Askofu Mkuu Auza ni Balozi mpya katika Umoja wa Ulaya
Vatican News
Jumamosi tarehe 22 Machi 2025 Baba Mtakatifu alimteua Askofu Mkuu Bernardito Cleopas Auza kuwa Balozi wa Vatican katika Umoja wa Ulaya(EU). Mwenye umri wa miaka sitini na sita, ni mzaliwa wa Ufilipino, na ambaye amekuwa na utume wake katika huduma ya Vatican kwa muda mrefu. Mwaka 2008, alikuwa Balozi wa Vatican nchini Haiti, kisha mnamo mwaka 2014 alishika nafasi ya kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican wa Umoja wa Mataifa huko New York Marekani na vile vile kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Shirika moja la Marekani (OAS).
Baada ya miaka 5 ahadi yake bado alitumwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Hispania na Andorra. Ana shahada ya Fasihi na Taalimungu. Anazungumza Kifaransa, Kiingereza, Kiitaliano, Kihispania na Kitagalogi. Nafasi hiyo ya katika Umoja wa Ulaya, anamrithi Askofu Mkuu Noël Treanor, aliyefariki ghafla kwa mshtuko wa moyo mnamo tarehe 11 Agosti 2024. Katika ujumbe wa rambirambi, kuhusiana na marehemu huyo Papa Francisko alitoa shukrani zake za kina kwa "huduma yake ya kujitolea na ya uaminifu" kwa ajili ya huduma ya Vatican.
Hongera kutoka kwa tume ya Comece
Baada ya kutangazwa kwa uteuzi wake, rais wa Tume ya Mabaraza ya Maaskofu ya Umoja wa nchi za Ulaya, (Comece) Askofu Mariano Crociata alionesha furaha yake: "Askofu Mkuu Auza analeta urithi mashuhuri wa kujitolea kwa kidiplomasia na huduma ya kikanisa. Kwa miongo kadhaa alijikita na jukumu kuu katika huduma ya kidiplomasia ya Vatican akionesha kujitolea kwa kina na kuona mbele. Nina hakika kwamba ushirikiano wetu utakuwa na manufaa na matokeo katika kukuza manufaa ya pamoja katika Umoja wa Ulaya. Ninampatia matashi yangu ya dhati kwa nguvu na hekima katika utume wake. Muongozo wa Mungu uwe pamoja naye katika kila hatua,” ndivyo tunasoma ujumbe wa Rais wa Tume ya COMECE.