Kard.Parolin ataadhimisha misa katika kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Papa Yohane Paulo II
Vatican News
Zaidi ya mwezi mmoja uliopita, tarehe 12 Februari iliyopita, Papa Francisko alituma barua Kardinali Stanisław Dziwisz, ambapo aliwahakikishia washiriki wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Mtakatifu Yohane Paulo II. “Nawatakia kila mtu Mwaka mtulivu wa Jubilei yenye tumaini,” aliandika Papa Francisko na, nikiomba maombezi ya Bikira Mbarikiwa na Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili, ninawabariki kwa moyo wote ninyi na wote watakaoshiriki katika Sherehe hiyo Aprili 2 ijayo.”
Misa na Mkesha wa tarehe 2 Aprili
Kardinali Dziwisz atakuwa katika Kanisa kuu la Vatican wakati tarehe 2 Aprili 2025 saa 9:00 alasiri, Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican atakuwa juu ya madhabahu kuongoza maadhimisho ya Liturujia ya Ekaristi. Kushiriki Misa hiyo itakuwa wazi kwa wote, bila kuhitaji pasi yoyote. Siku hiyo hiyo, majira ya saa 3.00 usiku masaa ya Ulaya, kutakuwa na maombi kwa lugha ya Kipoland na Kiitaliano katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, yatakayoongozwa na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Poland, Askofu Mkuu Tadeusz Wojda, ambaye pia atakuwa miongoni mwa wakonselebranti wa Liturujia ya alasiri.
Kardinali Reina:“zawadi kuu" ya maisha ya Papa Wojtyla
Katika siku za hivi karibuni, katika barua kwa mapadre, watawa, jumuiya na waamini wa Jimbo la Roma, Kardinali Baldassare Reina alifafanua kuwa maisha ya Mtakatifu Yohane Paulo II ni kama zawadi kuu pia, kwa huduma yake ya kichungaji katika jimbo letu, akiwaalika kila mtu kushiriki katika hafla hiyo.
Ikumbukwe Papa Yohane Paulo II alizaliwa mnamo tarehe 18 Mei 1920, huko Wadowice, Poland. Katika ujana wake, Wojtyła alishiriki katika uigizaji wa jukwaa. Alihitimu kwa alama bora zaidi katika shule ya Sekondari ya wavulana wote huko Wadowice, nchini Poland, mnamo mwaka 1938, baada ya muda mfupi Vita vya Pili vya Ulimwengu vilipozuka. Alichaguliwa kuwa Kharifa wa Mtume Petto kuanzia mwaka 1978 hadi kifo chake mnamo mwaka wa 2005 akiwa na umri wa miaka 84, katika Jumba la Kitume mjini Vatican.