Kupashwa habari Maria:Mimi ni mjakazi wa Bwana nitendewe ulivyonena!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kupashwa habari kwa Bikira Maria, ni tukio muhimu sana kwa wakaristo hasa Wakatoliki na Waorthodox ambapo tangazo la Malaika Mkuu Gabrieli alipomtangazia Bikira na akakubali kuwa Mama wa Mungu kwa kuitikia: ‘Tazama mimi hapa mjakazi wa Bwana, nitendewe kama ulivyo nena”(Lk 1:35).
Leo tarehe 25 Machi 2025 Mama Kanisa anaadhimisha siku kuu ya Maria kupashwa habari kuwa atakuwa ni Mama wa Mungu. Baba Mtatifu Francisko kama Mapapa wengine watangulizi wake amekuwa na ibada kuu kwa Mama Maria (inajionesha wazi ile ya "Salus Populi Romani) lakini hata hivyo kati ya sifa alizompatia anasisitiza kuwa: "Kujitolea kwa Maria sio nidhamu ya kiroho, bali kuwa ni hitaji la maisha ya Kikristo. Mama Maria ni msaini wa uandishi wa Mungu kwa wanadamu. Maria ndiye safina salama katikati ya gharika. Mkristo bila Mama Yetu Maria ni yatima," na sifa nyingi sana ambazo ni vigumu kuzieleza zote.
Mama Yetu wa Mateso Saba. Katika mahubiri yake tarehe 3 Aprili 2020, kutoka Mtakatifu Marta, Papa Francisko alizungumza kuhusu Mama Yetu wa Huzuni na kusisitiza umuhimu wa kutafakari juu ya mateso Saba. Kwa namna ya pekee, alionesha unyenyekevu wa Maria: "Hakuwahi kujitafutia vyeo mwenyewe. Cheo muhimu zaidi kwa Bikira Mwenyeheri ni 'Mama', ambayo alipokea kutoka kwa Yesu mwenyewe. Na kwa hiyo, kama Mama tunapaswa kumfikiria, lazima tumtafute, tunapaswa kumwomba. Yeye ni Mama, na katika Kanisa Mama. Tutaendeleza...
Tuombe: