Kard.Parolin:Kupokonya silaha na kudhibitiwa kunahitajika,amani ya haki na kudumu nchini Ukraine
Vatican News
Kupokonya silaha, vita nchini Ukraine, hali ya Papa Francisko zilikuwa ni mada kadhaa zilizoguswa na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican tarehe 17 Machi 2025 mjini Roma kando ya toleo la kwanza la “ Meza ya Ramadan – Iftar,” mpango uliohamasishwa na Ubalozi wa Morocco anayewakilisha mjini Vatican, na shirika la Klabu ya Mawasiliano ya Kimataifa ya Vyombo vya Habari - MICC, ambapo Katibu wa Vatican alipokea tuzo ya “Nyuso zilizofichika za Mazungumzo" kutoka kwa Balozi wa Morocco, Rajae Naji El Mekkaoui,
Kardinali huyo alikumbuka kuwa Vatican imekuwa na sera ya wazi kuhusu kuweka silaha tena tangu Vita vya Kwanza vya Ulimwengu, "yaani, kusisitiza katika ngazi ya kimataifa kwamba kuwe na upokonyaji silaha kwa ujumla na kudhibitiwa. Kwa hivyo hatuwezi kufurahishwa na mwelekeo wa mambo yanavyokwenda." Kuhusu uwezekano wa mapatano kati ya Urusi na Ukraine Kardinali Parolin alitumaini "kwamba hakuna masharti yoyote yatakayowekwa ili kuzuia kuanza kwa mazungumzo", akimaanisha ukweli kwamba Moscow imeweka mipaka "katika suala la kuthibitisha utiifu wa makubaliano hayo. Lakini mchakato huu uanze hata hivyo: ukizingatiwa kwamba Ukraine hatimaye iko tayari, basi kuwe na nia ya upande mwingine kuanzisha usitishaji vita ambao unapaswa kudumu kwa siku 30.”
Hatua inayofuata, anatumaini Kardinali, ni kuanzisha mazungumzo kutoka hapo ambayo yanaweza kukomesha vita na kuanzisha amani ya haki na ya kudumu ambayo tumeitarajia.” Kisha Kardinali Parolin aliulizwa na waandishi wa habari kuhusu afya ya Papa, akisisitiza kwamba taarifa za matibabu zinatuambia ni nini hasa masharti ya Papa. “Mimi nilimwoma juma moja lililopita basi sikupata nafasi ya kumuona tena kama ilivyokuwa mara ya kwanza. Lakini hii ni tathmini ya nje, basi kwa wengine tunapaswa kushikamana na kile ambacho madaktari wanatuambia.” Katika mikutano hiyo, Katibu wa Vatican alifafanua, “tunawasilisha kwake masuala na matatizo ambayo yanahitaji ufumbuzi na Papa anatoa maoni yake” Hatimaye , alipoulizwa kama kulikuwa na mazungumzo yoyote ya uwezekano wa kujiuzulu kwa Francisko, Kardinali Parolin alijibu: “Hakuna kabisa.”