Kusoma Angelicum kwa ufadhili wa masomo 2025/2026
Na Marina Tomarro na Angella Rwezaula – Vatican.
Ishara halisi ya kufanya elimu ya juu kupatikana kwa wote, kuthamini vipaji na motisha bila kujali hali ya kiuchumi. Hili ndilo lengo la ufadhili wa masomo kwa watu kumi kwa mwaka wa kwanza wa Shahada ya Kwanza katika Sayansi Jamii katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Thomas Aquinas - Angelicum, jijini Roma. Mpango huu ulizaliwa kwa lengo la kukuza upatikanaji wa masomo ya Chuo Kikuu na kusaidia wanafunzi walei, wanaoishi jijini Roma na maeneo mengine ya jirani, ambao wanataka kubobea katika programu hii ya masomo katika Chuo Kikuu cha Kipapa.
Miongoni mwa wanafunzi wa Angelicum waliosoma hapo pia kuna Papa wawili
Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Thomas wa Akwino kina mapokeo ya kale sana. Kwa hakika, msingi rasmi wa jumba la Watawa wa Wadominican jijini Roma, ambalo lingekuwa Angelicum, lilitokea kwa uhamisho wa kisheria wa jumba la Mtakatifu Sabina tangu Upapa wa Papa Honorius III, hadi Shirika la Wahubiri mnamo tarehe 5 Juni 1222. Mizizi yake iko katika Utume wa Kidominican wa kujifunza, kufundisha, na kuhubiri Ukweli, kama inavyooneshwa katika kauli mbiu au moto wa Shirika hilo: "Veritas," yaani “Ukweli”. Miongoni mwa wanafunzi mashuhuri waliopitia Chuo kikuu hicho ni mapapa wawili: Papa Leo XIV, ambapo alisoma na kutetea tasnifu yake ya Udaktari katika "Sheria ya Kanoni" miaka thelathini na minane iliyopita, na Mtakatifu Yohane Paulo II, ambaye alitetea tasnifu yake juu ya "Mtakatifu Yohane wa Msalaba" mnamo mwaka 1940.
Kusudi la kituo cha syansi Jamii
Kusudi la Kitivo cha Sayansi Jamii ni kukuza utafiti na masomo ya ukweli wa kijamii, ambamo mwanadamu anatambua uwepo wake katika haki na amani, kwa nia ya maendeleo kamili. Kupitia mbinu ya fani nyingi, inayojumuisha taaluma za kijamii, kisaikolojia, kihistoria, kisheria, kiuchumi na kisiasa, huwapatia wanafunzi zana za kinadharia na vitendo kuelewa na kushughulikia mienendo changamano ya kisasa ya kijamii, katika mazungumzo na mawazo ya kijamii ya Kikristo. Kwa hiyo uangalifu hasa unazingatia nyanja za kisiasa, kimaadili na kiuchumi, ili kutoa mafunzo kwa wataalamu wenye uwezo wa kuchangia katika michakato ya kufanya maamuzi na manufaa ya wote. Ahadi hii ni sehemu ya Tamaduni ya Wadominican ya maadili ya kijamii, ikiweka utaftaji wa ukweli kama msingi wa mabadiliko ya kweli kuelekea ustaarabu wa upendo na amani.
Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ni Septemba 15
Maombi lazima yawasilishwe ifikapo Septemba 15 kwa barua pepe: fass@pust.it, pamoja na nyaraka zinazohitajika ikiwa ni pamoja na: hati ya utambulisho, diploma na cheti cha kukamilika, barua ya motisha, na barua ya mapendekezo kutoka kwa Paroko. Masomo yamepangwa kuanza tarehe 6 Oktoba 2025. Aidha, wanafunzi watakaopata wastani wa angalau 8.5/10 katika mwaka huo watastahiki kutuma maombi ya ufadhili mpya kwa mwaka unaofuata. Kalenda ya kitaaluma, yaa mpango mzima wa masomo, na habari zaidi juu ya programu zinapatikana kwenye tovuti rasmi ya Angelicum:https://angelicum.it/it/