Kard.Parolin,Vita Ukraine:heshima za haki za binadamu na kubadilishana wafungwa
Vatican News
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya habari vya Vatican ilibanisha kuwa: “Tarehe 16 Septemba 2024, Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican alifanya mkutano kwa njia ya video na Tatiana Moskalkova, Kamishna kwa ajili ya haki za kibinadamu wa Shirikisho la Urusi.
Wakati wa mazungumzo hayo, Katibu wa Vatican, pamoja na kushukuru (Ombudslady) wa Urusi kwa jukumu lake katika ukombozi wa mapadre wawili wa Ukraine, alikumbuka hitaji la kulinda, katika muktadha wa mzozo wa sasa, haki za msingi za binadamu zilizoainishwa katika Mikataba ya Kimataifa na kushughulikia baadhi ya masuala ya kibinadamu. Hasa, alitaja msaada kwa askari wa Kiukraine waliowekwa magereza katika Shirikisho la Urusi na kubadilishana kwa pamoja kwa askari waliowekwa magereza nchini Urusi na Ukraine.