Tafuta

2026.01.16 Ibada ya kufungia zana za Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Petro. 2026.01.16 Ibada ya kufungia zana za Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Petro.  (@Vatican Media)

Basilika ya Mtakatifu Pietro:zana za Mlango Mtakatifu zawekwa na kufungwa kwenye ukuta

Ibada hiyo ilifanyika jioni ya tarehe 16 Januari 2026 kwa kuongozwa na Kardinali Mauro Gambetti,Mkuu wa Kanisa Kuu hilo.Kwenye Kisanduku cha shaba ufunguo wa Mlango Mtakatifu,Hati inayothibitisha kufunguliwa na kufungwa kwa Mlango na baadhi ya medali kutoka kwa mapapa:Papa Francisko na Papa Leo XIV ziliwekwa ndani ya Kisanduku na kufungwa ndani ya ukuta huo.

Vatican News

Ijumaa jioni tarehe 16 Januari 2026 Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Petro, uliofunguliwa kwa ajili ya Jubilei ya Kawaida ya 2025, ufungwa kwa uashi kama utamaduni na vifaa vinavyohusika kufungiwa ndani ya ukuta. Kardinali Mauro Gambetti, Mkuu wa Basilika ya Mtakatifu Petro, aliongoza tukio hilo la faragha la kuziba Mlango Mtakatifu wa Basilika  saa 1.30 za usiku saa za Ulaya mbele ya Mshereheshaji Mkuu wa Maadhimisho ya Liturujia za Kipapa, Askofu Mkuu Diego Giovanni Ravelli.

Ibada Ibada hiyo iliongozwa na Mkuu wa Sherehe za Kipapa, Monsinyo Massimiliano Matteo Boiardi. Katika sala yake fupi ya ufunguzi, Kardinali aliwaombea mahujaji wengi waliopitia Mlango Mtakatifu wakati wa Mwaka Mtakatifu, ili waweze kubaki imara katika imani na katika ushirika na Mrithi wa Petro.

Un momento del rito della muratura

Wakati wa Ibada ya kuweka zana ndani ya ukuta na kuziba (@Vatican Media)

Ibada

Mawe yanayotengezwa na kiwanda cha Mtakatifu Petro ( Fabbrica di San Pietro) yalijenga ukuta, ulioundwa na takriban matofali 3,200, ndani ya Basilika ili kufunga Mlango Mtakatifu. Ndani ya ukuta huo kuliingizwa kwenye chombo cha shaba, ambacho ni Sanduku lililotengenezwa maalum lililochongwa na nembo za Papa Francisko, aliyefungua Jubilei ya Kawaida ya 2025, na Papa Leo XIV, aliyeufunga mwaka huo.

La pergamena che attesta l'apertura e la chiusura della Porta Santa.

Hati inayoonesha kufunguliwa na kufungwa kwa Mlango Mtakatifu(@Vatican Media)

Chombo cha chuma chenye karatasi ya ngozi (pergamena) inayothibitisha kufunguliwa na kufungwa kwa Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Petro, medali mbili kutoka mwaka wa kwanza wa upapa wa Papa Leo XIV, medali inayolingana na mwaka wa mwisho wa upapa wa Papa Francisko, medali zingine za kuadhimisha miaka kumi kati ya Jubilei iliyopita, Jubilei ya Huruma mwaka 2016, na 2025, na medali ya Kiti kitupu(Sede Vacante 2025), ziliwekwa kwenye (kapsa) chombo hicho. Ufunguo wa Mlango Mtakatifu pia uliwekwa kwenye (kapsa) chombo hicho

La firma della pergamena.

Kutia saini kwenye pergamena. (@Vatican Media)

Chombo hicho (Capsa) cha shaba hatimaye kiliwekwa kwenye chombo cha risasi, ambacho kiliunganishwa na kufungwa. Kardinali Gambetti Mkuu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro pamoja na Mshereheshaji Mkuu wa Maadhimisho ya Kipapa  waliweka matofali mawili, hivyo kuanza awamu ya mwisho ya uashi. Ibada ilihitimishwa na Sala ya Bwana na baraka.

Un momento del rito di Muratura della Porta Santa della Basilica di San Pietro.

Wakati wa kibada ya kiziba Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Petro . (@Vatican Media)

Wakati wa Maombi

"Ni wakati maalum kwa sababu unaashiria tendo la mwisho la kufunga Mwaka Mtakatifu, kwa kuta za ndani ya Basilika ya Mlango Mtakatifu," Monsinyori Orazio Pepe, Katibu wa Kiwanda  cha Mtakatifu Petro, akizungumza na vyombo vya habari vya Vatican. "Sio tu ibada ya kiufundi bali pia ni wakati wa maombi kwa sababu tunakumbuka kwamba Mlango Mtakatifu, pamoja na ishara zake zote, pia ni uhalisia wa kiroho, mahali ambapo waamini humwona Mungu hata kwa kupitia mlango huu."

Preparazione della capsa di bronzo che verrà poi murata.

Maandalizi ya kisandku cha Shaba( capsa) kwa ajii ya kukifungia kwenye ukuta(@Vatican Media)

Ufuriko wa Mahujaji

Monsinyo Pepe, akizungumza na Eugenio Bonanata, pia alizungumzia "urithi" ulioachwa na Jubilei iliyomalizika hivi karibuni: "Ikiwa kwa upande mmoja mlango unafungwa, kwa upande mwingine mlango ni wazi kila wakati. Ufuriko wa mahujaji hakika utapungua, lakini bado kuna watu wengi wanaokuja kwenye kaburi la Mtakatifu Petro kama mahali pa hija, kama mahali patakatifu, kama wakati wenye nguvu katika maisha yao. Mwaka huu pia tulikuwa na ongezeko kubwa la mahujaji waliokuja kwa miguu: walikuwa wengi wao, na waliongezeka sana ikilinganishwa na zamani. Kwa hivyo kuna hamu hii ya kutembea kuelekea Mungu na kufikia maeneo ambayo inawezekana kumwona Mungu, kama katika Basilika ya Mtakatifu Petro." Matumaini ni kwamba "waamini wote wanaoendelea kumiminika kwa Mtakatifu Petro watapata nia hii kwa upande wetu kuwakaribisha katika mahitaji yote ya kiroho waliyo nayo mioyoni mwao na ambayo wanahisi ni muhimu kwa maisha yao."

Kuziba na kufunga Mlango

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

 

 

17 Januari 2026, 09:59