Tafuta

2025.09.09 Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Rieti 2025.09.09 Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Rieti 

Kard.Parolin huko Rieti:kuweni na matumaini licha ya uovu unaotabirika wa mwanadamu!

Alasiri Septemba 9,Katibu Mkuu wa Vatican aliadhimisha Misa kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 800 ya kuwekwa wakfu kwa Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria katika mji wa Rieti,Mkoa wa Lazio.Maadhimisho haya yanaangukia ndani ya Mwaka wa Jubilei ya Kanisa la Rieti ambapo Kardinali Parolin aliwahimiza waamini kuendelea kumpenda Bwana.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kuna mambo ya sasa ambayo ni marejeo sahihi ya ukweli wa Kanisa la Rieti na maelekezo muhimu kwa siku zijazo yaliyosikika katika mahubiri yaliyotolewa alasiri tarehe 9 Septemba 2025, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria huko Rieti mkoa wa Lazio, kilomita chache kutoka Roma na Kardinali Pietro Parolin, Katibu  Mkuu wa Vatican. Tukio hilo ni Jubilei iliyofunguliwa Septemba 9  katika  kuadhimisha miaka 800 ya kuwekwa wakfu kwa Kanisa Kuu mnamo tarehe 9 Septemba 1225, na Papa Honorius III, ambayo imerejea katika uzuri  wake wa zamani baada ya kazi ya kukarabati kutokana na uharibifu wa tetemeko la ardhi la  mwaka 2016. Kardinali Parolin awali ya yote alitoa salamu na "ukaribu na baraka za Papa Leo XIV" na akakumbuka kwamba kukumbuka tukio hili kunamaanisha kuadhimisha neema ambayo Mungu ameiweka kwa jumuiya hii. Kwa hiyo tunaadhimisha, anasema Kardinali Parolin, "Historia ya Wokovu" katika jimbo lililokuwa na mapapa watano kuanzia mwaka 1200 hadi 1300; kwa hivyo tunamsherehekea Bwana na watu wake.

Kanisa Kuu la Rieti
Kanisa Kuu la Rieti

Kardinali Parolin hakusahau juu ya matemeko la ardhi  kama asili na yale ya wanadamu kwamba: “Zaidi ya yote, uaminifu wa jumuiya ulijaribiwa mara nyingi, na misukosuko, ‘matetemeko ya dunia’ ya asili, bila shaka, ambayo yameacha alama zisizofutika kwa watu na kuta za jumuiya hii lakini pia na aina nyingine za ‘matetemeko ya dunia’ ambayo bado yanatikisa eneo hili katika utambulisho wao wa kina. Kardinali Parolin anarejea juu ya kuendelea kupungua kwa vituo vyake,  vya Rieti hasa kwa sababu ya kuhama kwa vijana; "ukosefu wa miito na mapambano ya kujenga upya uhusiano katika eneo lililogawanyika. Zaidi cha kusikitishwa kwa kuona hali ambazo hazijatatuliwa ambazo zina hatari ya kuongezeka."

Licha ya yote, uaminifu wa Kanisa la Rieti ni thabiti kwa sababu umejikita katika Kristo ambaye ni tumaini, ambalo ni Neno la mwongozo la Jubilei hii ya Ulimwengu 2025 na ambapo Jubilei ya Kanisa Kuu hilo pia inaadhimishwa. Kwa njia hiyo, Mwaliko ni kutokata tamaa na kumwomba Mungu kuthibitisha na kuimarisha imani yetu na kuendelea kutumaini." Kutumaini, hata wakati ulimwengu unaonekana kumeza tumaini letu kwa vita vya mara kwa mara, ghasia, matetemeko ya dunia ya kiroho, ya kianthropolojia na yaliyopo, wakati huu ambayo hayasababishwi na hali ya asili isiyotabirika, lakini na uovu unaotabirika wa mwanadamu; tumaini linalofanya kazi, hakika kwamba, hata kama mwanadamu anaweza kuharibu, Bwana ndiye anayefufua."

Ndani ya Kanisa Kuu la Rieti, mkoa wa Lazio
Ndani ya Kanisa Kuu la Rieti, mkoa wa Lazio

Kardinali Parolin alisisitiza kwamba “Kuwa ishara ya kupingana ni kuwa "chumvi ya dunia." “Mji huu huu, unatukumbusha jambo hili, lenye asili ya Kirumi na lililoko kwenye mojawapo ya barabara kuu za kibalozi, iitwayo Salaria, iliyounganisha Roma na pwani ya Bahari ya Adriatic, ambako chumvi ilitoka. Kwa hivyo, Kardinali Parolin alipendekeza njia zingine za kufuata ili kuongoza siku zijazo. Nyumba ya Bwana, iliyosafishwa kwa ishara ambazo haziiheshimu. Pendekezo la kwanza ni kuamsha upya imani yetu ya ubatizo, kusherehekea kama washiriki wa familia ya Mungu na kama kaka na dada, licha ya tofauti ambazo hata hivyo hujenga Kanisa. Mwaliko huo ni kupinga kutojali "ambako nyakati fulani huathiri jumuiya zetu za Kikristo" na kuruhusu "Bwana atengeneze nafasi popote ambapo nyumba yake imechafuliwa na ishara ambazo haziheshimu makao yake, hata katika hali zetu ndogo."  

Wazo lingine lilielekezwa kwa vijana, ili wawe na shauku ya Injili.  Kardinali alisema Kanisa lao ni Kanisa la kale na hivyo wasiruhusu kamwe 'lizeeke' kupitia mazoea, kwa kubebwa, au kwa kuchunga majivu tu." Mwaliko ni kutazama maisha ya watakatifu wapya Carlo Acutis na Pier Giorgio Frassati—kuwa wachukuaji wa furaha wenye afya njema, mashahidi wa matumaini, wa amani,” “wasijifungie wenyewe au kukatishwa tamaa tu na kile ambacho jamii haiwezi kukupatia, bali wazi kwa maisha”; asili na sio nakala, kama Acutis alisema; "vijana wanaopenda Kanisa la Mwenyezi Mungu, ambalo linajidhihirisha katika Kanisa hili la Rieti, mama wa milele na kamwe mama wa kambo." Kamwe usijiuzulu kwa kukosa miito, bali iombee iwepo.

Kanisa Kuu la Rieti
Kanisa Kuu la Rieti

Kardinali Parolin  anawahimiza mapadre, wanaume kwa wanawake watawa, na watu waliowekwa wakfu kuwasilisha furaha ya kuwa mali ya Mungu, kuleta faraja, na kujitoa wenyewe. Wawe watu wa kike na kiume waliowekwa wakfu katika upendo na Bwana na ambao daima wanajua jinsi ya kuweka upendo huu hai kwa njia ya sala, kusikiliza Neno, adhimisho la sakramenti, umoja na Kristo na mtu mwingine, na matendo ya upendo." Hatimaye, wazo kwa Maria, anayeheshimiwa kama "Mama wa Watu," ambaye "pamoja na Mtakatifu Barbara na Mtakatifu Felix wa Cantalice, Walezi na wasimamizi wa Jimbo hilo, waendelee kubariki jumuiya hiyo ya Jimbo ili iweze kuzidi kuwa "makao ya Mungu kwa njia ya Roho."

10 Septemba 2025, 10:15