Tafuta

Askofu Mkuu Fortunatus Nwachukwu,Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji(Kitengo cha Kwanza cha Uinjilishaji na Makanisa Mapya maalumu). Askofu Mkuu Fortunatus Nwachukwu,Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji(Kitengo cha Kwanza cha Uinjilishaji na Makanisa Mapya maalumu).  (Vatican Media)

Ask.Mkuu Nwachukwu:kuikomboa Nigeria kutoka eneo la moshi wa vurugu zilizoenea

Mnamo 2025,Nigeria ilirekodi idadi kubwa zaidi Afrika ya 5 wamisionari Wakatoliki na wahudumu wa kichungaji waliouawa.Ni nchi hiyo ambapo jumuiya ya Wakatoliki imekuwa ikikumbwa na janga la utekaji nyara kwa sababu ya unyang'anyi kwa muda mrefu.Kuhusu vurugu na mateso yanayowaathiri Wakristo wa Nigeria,Askofu Mkuu Nwachukwu,Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji(Kitengo cha Kwanza cha Uinjilishaji na Makanisa Mapya maalumu)alitoa maoni yake.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika mahojiano yaliyochapishwa na Shirika la Kipapa la Kimisionari Fides,tarehe 30 Desemba 2025 ya Gianni Valente na Askofu Mkuu Fortunatus Nwachukwu, Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji(Kitengo cha Kwanza cha Uinjilishaji na Makanisa Mapya maalumu)alielezea juu ya kuikomboa Nigeria kutoka katika alichokiita "eneo la moshi" wa vurugu zilizoenea. Mwandishi wa Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari katika mahojiano hayo alibainisha kwamba mnamo 2025, Nigeria ilikuwa nchi yenye idadi kubwa zaidi (5) ya wamisionari Wakatoliki na wafanyakazi wa kichungaji waliouawa.  Ni nchi ile ile ambapo Jumuiya ya Wakatoliki imeathiriwa kwa muda mrefu na janga la utekaji nyara na kwa ajili ya unyang'anyi. Kuhusu vurugu na mateso yaliyowahusisha Wakristo wa Nigeria, Askofu Mkuu Fortunatus Nwachukwu, mzaliwa wa ho Nigha, katika sehemu ya Kusini ya eneo la Nigeria, ambalo lilindwa zamani za ukoloni wa Kiingereza na kwa sasa ni Jamhuri ya Shirikisho la Nigeria, akiwa mmoja wa watu kabila la Igbo, ndani ya familia ni wa tatu kuzaliwa kati ya kaka na dada zake kumi na wawili. Wawili kati ya dada zake wadogo walifariki wakati wa Vita vya Biafra (1967-1970). Yafuatayo ni mahojiano kamili:

Ukiwa Mwana wa  Kanisa la Nigeria, unaionaje takwimu kuhusu wahudumu  wa kichungaji waliouawa nchini Nigeria mwaka 2025?

Yote haya ni chanzo cha huzuni kubwa. Na pia aibu kidogo. Kwa sababu Nigeria ni mojawapo ya nchi zenye idadi kubwa ya watu wa dini mbali mbali duniani. Watu waaamini, Wakristo na Waislamu. Sote tunadai kuwa watu wa amani. Hata marafiki zetu Waislamu wanarudia kila mara kwamba Uislamu ni dini ya amani. Na tukikabiliwa na ukweli na hali fulani, ningependa kuona marafiki zetu Waislamu wakishutumu na kukataa matumizi ya dini yao kufanya vitendo vya vurugu. Sote lazima tukatae uhalali wowote wa kutumia dini kufanya vitendo vya vurugu, hata kufikia hatua ya kuua watu.

Je, kuna kitu katika historia za mateso ya Wakristo wa Nigeria kinachokugusa kwa njia maalum?

Watu walioathiriwa hawataki kuwa mashujaa; si watu wanaojiweka katika hatari maalum. Wanaathiriwa na vurugu katika maisha yao ya kawaida, huku wakiwa na shughuli nyingi wakifanya wanachotakiwa kufanya: waseminari wanaoishi katika seminari, au wanafunzi waliotekwa nyara wakiwa shuleni. Na wale wanaopaswa kuwalinda hawafanyi chochote.

Je, kuna majukumu maalum kwa kuenea kwa vurugu?

Serikali inapaswa kuwa ya kwanza kuhisi aibu kwetu Wanigeria. Na wengi wanalaani uvivu wa serikali kutokana na kinachoendelea. Kundi lenye silaha linawezaje kuwachukua watoto 300 kutoka shuleni, kwa kutumia njia za kiteknolojia za udhibiti leo hii? Au ni uzembe tu? Au kuna ukosefu wa nia ya kujibu? Na ukosefu wa majibu ni chanzo cha aibu zaidi. Hata Jenerali alikamatwa na vikundi vyenye silaha, ambavyo kisha vikatoa video ya kunyongwa kwake. Pia wanataka kulidhalilisha jeshi, katika nchi kubwa zaidi barani

Mnamo Novemba, Urais nchini Marekani uliorodhesha Nigeria kama Nchi ya "Hatari Maalum," ikimaanisha hasa mateso ya Wakristo. Unaonaje utata ulioibuka kuhusu uamuzi huu?


Ninasema kwamba mijadala hii ni ya kuchosha, na inaweza hata kukatisha tamaa kutokana na maslahi na nguvu inayovutia. Kwa nini tujikute katika mijadala hii ya kufikirika inayoizunguka Nigeria, tukitumia muda wetu kujadili kama mateso yanafanyika nchini au la, badala ya kuwekeza nguvu hiyo hiyo katika hatua za kuondoa vurugu dhidi ya wasio na hatia ambazo ndizo chanzo cha mijadala hii?

Lakini je, inaweza kusemwa kwamba Wakristo wananyanyaswa nchini Nigeria?

Kuhusu jambo hili, kuna mambo kadhaa ya kuzingatia: Nigeria inakabiliwa na kuporomoka kabisa kwa usalama, na kuathiri kila mtu. Ukosefu huu mkubwa wa usalama ni kama kifuniko cha moshi kinachotuzuia kutambua wazi ni makundi gani yanalengwa kwa ukatili fulani. Mimi pia niliamini kwamba, hadi mwaka mmoja uliopita, vurugu hizo zilitokana zaidi na migogoro kati ya makundi ya kijamii au kikabila, kama vile ile kati ya wafugaji wa Fulani na wakulima. Lakini kulingana na taarifa nilizoweza kukusanya katika mwaka uliopita, ishara nyingi zinaonesha kwamba kuna makundi yenye nia ya kulenga Jumuiya za Kikristo kimfumo. Takwimu nyingi zinaweza kutumika kuunga mkono simulizi za wale wanaozungumzia mateso ya Kikristo.

Hizi ni zipi?

Uwepo wa mara kwa mara wa kutekwa nyara na mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya Wakristo, utafikiri kujibiwa kwa mpango wa kimfumo kwani, vikosi vya usalama vinapoitwa kuingilia kati, haviji au huja kwa kuchelewa. Kila kitu kinaonesha kuwa kuna nia ya makusudi ya kuwalenga waathiriwa Wakristo.

Nia hii inawezaje kuthibitishwa?

"Kifuniko cha moshi" cha vurugu zilizoenea kinapaswa kuondolewa angalau kwa kiasi fulani ili kubaini kama makundi fulani yanalengwa moja kwa moja na kwa makusudi, na kama kifuniko hiki cha moshi kimechochewa kuwalenga Wakristo huku kikificha nia zao wenyewe. Hii ndiyo maana utata kuhusu Nigeria kama nchi ya mateso ya Wakristo unatarajiwa kuendelea. Na serikali, badala ya kujizuia kujilinda tasa, inapaswa kuchukua suala la usalama mikononi mwake ili kuwakanusha wale wanaozungumzia mateso au hata mauaji ya halaiki ya Wakristo nchini Nigeria. Kwa mfano, hata baada ya utekaji nyara mkubwa wa wanafunzi 300 vijana, majibu ya serikali yalikuwa ya kutiliwa shaka sana.

Lakini je, kuna mwisho wazi kati ya mizizi ya migogoro ya kijamii au kikabila na vurugu za kidini na dini zinazoibuka?

Hali inabadilika. Hapo awali, mambo yanayolenga kijamii, kama vile mgogoro kati ya wafugaji wa kuhamahama na wakulima, yalitawala. Sasa ni wazi kwamba Wafulani si wafugaji tu. Ni wazi kwamba kundi hilo limeingiliwa; kuna wale ambao hawafuati wanyama wao; wanasafiri kwa pikipiki na magari mengine, wakiwa na silaha za kushambulia kiotomatiki. Sasa wanashambulia vijiji, shule, na seminari. Na hata mgogoro kati ya wafugaji na wakulima umekuwa kikwazo kwa mambo mengine kutokea. Na ninaona hatari nyingine katika haya yote: kuwafanya Wafulani kuwa mapepo.

Kuwafanya mapepo kunaweza kusababisha nini?

Kwa sasa , Wafulani wamekuwa kama mashetani kwa kila mtu. Kila mtu anaogopa. Hakuna anayezungumzia Wafulani wote wema, ambao pia wapo miongoni mwa wafanyabiashara na wasomi. Wafulani wanapotajwa, kila mtu anafikiria ugaidi. Katika hali hii, kinachohitajika ni cheche na chuki ya ulimwengu wote inaweza kutolewa dhidi yao. Vikundi vilivyojipenyeza vinawaweka Wafulani wote katika hatari hii, si tu nchini Nigeria bali  ukanda wa Sahel yote.

Je, Maaskofu wanaweza kuwa na maono ya pamoja ya kinachoendelea?

Kwa bahati mbaya, "kifuniko cha moshi" cha vurugu zilizoenea hufanya hili kuwa gumu pia. Kila mtu sasa anawalaumu Wafulani, lakini majambazi kutoka katika vikundi vingine wanaopata pesa kutokana na utekaji nyara pia wanafanya kazi, hata kusini. Hali inazidi kuwa ngumu, na hii pia inaathiri maoni ya Maaskofu, ambao hufanya tathmini tofauti kulingana na eneo lao. Na kwa vyovyote vile, wengi wao, hasa katikati mwa nchi, sasa wanashiriki maoni ya wale wanaosisitiza kwamba mateso ya Wakristo yanaendelea nchini Nigeria.

Je, Jumuiya  hufuata mikakati  fulani au tahadhari zozote ili kushughulikia hali hii?

 Ingawa mashirika ya serikali yanaonekana kushindwa kuhakikisha usalama wa Wakristo, Kanisa Katoliki na Makanisa ya Kiprotestanti ya kiutamaduni na Makanisa ya Marekebisho yanashiriki ushauri na hatua za jinsi ya kuwa na busara zaidi na kuepuka hatari. Vikundi vya Kipentekoste kwa ujumla vina ukali zaidi katika majibu yao na katika kuiwajibisha serikali. Zaidi ya hayo, taasisi nyingi zinaongozwa na watu waliojitangaza kuwa Wakristo. Katibu Mkuu wa Serikali na Spika wa Bunge la Kitaifa ni Wakatoliki. Mkuu wa jeshi anajitangaza kuwa Mkristo. Mke wa Rais wa Jamhuri anadai kuwa mchungaji... Lakini hawajibu wanachokiona kikitokea.

Wewe ni msomi wa Biblia. Neno la Mungu linahusije uzoefu wa mateso hadi kufikia hatua ya kuuawa kishahidi? Na tamaduni ya Kanisa imewakumbatia na kuwaonaje wafiadini wake?

Yesu hakuja kuleta kifo na mateso. Anawaahidi wafuasi wake uzima, na kwamba wapate uzima huo tele. Ili kuwawezesha wafuasi wake kupata uzima huu, Yesu alitoa uhai wake. Lazima tuangalie imani ya Kikristo katika nuru hii. Shahidi si mtu anayekwenda kujiua. Na ni upuuzi kuwaita wafiadini waliojiua. Shahidi ni mtu anayeshuhudia upendo wa Mungu kwa wote, kwa kumwiga Kristo. Kwa kushiriki katika upendo wake. Papa Francisko pia alizungumzia kuhusu imani ya kishahidi kwa wale waliohatarisha maisha yao wakati wa janga la Uviko -19 ili kukaa karibu na watu na kuwasaidia kila mtu. Shahidi si ushujaa wa kibinafsi wa kujivunia. Ni kuungana na Yesu na kumfuata, kubebwa naye. Na kwa kufanya hivyo, tunaweza kuitwa kutoa maisha yetu wenyewe.

Usiku kati ya Desemba 24 na 25, vikosi vya jeshi la Marekani vilifanya mashambulizi katika eneo la Nigeria kwa lengo lililotajwa la kushambulia maeneo ya makundi yanayoaminika kuhusishwa na kile kinachoitwa Dola ya Kiislamu. Je, hii ni njia ya kutosha na inayofaa kushughulikia matatizo hayo?

Nchi inaweza kujikuta haiwezi kushughulikia migogoro na migawanyiko yake bila msaada wa nje. Ninaona marafiki wengi Waislamu ambao wenyewe hawajui jinsi ya kuguswa na kinachoendelea. Na kutochukua hatua kwa serikali kunaonekana. Katika hali hii, uingiliaji kati wa nje usio wa moja kwa moja ili kuunga mkono serikali na serikali dhidi ya makundi yenye msimamo mkali na kusaidia nchi kushughulikia sababu za vurugu zilizoenea huenda usiwe wa haki kabisa au usiofaa.

Mahojiano As.Mkuu Nwachukwu

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

 

 

03 Januari 2026, 08:04