Tafuta

Mheshimiwa sana Padre Vicent Ouma Odundo, kutoka Jimbo kuu la Kisumu nchini Kenya, ameteuliwa na Papa Leo XIV kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Kisumu, nchini Kenya. Mheshimiwa sana Padre Vicent Ouma Odundo, kutoka Jimbo kuu la Kisumu nchini Kenya, ameteuliwa na Papa Leo XIV kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Kisumu, nchini Kenya. 

Askofu Msaidizi Vicent Ouma Odundo Jimbo Kuu la Kisumu, Kenya

Papa Leo XIV amemteuwa Mheshimiwa sana Padre Vicent Ouma Odundo, kutoka Jimbo kuu la Kisumu nchini Kenya, kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Kisumu. Hadi kuteuliwa kwake, Askofu Msaidizi mteule Vicent Ouma Odundo alikuwa ni Makmu wa Askofu Jimbo kuu la Kisumu, nchini Kenya. Itakumbukwa kwamba, Askofu Msaidizi mteule Vicent Ouma Odundo alizaliwa tarehe Mosi Juni 1978 mjini Kisumu. Alipadrishwa kunako tarehe 20 Februari 2008.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV Dominika tarehe 14 Desemba 2025 amemteuwa Mheshimiwa sana Padre Vicent Ouma Odundo, kutoka Jimbo kuu la Kisumu nchini Kenya, kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Kisumu. Hadi kuteuliwa kwake, Askofu Msaidizi mteule Vicent Ouma Odundo alikuwa ni Makmu wa Askofu Jimbo kuu la Kisumu, nchini Kenya. Itakumbukwa kwamba, Askofu Msaidizi mteule Vicent Ouma Odundo alizaliwa tarehe Mosi Juni 1978 mjini Kisumu. Baada ya malezi na majiundo yake ya Kipadre, tarehe 20 Februari 2008 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo kama Padre ametumikia kama: Paroko usu na Msimamizi wa Parokia ya Mtakatifu Augustino Nyamonye kati ya mwaka 2009 hadi mwaka 2012; Paroko wa Holy Cross Siaya kati ya Mwaka 2012 hadi Mwaka 2013.

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya
Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya

Baadaye, alitumwa na Jimbo kuu la Kisumu kuendelea na masomo ya juu kwenye Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana na kujipatia Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu katika Sheria za Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano. Baada ya masomo yake, alirejea nchini Kenya na kupangiwa kuwa Msimamizi wa Parokia ya St Andrew, huko Bondo kati ya Mwaka 2018 hadi mwaka 2019. Akateuliwa kuwa Hakimu wa Mahakama ya Jimbo kuu la Kisumu kati ya Mwaka 2018 hadi mwaka 2020; Kansela wa Jimbo Kuu Katoliki la Kisumu kati ya Mwaka 2019 hadi 2023. Na hatimaye tangu Mwaka 2019 hadi kuteuliwa kwake kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Kisumu, alikuwa ni Makamu wa Askofu.

Jimbo Kuu la Kisumu

 

14 Desemba 2025, 11:56