Tafuta

Cookie Policy
The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the services. Furthermore, technical and analysis cookies from third parties may be used. If you want to know more click here. By closing this banner you consent to the use of cookies.
I AGREE
Valse des flocons de neige
Ratiba Podcast
Umaskini wa familia nyingi unapelekea tatizo kubwa la kufanyishwa kazi za unyonyaji wa watoto Umaskini wa familia nyingi unapelekea tatizo kubwa la kufanyishwa kazi za unyonyaji wa watoto 

Mkutano wa Kimataifa juu ya ajira za watoto:Jitihada za Kanisa ni kuondoa mizizi ya janga hili!

Umefanyika Mkutano wa Kimataifa Mjini Vatican kuhusu ajira za utoro,ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu.Washiriki kwanza walikutana na Papa.Kardinali Turkson amesisitiza juu ya kujenga imani na mkakati kati ya wanaojikita kupambana ili kufikia mwisho wa tatizo.Mons.Chica Arellano,mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika mashirika ya Fao, Ifad na Pam:"bila unyonyaji,itapatikana jumuiya bora ya wakati ujao".

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu wakati wa kuwakilisha malengo ya Mkutano wa Kimataifa uliokuwa unaongozwa na mada: “Eradicating Child Labour, Building a Better Future”, yaani: "Kutokomeza Ajira ya Watoto, Kujenga Mustakabali Bora” ambao ulioandaliwa na Tume ya Vatican ya UVIKO-19, iliyo chini ya Baraza hilo pamoja na Uwakilishi wa Utume wa Kudumu katika makao ya Mashirika ya Fao, Ifad, na  Pam, Ijumaa tarehe 19 Novemba 2021 uliofanyika mchana katika Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu alisisitiza kwa kina kuhusu sababu, uongezekaji na mikakati ya kuweza kuzuia hizi ajira za watoto. Kardinali Turkson amesema: “kuamsha dhamiri, kuelezea mshikamano kwa watoto na familia zilizopata pigo za ajira za watoto, lakini pia hata kuwajengea imani na mkakati kati ya wale ambao wanajikita na shughuli hizi ya kumaliza shida hii ya unyonyaji wa ajira za watoto.

Kardinali Turkison kwa kukunuu maneno ya Papa Francisko ambaye walikuwa wamekutana naye asubuhi jijini Vatican amesema: “Namna ambayo tunahusiana na watoto, kiwango ambacho tunawaheshimu wao hadhi yao ya kibinadamu na haki msingi, zinajieleza ni kwa namna gani watu wazima tulivyo na tunataka kuwa na mtindo gani wa kijamii tunaotaka kuujenga”, na kwa maana hiyo, Kardinali amebainisha kuwa ni kashfa ambayo mara nyingi imeoneshwa mtindo wa maisha wa kibinadamu  ambao umeondoa hadhi ya  watu walio wadhaifu zaidi na familia ya binadamu,  yaani watoto ambao licha ya kuwa na maendeleo ya sasa, yenye utajiri mkubwa, maendeleo ya kisayansi, kiteknolokia na mawasiliano inaendelea kunyonya na katika kesi nyingine niyo mitindo ya kisasa ya utumwa! Akimnukuu tena Papa, Kadinali Turkson alisema "katika hatua dhidi ya uchumi huo unaua, hakuna anayeweza kusalia kutojali ukiukwaji wa hadhi ya  watoto, kwa sababu sisi sote ni wa familia moja ya kibinadamu, sote tumeunganishwa na tunategemeana, sisi sote tuko kwenye mtumbwi mmoja". Katika ufunguzi wa mkutano huo, mkuu wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu alisema kwamba "Vatican inakaribisha kwa matumaini lengo la Jumuiya ya Kimataifa la kukomesha utumikishwaji wa watoto kwa namna zote, ikiwa ni pamoja na kuajiri watoto kama askari mojawapo ya lengo la Maendeleo Endelevu ya Ajenda ya Umoja wa Mataifa 2030".

Naye Monsinyo Fernando Chica Arellano, Mwakilishi wa Vatican katika Fao, Ifad na Pam, pia alizungumzia juu ya siku zijazo katika hotuba yake ya kuhitimisha, na ambaye kwa mujibu wake alisema "kutokomeza utumikishwaji wa watoto kunamaanisha kujenga maisha bora ya baadaye, kwa sababu kwa kuwakomboa watoto kutoka katika ajira za unyonyaji tunaruhusu uwezo wao wote kuchipua kwa matunda kwa wakati na  kwa sababu bila unyonyaji tutafikia mustakabali mwema kwa jamii nzima, kwani watoto na vijana wa leo watakuwa watawala wetu wa kesho, wasimamizi wa baadaye wa jamii yetu na  nyumbani  kwetu".  Mosninyo Chica Arellano vile vile alisisitiza na kusema kwamba:“Ikiwa tunataka kuthibitisha kwamba tumepiga hatua, hatupaswi tu kuangalia maendeleo ya kisayansi au maendeleo ya kiufundi. Ni lazima kwanza kabisa tufikirie juu ya kimo chetu cha maadili, ambacho kinaendana na ulinzi,  juu ya haki msingi za watoto na utulivu na furaha ya watoto”.

Kati ya watoa mada pia naye Bwana Maximo Torero, mchumi mkuu wa FAO, alizungumzia juu ya aja ya kushambulia sababu msingi za ajira ya watoto katika ujumbe wake kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa Fao, Dk.Qu Dongyu. "Umaskini, njaa, mazingira magumu ya kiuchumi na mabadiliko ya tabianchi ni mambo  ambayo ni kwa lengo la hatua hii, ambayo inahitaji pia kutambua thamani ya elimu" alisisitiza. Vile vile haja ya uratibu na ushirikiano kati ya serikali, mashirika ya kimataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika msingi ilisisitizwa na Chetra Khieu, mkurugenzi mtendaji wa shirika la Damnok Toek, linalosaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na familia zao nchini Cambodia, ambaye alibainisha kuwa katika nchi ya Asia ajira ya watoto ni tatizo la kimuundo lenye mizizi ya kijamii na kiuchumi ambalo linahitaji kweli mwingilio wa sera  za kisiasa kabla  ya kiutamaduni.

20 Novemba 2021, 15:06
Prev
March 2025
SuMoTuWeThFrSa
      1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031     
Next
April 2025
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930