbaji na kumwita, akinukuu kifungu kutoka kwa Wimbo uliobora "yungiyungi kati ya miiba." Mtaalamu huyo pia alibainisha kuwa Mtakatifu Rose bado anapendwa na watunza maua na bustani - taaluma alizojitolea maisha yake mengi na ambazo bado ni muhimu sana Amerika Kusini leo.

Neema katika kujitolea kila siku

Kardinali Carlos Castillo Mattasoglio, Askofu Mkuu wa Lima na wa Kanisa Lote nchini Peru, alizingatia "taalimungu  ya kiroho" ya Mtakatifu Rose, akibainisha kuwa alizingatia maisha yake katika hali yake ya ndani. Alinukuu kifungu ambacho mara nyingi alielekeza kwa Yesu: "Mchumba wangu mpendwa, nisaidie kufanya kazi." Kazi ya kila siku ikawa aina ya neema. "Tatizo kuu," Kardinali alisema, ni kinyume cha fadhila hii, wakati "neema" inakuwa "ushindi" badala ya zawadi, kutokana na ukosefu wa "msingi wa kiroho" ulioashiria maisha ya Mtakatifu Rose. "Basi si neema tena, bali ni aibu."

Santa Rosa da Lima

Kwa kuhitimisha Jorge Ponce San Román, Balozi wa Peru anayewakilisha nchi yake mjini Vatican, aliwashukuru waliohudhuria na taasisi zilizowezesha tukio hilo. Pia aliakisi  onyesho la awali katika Maktaba ya Vatican ya  Filamu ya “Una Rosa per il Mondo”,  yaani "Waridi moja kwa ajili ya Ulimwengu" iliyoongozwa na mtengenezaji wa filamu wa Peru Luis Enrique Cam. Filamu hiyo inaeneza mfano wa Mtakatifu huyu ambaye bado ni muhimu sana na mwenye ushawishi mkubwa leo. Katika kipindi "kabla ya mtandao," Balozi alibainisha, robo tatu ya wakazi wa Lima walishiriki katika maandamano ya Jeneza lake.

KONGAMANO MATAKATIFU ROSE

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here

30 Januari 2026, 10:58