Bi Gambino:Miaka 30 ya Evangelium Vitae ni maono ya mbali ya Papa Yohane Paulo II
Na Angella Rwezaula – Vatican.
"Tunapaswa pia kuwafundisha mapadre wajao, katika seminari na baadaye: ili wajue jinsi ya kuwaongoza vijana na familia kuelekea kwenye ukweli na wema; Mafunzo haya leo hii hayapo kuhusiana na hitaji la usindikizaji lililopo ulimwenguni kote. Kwa sababu hiyo, Baraza letu la kipapa la Walei, Familia na Maisha lilichapisha, tarehe 24 Machi 2025 katika mkesha wa kumbukizi ya Waraka wa Evangelii Vitae (EV), ambao ni mwongozo wa kichungaji uitwao: "Maisha ni mazuri daima" wenye mapendekezo kwa Makanisa mahalia kuanzisha mchakato na kujenga huduma ya kichungaji kwa ajili ya maisha ya binadamu katika mabaraza ya maaskofu na majimbo, na ambako kuna ofisi za Walei, Familia na Maisha." Ni katika mahojiano na mwandishi wetu wa Vatican News, Dorota Abdelmoula-Viet na Bi Gabriella Gambino, Katibu Mkuu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Walei Familia na Maisha, akifafanua juu ya Waraka wa Kitume wa Evangelium vitae" kuhusu Thamani ya Maisha ya mwanadamu ukitimiza miaka 30 tangu uliochapishwa na Mtakatifu Papa Yohane Paulo II kunako tarehe 25 Machi 1995. Yafuatayo ni mahojiano kamili ya Mwandishi wetu wa Vatican, Viet na Gambino:
Miaka thelathini imepita tangu kuchapishwa kwa Waraka wa Evangelium vitae, nguzo ya mafundisho ya Kanisa kuhusu utakatifu wa maisha ya mwanadamu. Je, ni kwa jinsi gani waraka huo umeongoza na kuendelea kulitia Kanisa moyo? Je, bado ni kitovu cha kumbukumbu leo hii?
Evangelii vitae (EV) ni nguzo ya mafundisho ya Kikristo juu ya thamani isiyoweza kuondolewa ya maisha ya kila mwanadamu. Mtakatifu Yohane Paulo II alikuwa ameelewa kwamba aina mbaya sana za ukiukaji wa maisha ya walio dhaifu zaidi, ya watoto wadogo, kati ya wale ambao ni dhaifu, haikuwa chochote zaidi lakini ni usemi wa wazo potovu la uhuru, ambalo hubadilisha uhalifu kuwa sawa, kuficha uwezo wa mwanadamu kuelewa kwamba uhuru ni kama vile mtu anajua jinsi ya kuchukua jukumu kwa maisha ya ndugu ambaye yuko karibu nasi. Si kwa bahati mbaya kwamba Waraka huo ulianza na swali la Mungu kwa Kaini, Umefanya nini? Hata leo hii swali hilo linasikika katika majisterio ya sasa, kuanzia Evangelii gaudium hadi Dignitas infinita: aina mbaya sana za ukiukwaji wa maisha ya mwanadamu hazijapungua, kwa hakika, na Kanisa zaidi ya hapo awali linataka kuthibitisha kwa nguvu tena thamani ya maisha na kuunda dhamiri ili kuelewa thamani hii, ambayo haimaanishi ‘usiue’ tu bali pia utengeneza hali hizo ili kila mtu aweze kufikia utimilifu wa maisha ambayo ameitiwa na Upendo wa Mungu.
Hii ndiyo sababu Dignitas infinita inasasisha ujumbe wa Evangelium Vitae na sio tu kwamba inaeleza tena kwa nini utu wa binadamu lazima uheshimiwe tangu kutungwa mimba hadi kifo cha asili, lakini umepanua mtazamo wake kujumuisha hali za kijamii ambazo tunaonekana kutokuwa na uwezo wa kuona kwamba ni ukiukwaji wa utu wa mtu: Nafikiria vita vya kutisha ambavyo vinatuzunguka, unyanyasaji wa watoto na unyanyasaji wa kijinsia kupitia ulimwengu wa kidijitali, ambao huharibu na kuharibu maisha ya maelfu ya familia ni mambo ambayo yanaonekana wazi. Tukumbuke kwamba thamani ya maisha si tu thamani ya Kikatoliki, bali ya kidunia, ya ulimwengu wote, ni ya mwanadamu hivyo na kila mtu anaweza kuielewa na kuishiriki. Na haipatikani, ambayo ina maana kwamba hakuna mtu anayeweza kuiondoa, hata hakuna mtu anayeimiliki. Leo, tunatatizika kuelewa hili katika ulimwengu uliojaa (relativism)ikiwa na maana mitazamo ya kifalsafa inayokanusha madai ya usawa,au uhusiano na mtazamo wa muktadha fulani unaothamaniwa) ambayo hutafsiri kuwa sheria ambazo mara nyingi zisizo za haki, ambazo hutuchanganya kama kila maisha ya mwanadamu ni kitu kizuri kila wakati. Na sasa tunajua kwamba mkanganyiko huu, kwa njia moja au nyingine, unajidhihirisha katika tamaduni zote, katika kila sehemu ya dunia.
Je, kuna mapendekezo yoyote thabiti na njia ambazo Makanisa yanaweza kupendekeza tena ujumbe wa Evangelium vitae?
Kwa hakika, kusoma tena waraka pamoja na ule wa Dignitas infinita, ambao unathibitisha tena kuwa Evangelii Viate, unaendelea kufungua mlango wa tumaini, ambao tunahitaji: maisha yanashinda, hii ndiyo Injili inatufundisha. Lakini ni lazima tuunde dhamiri ili watu waweze kufanya ‘chaguo za maisha’ kikweli: utoaji mimba, euthanasia, jeuri, utamaduni wa kutupa huharibu mtu anayezitenda, si wale tu wanaoteseka, huzalisha mateso makubwa sana. Kwa sababu hiyo, umefika wakati wa kujaribu kujenga Utunzaji wa kweli wa Kichungaji wa Maisha ya Mwanadamu katika majimbo na parokia, na kuwafundisha wachungaji, waelimishaji, walimu, wazazi na vijana kuheshimu maisha. Hatupaswi kulazimisha sheria, lakini kusambaza maadili, kujua jinsi ya kutetea ukweli wake, lakini pia kuonesha katika uzuri wake wa kushangaza. Ni muhimu sana kwa vijana leo hii kupata uzoefu wa huduma ya maisha, kutoa wakati wao kwa wale wanaohitaji: ni kwa njia hiyo tu wanajihisi kuwa muhimu, kugundua maana katika maisha yao na kisha wito au wito kwa taaluma ambayo inakuwa huduma ya maisha.
Tunapaswa pia kuwafundisha mapadre wajao, katika seminari na baadaye: ili wajue jinsi ya kuwaongoza vijana na familia kuelekea kwenye ukweli na wema; Mafunzo haya leo hii hayapo kuhusiana na hitaji la usindikizaji lililopo duniani. Kwa sababu hiyo, Baraza letu lilichapisha, tarehe 24 Machi 2025 katika mkesha wa kumbukumbu ya Waraka wa Evangelii Vitae (EV), mwongozo wa kichungaji uitwao: ‘Maisha ni mazuri daima’, wenye mapendekezo kwa Makanisa maalumu kuanzisha mchakato na kujenga huduma ya kichungaji kwa maisha ya binadamu katika mikutano ya maaskofu na majimbo, na ambako kuna ofisi za Familia na Maisha. Kuna mipango ya hapa na pale, lakini mara nyingi ni ya nadra na ya hapa na pale. Tunahitaji kuunda meza za kudumu za kufanya kazi ili kupanga dhamira thabiti na endelevu ya kuwafunza waamini katika ulinzi na uendelezaji wa maisha na utu wa mtu. Maadhimisho haya, kwetu sisi kama Kanisa, si tukio la kusherehekea tu, bali lazima liwe ni fursa ya kuchukua hatua madhubuti za kikanisa kwa maisha.
Je, ni kwa Jinsi gani, Baraza litasindikiza Makanisa katika utekelezaji wa mwongozo huu wa huduma ya kichungaji ya maisha ya mwanadamu?
Katika miezi ijayo tutaanza mikutano ya mtandaoni na ofisi za familia na maisha za Mabaraza ya Maaskofu duniani kote, ili wajisikie kuwa wanaambatana katika kuanzisha michakato ya kupanga na kutengeneza huduma ya kichungaji ya maisha katika majimbo. Kwa mbinu ya utambuzi wa kisinodi, kila mtu ataweza kufanya kazi kuanzia uhalisia wake wa kiutamaduni na kijamii na kutambua vipaumbele kwenye mada, mbinu za mafunzo, na hatua za kichungaji. Hii ndiyo sababu rasilimali ya Mwongozo tunayopendekeza, ambayo inaweza kupatikana kwenye tovuti ya Baraza la Kipapa la Walei Familia na Maisha: www.laityfamilylife.va. na ambayo haitazami masuala ya mtu binafsi kuhusu maisha, ambayo Majisterio imeshughulikia kwa kina, lakini wakati huu inapendekeza mbinu ya sinodi ya utambuzi ili kuhakikisha kwamba "utamaduni wa maisha" unakuwa wasiwasi wa mara kwa mara wa kujua jinsi ya kukaribisha na kuambatana na maisha daima. Zaidi ya hayo, kazi hii si chochote zaidi ya utekelezaji zaidi wa Mkataba wa Kimataifa wa Familia, unaotoa ushirikiano kati ya vyuo vikuu vya Kikatoliki–ambavyo vina taasisi za utafiti na mafunzo kwa ajili ya familia na maisha – na majimbo, kwa lengo la kuwafunza walei kadiri ya vipaumbele na mahitaji ya kichungaji ya Makanisa husika.”