Kardinali Semeraro: Salvo D’Acquisto ni mfano angavu wa upendo kwa familia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ujana wa aina tatu wa Salvo D'Acquisto ndiyo mada iliyokuwa katikati ya misa iliyoadhimishwa Jumamosi tarehe 22 Machi 2025 huko Napoli nchini Italia baada ya kutangazwa kwa amri ya Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu ambayo ilitangaza Mtumishi wa Mungu kuheshimiwa. Katika Basilika ya Mtakatifu Clara ambapo Askari wa kishujaa amezikwa, ibada hiyo iliongozwa na Kardinali Marcello Semeraro, Mkuu wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu akishirikiana na Askofu Mkuu Santo Marciano, wa Shirika la kawaida la kijeshi kwa Italia. Wengine waliokuwapo walikuwa Katibu Msaidizi wa Ulinzi, Isabella Rauti, na Kamanda Mkuu wa Polisi, Mkuu wa Kikosi cha Jeshi, Salvatore Luogo, na Alessandro kaka yake Mtumishi wa Mungu Salvo. Katika hatua za mwanzo za maisha, thamani ya familia inakuzwa na kujifunza kupenda. Na ni katika mtazamo huu ambapo histori ya kibinadamu na ya Kikristo ya makamu wa Brigedia inajipendekeza kama kichocheo na kutia moyo kwa kutafakari upya umuhimu wa mahusiano ya kifamilia.
Uaminifu, upendo katika kivuli cha familia
Kardinali katika mahubiri yake kwa kuongoza na kifungu cha Injili kilichosomwa kwa ajili ya tukio hilo, cha mwana mpotevu, alikiunganisha na wakati wa Kwaresima kwamba:"Ni wakati ambao lazima tufanye moyo wa Baba, moyo wa Mungu, kuwa na furaha kwa kurudi kwake daima." Kardinali pia alitualika kusali kwa maneno ya mkonselebranti, Monsinyo Santo Marciano, Msimamizi wa Shirika la kijeshi la kawaida kwa upande wa Italia, "ili kupata kutoka kwa Bwana neema ya muujiza ambapo Papa anaita muujiza wa 'muhuri wa Mungu juu ya tamaa zetu' ambapo Kanisa litajisikia mamlaka ya kuendelea na kutangazwa kuwa Mwenye heri. Kardinali Semeraro kisha alifuatilia hatua za maisha ya makamu wa Brigedia: ujana wake wa mapema, alitumia kujifunza uaminifu na kujitolea kufanya kazi"kutoka kwa baba yake, na upendo kwa wengine kutoka kwa mama yake, pamoja na imani kubwa katika Mungu mpaji. Mapenzi ya D'Acquisto pia yalienea kwa Bibi yake mzaa mama, ambaye alishiriki naye katika sherehe za kiliturujia na kusali kila siku wa Rozari.
Sala lakini pia matendo mema ya huruma
"Haitoshi kusali, lakini lazima pia tufanye matendo mema." Hivi ndivyo makamu wa Brigedia alikuwa akieleza familia yake. "Hakuwa mtu shupavu, alikuwa muumini,"Kardinali Semeraro alisema. Kanuni ambayo aliitumia tangu utotoni, kama inavyooneshwa na kipindi fulani muhimu: alichochewa na huruma kwa mvulana asiye na viatu na baridi ambaye alikuwa akiomba zawadi, alivua viatu vyake na kumpatia. Katika zawadi hizi za kwanza zawadi yake kuu ilikomaa, zawadi ya maisha yake mwenyewe.
Ujana wake wa pili
Familia ya pili, kwa Mtumishi wa Mungu ilikuwa ya kuwa Askari. Muktadha ambao, kama Kardinali Semeraro alikumbuka, D'Acquisto kuwa "alikomaa kwa uzito na heshima". Wenzake katika katika kushika silaha walishuhudia kujitolea kwake kwa huduma. "Alionekana mzee kuliko alivyokuwa." Askari mwenzake alimtaja kuwa mtu ambaye alikuwa kielelezo kwao, hata kwa maisha yake ya imani, zaidi ya maneno. Ingawa alijitolea sana kwa jukumu, hakukosa kufurahiya wakati wa burudani, pamoja na matembezi huko Vomero, safari za Bagnoli na ziara za kiutamaduni huko Roma. Bado wakati wake wa kupumzika pia ulijumuisha kazi za hisani, kama vile Dominika zilizotumiwa katika hospitali za Napolo kuwafariji wagonjwa.
Aliipenda familia yake, familia aliyozaliwa, aliipenda familia ya urafiki wake wa ujana, aliipenda familia ya kijeshi. Aliipenda na kuitumikia familia ambayo ilikuwa imekabidhiwa kwake Torrimpietra". Hayo yalisemwa na Kardinali Semeraro, akitoa mfano wa Sheria za mchakato wa kutangazwa kuwa mwenyeheri na kutangazwa kuwa mtakatifu kwa D'Acquisto. Kituo cha Polisi alichokuwa amepewa kilikuwa Torrimpietra. Upendo wa kina baba na wa kina mama hutajirishwa na mchango wa "vyombo vingine vya elimu", kama vile mazingira ya kikanisa, shule na michezo. Kama vile Polisi mwenyewe, ambaye tayari alisifiwa D'Acquisto na Mtakatifu Yohane Paulo II kama "ukweli wa kielimu", akitoa mfano wa "tabia ya kishujaa." Walakini, kulingana na Kardinali, shule ya kwanza na muhimu zaidi ya maisha inabaki kuwa familia, kila moja na "physiognomy" yake ya kipekee, kama ile ya familia za Kusini mwa Italia.
Chemchemi ya maisha yake
Kijana wa tatu aliyepatikana na D'Acquisto ndiye, dhahiri tu, mbaya zaidi: kifo chake. Mnamo tarehe 23 Septemba 1943, kwenye Torre di Palidoro, kwenye pwani kaskazini mwa Roma, kikosi cha kinazi kilimkamata D'Acquisto kufuatia shambulio linaloshukiwa. Katika kulipiza kisasi, raia ishirini na wawili walikamatwa na kulazimishwa kuchimba makaburi yao wenyewe, wakikabiliwa na kunyongwa. Ili kuokoa mateka, D'Acquisto alijishutumu kuwa ndiye pekee aliyehusika, akitoa maisha yake badala ya yao. Alipigwa risasi papo hapo. Kifo chake, hata hivyo, hakikuwakilisha mwisho, bali uhai. Na katika suala hili Semeraro alihitimisha mahubiri yake kwa kurejea kwa nguvu maneno ya Yesu msalabani: "Leo utakuwa pamoja nami peponi." Ninasadiki kwamba, moyoni mwake, neno hili la Yesu lilikuwa na nguvu zaidi kuliko mvuto wa maisha uliomhukumu kifo. Hata Salvo D'Acquisto, akifa, alihisi maneno haya moyoni mwake. Alitoa uhai wake na ndiyo maana yuko Mbinguni.