Tafuta

2025.12.19 Kanisa la China. 2025.12.19 Kanisa la China. 

China na Kanisa:Kujenga Madaraja

Makao makuu ya Vyombo vya habari vya Vatican iliandaa hafla ya uzinduzi wa kitabu kipya kilichoandikwa na mwandishi wa China Chiaretto Yan,chenye kichwa:"Ndoto Yangu ya Kichina:Mazungumzo na Kukutana na Ukristo."

Na Guglielmo Gallone

"Ndoto yangu ya Kichina ni kuwa daraja kati ya Ukristo na Uchina: Ninatumaini kwamba Papa anaweza kutembelea nchi yangu, na kwamba China inaweza kukaribisha nuru ya Injili." Hayo yalikuwa maneno ya Chiaretto Yan, mwanachama wa Kichina wa Harakati ya Wafocolari, katika mahojiano na Vyombo vya habari vya Vatican. Alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu chake “Il mio sogno cinese: Dialoghi e incontri con il cristianesimo” yaani "Ndoto Yangu ya Kichina: Mazungumzo na Kukutana na Ukristo," ambacho kiliwasilishwa Jumanne tarehe 15 Desemba 2025  katika makao makuu ya Vyombo vya habari vya Vatican kwenye Jumba la Pio, Roma.

Tamaa ya ulimwengu kwa ajili ya ukweli, wema, na uzuri

Ndoto hii, Yan anaelezea, imejikita katika imani kwamba, kwa utamaduni wa Kichina, Ukristo si kipengele kigeni bali ni mshirika wa mazungumzo. "Katika kila mwanadamu kuna hamu ya ulimwengu kwa ajili ya ukweli, wema, uzuri na upendo," alisema, "tamaa kubwa inayovuka tamaduni na mila, na kwamba katika Ukristo huonyeshwa katika uhusiano wa kibinafsi na Mungu."

"Kwa upande mmoja mimi ni Mkristo Mkatoliki," Yan aliendelea, "na kwa upande mwingine mimi ni Mchina. Imani ya Kikristo inaniambia kwamba Mungu huja kwetu, kwamba alifanyika mwili kutokana na upendo kwa wanadamu. Mpango wa Mungu kwa mwanadamu ni Ufunuo wa kimungu. Tamaduni zingine, pamoja na dini zingine, pia ni juhudi za wanadamu kumtafuta Mungu. Ndiyo maana naamini 'maelekeo' haya mawili yanakutana; hayapingani."

Njia tano za kusonga mbele

Kwa roho hii, mwandishi alichagua kuzingatia maeneo matano ya utafiti ambayo yangeweza kuunganisha utamaduni wa Kichina na Ukristo: falsafa, ikolojia, siasa, uchumi na mazungumzo ya kiutamaduni. "Haya yote ni masuala ya mada kuu," Yan alisema, "na ni changamoto ya pamoja kwa wanadamu wote. Tumeona hili katika upapa wa Papa Francisko, katika hati kama vile Wwaraka wa Laudato Si' na Fratelli Tutti, lakini pia tunaliona katika mjadala wa Kichina wa kisasa." Muunganiko huu pia umejengwa katika utamaduni wa Kichina, Yan anaendelea. "Confucius alisema: 'Hatuwezi kujua vya kutosha kuhusu maisha haya, kwa hivyo sichunguzi maisha ya baada ya kifo.' Laozi alisema: 'Wale wanaojua hawasemi; wale wanaozungumza hawajui.' Kauli hizi hazioneshi kukataa kupita kiasi, bali mtazamo wa unyenyekevu: maisha ya baada ya kifo ni fumbo, na wanadamu hawana hilo wanaweza tu kukaribia hilo.

Kiini, huo ni mtazamo wa uwazi unaotambua mipaka ya lugha na sababu, na unaopata sehemu ya kuwasiliana na Ukristo." Ingawa katika lugha ya Magharibi mara nyingi huchukuliwa kama mgongano, Yan alielezea, akifuata mipango ya kifalsafa kama vile ya Hegel, "katika Utao inachukua umbo la maelewano: yin na yang hazipingani ili kuangamizana, bali huitana na kukamilishana." Ndani ya mantiki hii, Yan alibainisha "lugha ya upendo" inayofaa kwa Ukristo, hasa katika fumbo la Kristo msalabani, ambaye hujitoa mwenyewe, huweka nafasi, hukumbatia utupu ili kutimiza mapenzi ya Baba. "Katika lugha ya kifalsafa ya Kichina pia," Yan alibainisha, "uhusiano kati ya kuwa na kutokuwa na uhai si wa uharibifu, bali wa kuzalisha: ni kutokana na uhusiano huu ambapo maelewano huzaliwa. Na hapa ndipo mazungumzo yanakuwa ya kina zaidi, hadi kufikia hatua ambapo inawezekana kuzungumza."

Uzinduzi wa kitabu

Mazungumzo yalikuwa katikati ya uzinduzi wa kitabu, ambapo Profesa Agostino Giovagnoli, profesa wa Historia ya Kisasa katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Moyo Mtakatifu huko Milano; Padre Federico Lombardi, S.J., rais wa Mfuko wa Vatican wa Joseph Ratzinger–Benedikto XVI; na Padre Antonio Spadaro, S.J., katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu. Aliyesimamia majadiliano alikuwa Gianni Valente, mkurugenzi wa Shirika la Kipapa Habari za Kimisionari  Fides.

Kitabu ukristo China

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

20 Desemba 2025, 12:40