John Allen,mwandishi wa habari aliyeelezea Vatican kwa utaalamu na akili!
Na Andrea Tornielli
John Allen Jr., 61, alikuwa mwanzilishi na mhariri wa Crux, Tovuti iliyobobea katika habari za Vatican na Kanisa lote ulimwenguni kwa wasomaji wa lugha ya Kiingereza, hasa nchini Marekani. Alifariki baada ya kupambana na saratani kwa miaka minne, lakini hakukata tamaa na kuendelea kufanya kazi kwa muda mrefu kama nguvu zake zilivyoruhusu. Nilikutana na John alipofika Roma miaka 26 iliyopita kama mwandishi wa habari wa “National Catholic Reporter,”yaani (Mwandishi wa Habari Kikatoliki wa Kitaifa ) akizingatia habari kuhusu Papa na Vatican na kufuatilia Ziara za Kitume za Papa Mtakatifu Yohane Paulo II. Ninachokumbuka kwanza kabisa kumhusu ni tabasamu lake na njia yake ya uwazi na uchangamfu ya kushirikiana na watu.
Milenia mpya ilianza kwa matumaini
Mwaka 2000, Papa Yohane Paulo II, ambaye tayari alikuwa ameathiriwa na ugonjwa, alikuwa akiishi Jubilei Kuu, hatua muhimu ya upapa wake, na kufanya ziara zilizokusudiwa kuingia katika historia. Kwa miaka mingi, uvumi na uvumisho kuhusu upapa wa baadaye wa Uchaguzi Mkuu ujao ulikuwa ukisambaa (baadhi yao, zaidi ya hayo, waliitwa kwenye Nyumba ya Baba, kabla ya Papa wa Poland). Milenia mpya ilianza kwa matumaini makubwa na uwazi, chini ya udanganyifu wa "mwisho wa historia" baada ya kuanguka kwa ukomunisti. Mtazamo huo ulivunjwa ghafla na mshtuko wa mashambulizi ya tarehe 11 Septemba 2001 na vita vilivyofuata nchini Afghanistan na Iraq. John aliweza kusimulia na kutafsiri mambo ya ndani ya Vatican na Kanisa (kwa mfano, kuibuka kwa kashfa ya unyanyasaji wa watoto) na jukumu la Vatican na diplomasia yake katika matukio ya kimataifa, hasa yale yanayohusisha Marekani.
Umakini na umuhimu wa mifumo ya tafsiri, uchambuzi na muktadha
Katika kila makala, John alichanganya umuhimu na umakini kwa vyanzo vyenye mifumo ya tafsiri, uchambuzi, na muktadha, na alisisitiza kutumia nukuu "kwenye kumbukumbu," kila mara zikiambatana na majina kamili. Kipengele kingine cha kufafanua kazi yake ni kwamba hakuchukua chochote kirahisi na kwa hivyo hakuwahi kuandika kwa ajili ya watu wa ndani pekee: Alijua jinsi ya kuzungumza na hadhira yake, na sio kwa Wakatoliki tu wala waamini pekee. Hata mtu alipopingana na hitimisho la uchambuzi wake, kila mara zilikuwa za thamani kusomwa, kwa sababu John alielezea ukweli tata wa Kiti Kitakaifu bila kuupuuza.
Mnamo Mwaka 2014, John aliondoka kwenye Gazeti la “National Catholic Reporter” na kuanzisha “Crux” ambayo mwanzoni ilikuwa tawi la “Boston Globe” na baadaye chapisho huru. Katika wakati wa taarifa zilizosambazwa na kurahisishwa kupita kiasi, alikuwa ameelewa kwamba uandishi wa habari wa kitaalamu na maalum ulikuwa wa thamani, kwa sababu wasomaji, waliokuwa wakisumbuliwa na habari ambazo mara nyingi si sahihi, walitaka na walihitaji kuelewa. John Allen aliandika kuhusu mienendo ya mikutano ya Kanisa na alikuwa amejitolea kwa wasifu wa Joseph Ratzinger (Kardinali Ratzinger: Mtekelezaji wa Imani wa Vatican) miaka mitano kabla ya kuwa Papa Benedikto XVI. Alifuatilia upapa wake na kuchaguliwa kwa Papa Francisko.
Kumuona Mrithi wa Mtume Petro kutoka Marekani
Pia alikuwa na furaha ya kumuona akichaguliwa kama Mrithi wa Petro, Mmarekani wa kwanza katika historia ya Kanisa Katoliki, ambaye alimjua na kutumia muda naye pia, shukrani pia kwa Elise, mwandishi wa habari wa Vatican ambaye alimwoa miaka sita iliyopita na mwandishi wa wasifu wa Papa Leo XIV, na ambaye alimtunza na kumsaidia wakati huu mgumu wa ugonjwa. Kuhusu John, mpenda vyakula vya Roma, na Mshabiki mkubwa wa Timu ya mpira ya Roma (AS Roma)ningependa kukumbuka sifa nne zaidi: uwezo wake wa kujenga uhusiano na mawasiliano na watu katika kila ngazi ya Kanisa; azimio lake la kutosimama kwenye hisia za kwanza, bali kutafuta kuelewa sababu za wengine; ucheshi wake; na ujuzi wake wa ajabu kama mzungumzaji, mwenye uwezo wa kuvutia hadhira yoyote kwa kubadilisha uchambuzi wa hali ya juu na historia na akili.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here