Tafuta

Kanisa Kuu la Mtakatifu Mikaeli na Gudula huko Brussels. Kanisa Kuu la Mtakatifu Mikaeli na Gudula huko Brussels.  (@VaticanNews)

Kard.Parolin,Mjumbe wa Papa huko Brussels kwa Maadhimisho ya Miaka 800 ya Kanisa Kuu

Katibu Mkuu wa Vatican atamwakilisha Papa Leo XIV tarehe 11 Januari,katika sherehe ya maadhimisho ya Kanisa Kuu la Watakatifu Michael na Gudula,lililojengwa mwaka 1226. Matukio mengi ya kiutamaduni na kiroho yatafanyika mwaka mzima wa 2026.

Vatican News

Katika barua, Baba Mtakatifu Leo XIV alimteua Kardinali Pietro Parolin,  Katibu Mkuu wa Vatican kuwa Mwakilishi wake katika hafla ya Maadhimiosho huko jijini Brussels itakayoadhimisha miaka 800 ya ujenzi wa Kanisa Kuu la Ubelgiji, Dominika tarehe 11 Januari 2026. Kanisa Kuu likiwa limewakwa kwa wasimamizi wake Watakatifu Michael na Gudula, watakatifu walinzi wa jiji hilo, lilijengwa kunako mwaka 1226 kwa amri ya Henry II, Mfalme wa Brabant, ambaye alilisimamisha Kanisa dogo lililopo kwenye makutano ya barabara zinazoelekea Ufaransa na Ujerumani.

Waamini wakati wa kumkaribisha Papa Francisko kunako Septemba 2024
Waamini wakati wa kumkaribisha Papa Francisko kunako Septemba 2024   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Mnamo tarehe 11 Januari 2026, Kardinali Parolin kwa hiyo atahudhuria Misa itakayoongozwa na  Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, akishirikiana na Askofu Mkuu Luc Terlinden wa Mechelen-Brussels na Maaskofu wote wa nchi hiyo, mbele ya familia ya kifalme ya Ubelgiji.

Matukio mengi ya kiutamaduni na kiroho yatafanyika mwaka mzima wa 2026 kuadhimisha kumbukumbu hii, yakiwa ni: matamasha, mikutano, na maonesho kuhusu historia ya Kanisa kuu, kazi bora ya usanifu wa Brabant Gothic.

Wafalme wa Ubelgiji walimkaribisha Papa Francisko Septemba 2024.
Wafalme wa Ubelgiji walimkaribisha Papa Francisko Septemba 2024.   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

Imesasishwa saa 7.58 mchana, Jumatatu 5 Januari.

03 Januari 2026, 15:05