Jubilei ya Wamisionari wa Huruma:Zaidi ya Mapadre 500 kutoka mabara yote!
Vatican News
Kuanzia Italia, Marekani, Poland, Brazil, Hispania, Ufaransa, Mexico, Ujerumani, Slovakia, Ufilipino, Bangladesh, Ukrane, Colombia, India, ni baadhi tu ya nchi ambazo wamisionari wa Huruma wapatao 500 wanatoka, kuanzia Ijumaa,Machi 28, hadi Dominika waweza kuishi Uzoefu wa Jubilei yao, ambayo ni ya sita kati ya matukio makuu yaliyoratibiwa kwa Mwaka Mtakatifu Mtakatifu uliowekwa wakfu kwa ajili ya matumaini. Papa Francisko ambaye alirejea Nyumbani, Mtakatifu Marta, mjini Vatican baada ya kulazwa hospitalini kwa zaidi ya mwezi mmoja huko Gemelli, hataweza kushiriki lakini atatuma ujumbe wa maandishi.
Idadi ya wamsionari wa huruma inaongezeka
Idadi ya Wamisionari wa Huruma, ambayo huduma yao maaalum ilianzishwa na Papa wakati wa kuadhimisha Mwaka Mtakatifu maalum wa Huruma, pamoja na Hati ya Kuangaza ya mwaka 2015, inazidi kuongezeka na leo hii kuna mapadre wapatao 1258 waliowekwa rasmi duniani kote katika huduma hiyo. Kwa Wamisionari, “ishara ya kujali kwa Mama Kanisa Watu wa Mungu" (Misericordiae Vultus, n. 18), kitivo maalum kilitolewa kusamehe hata dhambi ambazo zimehifadhiwa kwa Kiti cha Kitume. Ratiba ya Jubilei ya Wamisionari wa Huruma itaanza saa 4:00 asubuhi siku ya Ijumaa tarehe 28 Machi, kwa sala katika Ukumbi wa Paulo VI itakayofungua Mkutano wa nne wa Dunia wa Wamisionari. Mkutano huo wa kimataifa unaoandaliwa na Baraza la Kipapa la Uinjilishaji na kufanyika kila baada ya miaka miwili, utakuwa na mada kuu "Msamaha kama Chanzo cha Matumaini" na utagawanywa katika vipindi viwili vya mafunzo.
Dakika za kwanza asili ya kitaalimungu itatambulishwa saa 4.30 asubuhi na Askofu Mkuu Rino Fisichella, Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, wakati katika kikao cha pili, kuanzia saa 6.00, kamili masaa ya Ulaya, huku saa 8 masaa ya Afrika Mashariki na Kati baadhi ya miongozo kwa ajili ya huduma yao ya kichungaji itapendekezwa kwa washiriki. Mkutano utaendelea saa 10:00 jioni kwa kuadhimisha toleo la XII la "Saa 24 kwa Bwana" katika Kanisa Kuu la Mtakatifu 'Andrea della Valle, lililotengwa kwa ajili ya Wamisionari. Mpango wa Kwaresima wa sala na upatanisho, ambao pia ulitamaniwa na Papa Francisko kwa mwaka 2013, utaadhimishwa pia katika majimbo yote ya duniani katika mkesha wa Dominika ya Nne ya Kwaresima, kati ya Ijumaa tarehe 28 na Jumamosi tarehe 29 Machi 2025. Kwa toleo hili, katika Mwaka wa Jubilei, Papa amechagua kauli mbiu muhimu sana: "Wewe ni tumaini langu" (Zab 71:5). Madhumuni ya tukio hilo ni kuweka sakramenti ya upatanisho kuwa kitovu cha maisha ya kichungaji ya Kanisa. Katika tovuti ya Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, parokia na jumuiya za Kikristo zinaweza kupakua bila malipo nyenzo za kuadhimisha jumuiya ya liturujia.
Rozari, Misa na Tamasha
Siku ya Jumamosi tarehe 29 Machi 2025 Wamisionari watapata fursa ya kujionea, kati ya saa 3.00 na 5.00, Asubuhi hija yao kwenye Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Petro. Kisha watakutana kusali Rozari katika Grotto ya Lourdes katika bustani ya Vatican. Tukio la Jubilei litahitimishwa Dominika tarehe 30 Machi 2025 kwa kuadhimisha Misa, itakayoongozwa na Askofu Mkuu Fisichella, kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Andrea della Valle saa 4:00 asubuhi, masaa ya Ulaya. Hatimaye, Dominika alasiri, kwa Wamisionari na kwa yeyote anayetaka, kuwakuwa na Tamasha la tano la Mwaka Mtakatifu lenye mada: "Jubilei ni Utamaduni" Mapitio yatafanyika: tamasha la bure.