Papa akutana na Rais wa Hungaria:mahusino mema baina ya Vatican na Hungaria
Vatican News
Baba Mtakatifu Leo XIV, Jumatatu tarehe 27 Oktoba 2025 alikutana na Waziri Mkuu wa Hungaria, Bwana Viktor Orbán, ambapo mara baada ya mkutano huo alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na nchi na Mashirikia ya Kimataifa.
Katika mazungumzo yao, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya habari Vatican, walionesha uhusiano thabiti kati yao na kupongeza jitihada za Kanisa Katoliki katika kuhamasisha maendeleo kijamii na ustwi wa Jumuiya ya Hungaria, kwa namna ya pekee umakini katika nafasi ya familia, mafunzo na wakati ujao wa vijana ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kulinda jumumuiya za kikristo zilizo katika mazingira magumu.”
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi za vyombo vya habari, Vaticam imebanisha kuwa sehemu kubwa ya mazungumzo hayo ilipewa “masuala ya Ulaya kwa namna ya pekee umakini wa mgogoro wa Ukraine na hali halisi ya Mashariki ya Kati.”