Tafuta

Reliquie di San Pier Giorgio Frassati esposte nella chiesa della Domus Mariae

Kardinali Parolin kutembelea Denmark

Katibu Mkuu wa Vatican anatembelea Denmark kama Mwakilishi wa Papa kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 1,200 ya kuanza kwa utume wa Mtakatifu Ansgar.Programu yake pia inajumuisha mikutano ya kidiplomasia,miongoni mwao ikiwa ni ziara na Mfalme Frederik X na Waziri wa Mambo ya Nje Rasmussen.

Vatican News

Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, yuko Denmark kuanzia Jumamosi, tarehe 24, hadi 26 Januari 2026, akishiriki kama Mjumbe wa Papa, maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 1,200 ya kuanza kwa Utume wa Mtakatifu Ansgar katika nchi ya Kaskazini. Kulingana na taarifa iliyochapishwa kwenye akaunti ya Sekretarieti ya Vatican X, @TerzaLoggia, ziara hiyo itakamilika Jumatatu, Januari 26.

Masifu ya jioni na mikutano ya kiekumeni

Programu ya Jumamosi Januari 24 inajumuisha ushiriki katika Masifu ya Jioni ya  kiekumeni katika Kanisa Kuu la Kilutheri la Copenhagen (Vor Frue Domkirke), ikifuatiwa na mikutano na wanadiplomasia na viongozi wa jumuiya zingine za Kikristo.

Siku ya Dominika, Januari 25, Kardinali Parolin atatembelea monasteri ya Sankt Josefs Karmel huko Hillerød, kukutana na Masista wa Benedictine wa Vor Frue Kloster huko Birkerød, na kuongoza Misa katika Kanisa Kuu la St Ansgar huko Copenhagen, kuadhimisha sherehe za kumbukumbu hiyo.

Mikutano ya kidiplomasia

Siku ya Jumatatu, tarehe 26 Januari 2026, Katibu Mkuu  atafanya ziara ya heshima kwa Mfalme Frederik X wa Denmark katika Jumba la Amalienborg. Kisha atakutana na Waziri wa Mambo ya Nje Lars Løkke Rasmussen huko Eigtveds Pakhus, kabla ya kuhitimisha ziara yake kwa kusimama katika Seminari ya Mater ya Redemptoris huko Vedbæk.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku.Just click here

 

24 Januari 2026, 11:42