Rais wa Poland Andrzej Duda,akutana na Katibu wa Vatican
Mazungumzo ya kina katika kuelekea kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Mtakatifu Yohane Paulo II na milenia ya kutawazwa kwa Mfalme wa kwanza wa Poland, masuala ya kimataifa kwa kuzingatia vita nchini Ukraine na usalama barani Ulaya yalikuwa ni mazungumzo kati ya Rais wa Jamhuri ya Poland,Bwana Duda na Sekretarieti ya Vatican,Jumamosi asubuhi,Machi 28.
Vatican News
Ijumaa asubuhi tarehe 28 Machi 2025, Rais wa Jamhuri ya Poland, Bwana Andrzej Duda, alipokelewa na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, akisindikizana na Monsinyo Mirosław Wachowski, Katibu Msaidizi wa Vatican kwa ajili ya Mahusiano na Mataifa.
Masuala ya kikanda na kimataifa
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya habari Vatican, ilibainisha kuwa kulikuwa na Mazungumzo ya kina yalifanyika katika kuelekea kumbukumbu ya miaka 20 tangu kifo cha Mtakatifu Yohane Paulo II na katika kuelekea milenia ya kutawazwa kwa Mfalme wa kwanza wa Poland, Bolesław Chrobry. Baadhi ya mada zenye maslahi kwa pande zote mbili zilijadiliwa. Baadaye, lengo lilikuwa katika masuala ya sasa ya kimataifa, kwa kuzingatia hasa vita vya Ukraine na usalama na amani katika Ulaya.
28 Machi 2025, 14:53