Ratiba ya maadhimisho ya Juma Kuu Takatifu imechapishwa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ofisi ya Maadhimisho ya Liturujia za Kipapa imechapisha ratiba ya Misa Takatifu kuanzia na maadhmishyo yatakayofanyika tarehe 13 Aprili, Dominika ya Mawawi, hadi tarehe 27 katika Dominka ya Pili au ya Huruma ya Mungu. Saa 4.00 asubuhi mnamo tarehe 13 Aprili 2025 katika, Dominika ya Matawi, Misa itafanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro ili kukumbuka kuingia kwa Yesu Yerusalemu na wakati wa Mateso yake. Tarehe 17 Aprili, itakuwa ni Alhamisi ya Juma Kuu Takatifu, Misa ya Crismai itaadhimishwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kuanzia saa 3:30 asubuhi, majira ya Ulaya.
Na tena katika Basilika hiyo ya Mtakatifu Petr, siku itayofuata, Aprili 18, Ijumaa Kuu, saa 11 jioni, Ibada ya Mateso ya Bwana itafanyika. Ibada ya kiutamaduni ya Njia ya Msalaba(Via Crucis) imepangwa, kama ilivyo kwa kila mwaka, saa 3.15 usiku majira ya Ulaya kati ya mienge ya waamini katika magofu ya kizamani walipoteswa wakrito wa kwanza paitwapo ‘Colosseum.’
Kwa hiyo jioni ya jioni ya tarehe 19 Aprili 2025, ni Jumamosi Kuu, ambapo Mkesha utaanza saa 1:30 za jioni,masaa ya Ulaya, ambayo yataambatana na Usiku Mtakatifu kuelekea Ufufuko wa wa Bwana na Dominika ya Pasaka. Siku hiyo, tarehe 20 Aprili 2025, katika ratiba iliyotolewa Alhamisi tarehe 27 Machi 2025, inaripoti kwamba Misa itafanyika saa 4:30 asubuhi masaa ya Ulaya, katika Uwanja wa Mtakatifu Petro na baraka ya "Urbi et Orbi" itafanyika.
Hatimaye, maadhimisho ya tarehe 27 Aprili 2025 katika Dominika ya Pili ya Pasaka au ya Huruma ya Mungu, saa 4.30 asubuhi, kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro, pia itakuwa ni kwa ajili ya kumtangaza Mwenyeheri Carlo Acutis ambayo ni sehemu ya Jubilei ya Vijana au barubaru kama yeye.