Papa akutana na Waziri Mkuu wa Armenia
Vatican News
Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 20 Oktoba 2025 alikutana na Bwana Nikol Pashinyan, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Armenia katika Jumba la Kitume. Baadaye Pashinyan alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
Mazungumzo katika Sekretarieti ya Nchi
"Wakati wa majadiliano ya kindani katika Sekretarieti ya Vatican, katika taarifa kutoka Ofisi ya Habari inasema, "kuridhika kulioneshwa kwa uhusiano mzuri kati ya Vatican na Armenia, nchi yenye utamaduni wa kale wa Kikristo, na vipengele fulani vya maisha ya Kanisa Katoliki nchini humo vilioneshwa." "Wakati huo huo," taarifa hiyo inaendelea, "tahadhari ilitolewa kwa masuala mengine ya maslahi ya pande zote, hasa haja ya amani ya utulivu na ya kudumu katika Caucasus Kusini."