Jubilei,zaidi ya mahujaji milioni 33 wamefika Roma.Fisichella:matumaini kwa Ulimwengu mzima
Na Daniele Piccini – Vatican.
"Dunia nzima" imefika Roma kwa Mwaka Mtakatifu wa 2025. Jumla ya mahujaji 33,475,369 walifika kutoka nchi 185 kwa ajili ya Jubilei ya Matumaini, ambayo Papa Leo XIV atahitimisha rasmi katika saa chache zijazo kwa kufunga Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Petro, tarehe 6 januari 2026. Hawa walizidi sana makadirio—yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Roma Tre—yaliyotabiri waamini milioni 31 pekee katika Jiji la Milele kwa mwaka wa neema maalum kwa Kanisa.
Askofu Mkuu Rino Fisichella, Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji na anayehusika na maandalizi ya ya Jubiliei alitathmini Mwaka Mtakatifu wakati wa mkutano uliofanyika asubuhi ya tarehe 5 Januari 2026, katika Kesha la kufungwa kwa Jubilei Takatifu , katika Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican. Mamlaka za kiraia zilizoshirikiana, kwa kutumia kile wanachokiita kwa kauli moja kuwa“mbinu ya Jubilei” katika kuandaa tukio hilo na miundombinu yote muhimu walikuwepo. Ulimwengu mzima ulikuja Roma, lakini hasa bara la Ulaya kwa asilimia: 62% ya mahujaji walitoka bara la zamani, huku Italia ikishika nafasi ya kwanza kwa idadi ya wageni waliofika jiji la Milele. "Kipimo cha kiroho kinachosimamia Jubilei kimetuwezesha kuona watu wakihama, wakiwa na hamu kubwa ya maombi na uongofu," alisema Askofu Mkuu Fisichella.
Maisha ya kiroho ya mahujaji yamestawi, kwani yalijaza sehemu kuu za hija na madhabahu za Roma. "Basilika za kipapa na vituo vingine vya maombi," aliongeza, "kama vile (Scala Santa) Ngazi Takatifu, vimeshuhudia mahudhurio yasiyo na kifani. Maungamo yameongezeka, na sherehe ya Jubilei ya msamaha kamili, msamaha, imewafikia kila mtu." Mwaka 2025, ambao umeisha hivi karibuni, umetoa matumaini kwa watu binafsi na kwa ulimwengu: "Jubilei inakaribia mwisho," Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji aliendelea, "lakini ishara nyingi za matumaini ambazo zimetolewa zinabaki, na upeo wa macho unapanuka ili kusaidia mustakabali uliojaa amani na utulivu, kama kila mtu anavyotaka. Kwa kifupi, Mwaka huu Mtakatifu ulifanikisha lengo lililoelezwa katika Hati ya Kutungaza Jubiliei yenye Kauli mbiu: Spes non confundit:"yaani, Matumaini hayakatishi Tamaa: kuwa fursa kwa kila mtu kufufua matumaini."
Ukarimu wa Watu wa Kujitolea 7,000
Hata hivyo, baadhi ya idadi ni muhimu, kwa sababu "katika wakati wa binafsi na rahisi," kama Askofu Mkuu alivyomalizia kuwashukuru, walipima ukarimu wa watu wa kujitolea wengi: Watu wa kujitolea 5,000 walio kazini katika Mwaka mzima na 2,000 kutoka Shirika la Kijeshi la Malta waliotoa uitikiaji wa kwanza katika Basilica nne za Kipapa.
Mazungumzo na Ushirikiano: "Mbinu ya Jubilei"
Alfredo Mantovano, Katibu Msaidizi wa Nchi kwa Urais wa Baraza la Mawaziri la Italia, alielezea "Mbinu ya Jubilei kuwa" ilikuwa na nini ya: "Utawala wa serikali ambao lazima uratibu, sio kuelekeza, tawala zingine. Mikutano ya uratibu ambayo hutatua matatizo, sio kuyaunda. Kila mmoja wa wadau huepuka kuchukua matokeo ambayo ni matunda ya kazi ya kila mtu. Haya yote yameruhusu mabadiliko ya kasi." Mashine ya utawala ambayo imejiweka katika huduma ya kiroho. "Taasisi hazipaswi kujibu maswali muhimu, kama yale tunayojiuliza sote tunapokabiliana na janga la Crans-Montana nchini Uswisi, bali ziwawezeshe watu kuyapitia, kama walivyofanya mahujaji." Fursa inayofuata itakuwa mwaka huu wa miaka mia nane tangu kifo cha Mtakatifu Francis wa Assisi. "Maisha ya Mtakatifu Francis kiukweli ndiyo jibu kamili zaidi kwa maswali mazito na ya kutisha yaliyoulizwa na matukio ya mwanzo huu wa mwaka. Hili pia linafaa kuendelea kufanyia kazi."
Karibu ya Jiji la Milele
Meya wa Roma na Kamishna Maalum wa Serikali wa Jubilei, Roberto Gualtieri, aliona jiji lake likiwakaribisha kwa subira waaminifu wengi waliokuja katika mji mkuu ili kupata furaha katika uhusiano wa manufaa kwa pande zote. "Mahujaji hawajapunguza uwezo wa Roma wa kuwakaribisha watalii na kutoa huduma kwa raia wake. Jubilei, kinyume chake, imekuwa nguvu inayowasukuma," alisema Meya. "Furaha, imani, na matumaini ya mahujaji yaligusa mioyo ya Warumi, ambao nao waliwakaribisha, hata wakati idadi yao ilikuwa ya ajabu. Tor Vergata, kwa mfano, ni tukio ambalo litabaki katika historia ya Jiji letu na Kanisa," Gualtieri alihitimisha.
Mchango wa Wafanyakazi wa Afya na Vikosi vya Usalama
"Mbinu ya Jubilei," alielezea Francesco Rocca, Rais wa Mkoa wa Lazio, "aliongoza kikundi cha uratibu kufanya kazi kwa utulivu, si ushindani, utulivu ulioenea kwa waendeshaji wote. Huduma ya dharura 118 ilifanya uingiliaji kati 580,000, 40,000 zaidi ya mwaka uliopita. Ziara za vyumba vya dharura zilifikia jumla ya 1,600,000, 100,000 zaidi ya mwaka 2024." Lamberto Giannini, Mkuu wa Usalama, Roma, hatimaye alielezea kanuni iliyo nyuma ya vitendo vya vikosi vya usalama katika mji mkuu: "Tulihitaji usalama na utulivu, kwa hivyo tulijaribu kuwasilisha usalama si kwa kutumia jeshi, bali kwa kushiriki katika kuzuia. Nilishangazwa na Jubilei ya Vijana, ambapo maungamo yaliwekwa katika Uwanda wa (Circus Maximus.) Ilikuwa kitu cha kipekee ambacho kitabaki katika kumbukumbu ya kila mtu."