Kumbukizi ya Kifo cha Papa Benedikto XVI,Kard Koch:Ukombozi unatimizwa kwa kila mtu!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika maadhimisho ya Misa tarehe 31 Desemba 2025 kwa ajili ya kukumbuka kifo cha Papa Benedikto XVI iliyofanyika katika Groto za Vatican, mahali kaburi lake lilipo na mapapa wengine Kardinali Kurt Koch, Mweyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamaisha Umoja wa Wakristo, alikumbuka katika mahubiri yake kusudi kuu la maisha ya Kikristo, ambalo Papa Ratzinger alionesha kwa mfano katika maisha yake mwenyewe hasa kukuza uhusiano na Mungu na kujiandaa kwa muungano naye. Kardinali Koch alisema “Ikiwa uzima wa milele unatokana na ushirika na Mungu, inafaa kujitayarisha tayari katika maisha yetu ya kidunia, kama Joseph Ratzinger alivyofanya kwa bidii katika maisha yake yote.”
Kardinali Koch alisisitiza kwamba Papa wa Bavaria, ambaye alirudi nyumbani kwa Baba mnamo tarehe 31 Desemba 2022, alikuwa akitafuta na kupata uso wa Bwana katika kukutana kwake na Yesu Kristo. Kwani ndani yake, Mungu mwenyewe alijifunua na kuonesha uso wake wa kweli. Kardinali Koch kadhalika alikumbuka jinsi ambavyo Papa Benedikto XVI alivyozingatia vitabu vyake vitatu kuhusu "Yesu wa Nazareti" – vilivyochapishwa kati ya 2007 na 2012 - kama usemi wa utafutaji wangu binafsi wa uso wa Bwana.
Siku ya mwisho ya mwaka wa kawaida, Kardinali Koch alisema mwanzoni mwa mahubiri yake, kuwa liturujia ya Kanisa inapendekeza usomaji kutoka Dibaji ya Yohane, ambayo huanza na maneno, “hapo mwanzo kulikuwako Neno, na Neno alikuwa pamoja na Mungu, na Neno alikuwa Mungu.” Kwa njia hiyo ninaona ni jambo zuri sana na la kugusa moyo, kwamba katika siku ya mwisho ya mwaka, imani ya Kikristo inaleta mwanzo mpya kabisa, ikiwa na ahadi kwamba mwisho wa maisha ya mwanadamu duniani si mwisho kabisa, bali mwanzo mpya, na kwamba siku ya mwisho ya maisha ya mtu duniani ni mwanzo wa maisha mapya, uzima wa milele na Mungu."
Papa Ratzinger, Kardinali Kurt aliongeza, akinukuu kutoka kwa "Mahubiri yasiyochapishwa 2005-2017" ya Papa Benedikto XVI, yaliyochukuliwa kuwa kifo kama "kuvunjika kwa mahusiano yote ya kibinadamu, kuharibika kwa upendo, urafiki, na hii, Papa alisema, ndio sehemu ya kusikitisha zaidi ya uzoefu wa kifo. Lakini katika mahali hapa pa kuachwa kabisa, ni upendo wa Mungu na upendo wake pekee unaoweza kutoa mwanzo mpya. Ni ikiwa Mungu tu mwenyewe atajidhihirisha na upendo wake katika mahali hapa pa upweke kabisa na kunyimwa kabisa mahusiano ya kibinadamu ndio mwanzo mpya unaowezekana.”
“Ubatizo ni mwanzo wa kweli wa uzima wa milele. Kwa njia hiyo, kiukweli, tayari tumejumuishwa katika ushirika huo na Mungu aliye hai ambao tulipewa katika kifo na ufufuko wa Yesu Kristo, na ambao unajumuisha hili: kuishi uso kwa uso na Mungu aliye hai milele na kufurahia upendo wake usio na kikomo. Kwa maana yeyote anayeishi na Mungu hafi; upendo wa Mungu hutoa umilele. Kwa hivyo, uzima wa milele ni huu kweli: "Kukujua wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma."
Papa Ratzinger alisisitiza wakati wa kutafakari kwake mbele ya Sanda Takatifu ya Torino mnamo tarehe 2 Mei 2010 kwamba “Upendo umeingia katika ulimwengu wa chini” kwa mjibu wa Hii, Kardinali “hii ni ahadi inayohusiana na liturujia ya Jumamosi Kuu Takatifu kwamba "Kristo, akileta upendo wa kimungu mahali pa kifo, hutoa uzima katikati ya kifo, na mwanzo mpya mwishoni mwa maisha ya kidunia." Kazi, hiyo alisisitiza, ambayo pia inatimizwa katika kifo cha kila mtu: kama vile Kristo alivyoingia katika ufalme wa mauti na, kwa moto wa upendo wake, alileta harakati katika hali ngumu ya kifo, vivyo hivyo leo hii pia analeta upendo wake katika kifo cha mwanadamu na kuvunja kutengwa kwa kifo kwa kuanzisha ushirika mpya, ushirika na Mungu mwenyewe." Huu ndio umilele ambao Mungu amewapatia wanadamu: "Tunadaiwa uzima wa milele kwa uhusiano usioharibika wa upendo ambao Mungu anao nasi," Kardinali Koch alisisitiza.
“Katika sala yake ya kuaga, Yesu hatimaye anaomba: "Baba, nitukuze sasa mbele zako kwa utukufu niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako"(Yh 17:5). Hakika, katika uzima wa milele, Joseph Ratzinger-Benedikto XVI anajiunga na sala hii, akiitumia kwake mwenyewe na kuomba utimilifu wa maisha yake mbele ya Mungu milele. Na tunaifanya sala yake kuwa yetu wenyewe, tukimkumbuka katika Misa Takatifu, ambayo tunasherehekea fumbo la imani yetu, linalosema: uzima hushinda kifo, kwa sababu upendo wa milele wa Mungu una nguvu zaidi kuliko kifo. Amina.
Na kama vile Kristo, katika sala yake ya kuaga, iliyoandikwa katika Injili ya Yohane 17 alivyomwomba Baba amtukuze, vivyo hivyo, Kardinali alihitimisha, kuwa “hakika, katika uzima wa milele, Joseph Ratzinger-Benedikto XVI anajiunga na ombi hili, akiitumia kwake mwenyewe na kuomba utimilifu wa maisha yake katika uwepo wa milele wa Mungu." Ombi ambalo Kardinali Koch, mwishoni mwa mahubiri yake, alitoa mwaliko kwa wote ili kufanya hivyo hivyo kwao wenyewe.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.