Tafuta

2025.10.18 Tuzo ya Mfuko wa Vatican wa Yohane Paulo II kwa Askofu Mkuu Jacques Mourad. 2025.10.18 Tuzo ya Mfuko wa Vatican wa Yohane Paulo II kwa Askofu Mkuu Jacques Mourad.  (© don Marek Weresa)

Kard.Koch:Askofu Mkuu Mourad ni mtu wa upatanisho

Katika Jumba la Kitume,Oktoba 18 ilifanyika hafla iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Kikristo,ya kutoa Tuzo ya Mfuko wa Vatican wa Yohane Paulo II ambayo ilipokelewa na Mkuu wa Kanisa ka Kikatoliki-Kisiria huko Homs.Riccardi,Mwanzilishi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio alisema:“Shauku yake ya kuishi pamoja kati ya watu tofauti kati ya ndugu inapaswa kuwa ujume kwa wote.”

Vatican News

Tuzo ilitolewa kwa utambuzi wa maisha yake, ushuhda wake wa imani, upendo wa kikristo, mazungumzo ya kidini na jitihada kwa ahadi ya amani na upatanisho. Ndiyo yalikuwa maneno ambayo Kardinali Kurt Koch, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Kikristo alieleza sababu zilizopelekea Mfuko wa Vatican wenye jina la  Papa Wojtyla kuchangia katika Toleo la 2025 la Tuzo ya Yohane Paulo II, kwa Askofu Mkuu Jacques Mourad, Mkuu wa Kanisa Kikatoliki la Kisiria la huko  Homs.

Askofu Mkuu aliyepewa Tuzo
Askofu Mkuu aliyepewa Tuzo   (© don Marek Weresa)

Sherehe

Sherehe hizo zilifanyika tarehe 18 Oktoba 2025 kwenye Ukumbi mmojawapo wa Jumba la Kitume, mjini Vatican mbele ya Kardinali Mario Zenari, Balozi wa Kitume nchini Syria, na Kardinali James Harvey, Mkuu wa Kanisa kuu la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta. Kadhalika walijumuishwa pia na viongozi kadhaa, akiwemo Waziri Mkuu wa zamani wa Poland Hanna Suchocka, pamoja na wawakilishi wa mabalozi na mapadre. Askofu Mkuu Mourad alipokea Tuzo kutoka kwa Padre Paweł Ptasznik, Rais wa Mfuko wa Yohane Paulo II wa Vatican, tuzo iliyoundwa ili kukuza ujuzi wa mawazo na kazi ya Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili na matokeo yake katika maisha ya Kanisa.

Kupokea tuzo
Kupokea tuzo   (© don Marek Weresa)

Kuishi kati ya watu mbalimbali kama ndugu

Kardinali Koch alimshukuru Askofu Mkuu Mourad kwa ushuhuda wake wa maisha na imani na akakumbuka maneno ya Mtakatifu Yohane Paulo II kuhusu kiini cha majadiliano ya kiekumene—kwamba Kanisa linapaswa kupumua kwa mapafu mawili, Mashariki na Magharibi— hatua ambayo ina sifa na inaendelea kuwa sifa ya huduma ya Askofu Mkuu Mourad, ambaye, alitekwa nyara na kuteswa kwa miezi kadhaa na magaidi wa ISIS, hakuikana imani yake na baadaye akawa mtume wa upatanisho. Bwana Andrea Riccardi, mwanahistoria na mwanzilishi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, pia alisisitiza upekee huu wa Metropolitan wa Kikatoliki wa Kisiria wa Homs, akimalizia kwamba hamu ya askofu huyo "kuishi pamoja kati ya watu mbalimbali kama ndugu" inapaswa kuwa ujumbe kwa kila mtu.

Picha ya pamoja siku ya kupkea tuzo
Picha ya pamoja siku ya kupkea tuzo   (© don Marek Weresa)

Mazungumzo sio chaguo

Kwa upande wake, mshindi alifafanua Tuzo hiyo kuwa ni utambuzi wa kazi ya kiroho, kijamii na kiakili ambayo Kanisa nchini Syria limetekeleza katika miundo yake yote. “Ni Kanisa,” akasema, “ambalo limepigana vita vya hali ya juu katika miaka hii yote migumu katika eneo lote la Siria,” na “leo, hasa katika Siria, tunaitwa wote Wakristo na Waislamu, kutambua na kuendeleza vifungo vinavyotuunganisha.” Askofu Mkuu  Mourad, aliongeza kusema kuwa “hapa, ndiyo maana nasema kwa nguvu: utafiti wa kitaalimungu na mazungumzo ya kidini na ya kiutamaduni sio chaguo, lakini ni hitaji muhimu la nyakati zetu, hasa kwa nchi yetu, Syria, iliyosambaratishwa na vita." Kile ambacho nchi yake inahitaji zaidi, na alihitimisha, akimshukuru Papa  Leo XIV na jumuiya yake ya watawa wa Mar Moussa kwamba “ni mshikamano, wa msaada wa kusonga kwa nguvu kubwa kuelekea upatanisho na demokrasia."

Asante kwa kusoma makala hii. Kama unataka kusasishwa kila siku bonyeza hapa: cliccando qui

 

21 Oktoba 2025, 11:57