Tafuta

Cookie Policy
The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the services. Furthermore, technical and analysis cookies from third parties may be used. If you want to know more click here. By closing this banner you consent to the use of cookies.
I AGREE
Presto La tempesta
Ratiba Podcast
Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 15 Machi 2025 amemteua Askofu mkuu Kurian Mathew Vayalunkal kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Chile. Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 15 Machi 2025 amemteua Askofu mkuu Kurian Mathew Vayalunkal kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Chile. 

Askofu Mkuu Kurian Mathew Vayalunkal Balozi wa Vatican Chile

Kabla ya uteuzi huu Askofu mkuu Kurian Mathew Vayalunkal alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Tunisia naAlgeria. Askofu mkuu Kurian Mathew Vayalunkal amewahi pia kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Papua New Guinea pamoja na Visiwa vya Solomon. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Kurian Mathew Vayalunkal alizaliwa tarehe 4 Agosti 1966 huko Vadavathoor, nchini India. Akapewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 26 Desemba 1991 kwa Jimbo la Kottayam.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 15 Machi 2025 amemteua Askofu mkuu Kurian Mathew Vayalunkal kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Chile. Kabla ya uteuzi huu Askofu mkuu Kurian Mathew Vayalunkal alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Tunisia naAlgeria. Askofu mkuu Kurian Mathew Vayalunkal amewahi pia kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Papua New Guinea pamoja na Visiwa vya Solomon. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Kurian Mathew Vayalunkal alizaliwa tarehe 4 Agosti 1966 huko Vadavathoor, nchini India. Baada ya masomo na majiundo yake ya kipadre, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 26 Desemba 1991 na Askofu mkuu Kuriakose Kunnacherry wa “Arcieparchia Kottayam.” Kunako tarehe 3 Juni 1998 alijiunga na utume wa kidiplomasia mjini Vatican na kubahatika kushirikisha karama na vipaji vyake kwenye balozi za Vatican nchini Guinea, Korea, Jamhuri ya Watu wa Dominican, Bangaladesh, Hungaria na Misri.

Askofu mkuu Kurian M. Vayalunkal, Balozi wa Vatican nchini Chile
Askofu mkuu Kurian M. Vayalunkal, Balozi wa Vatican nchini Chile   (Vatican Media)

Tarehe 3 Mei 2016 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Papua New Guinea na kuwekwa wakfu kama Askofu mkuu hapo tarehe 25 Julai 2016. Tarehe 21 Septemba 2016, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa tena kuwa ni Balozi wa Vatican kwenye Visiwa vya Solomon. Tarehe Mosi Januari 2021, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Algeria. Wakati wa maadhimisho ya Sherehe ya Kutolewa Bwana Hekaluni, sanjari na maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 25 tangu Mtakatifu Yohane Paulo II alipoanzisha Siku ya Watawa Duniani, tarehe 2 Februari 2021, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa tena Balozi mpya wa Vatican nchini Tunisia na hatimaye, tarehe 15 Machi 2025 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa tena kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Chile.

Balozi Chile

 

16 Machi 2025, 11:18
Prev
April 2025
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930   
Next
May 2025
SuMoTuWeThFrSa
    123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031