Askofu Duncan Theodore Tsoke Jimbo Katoliki la Kimberley!
Askofu Duncan Theodore Tsoke alizaliwa tarehe 15 Aprili 1964. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 2 Desemba 1995 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo kuu la Johannesburg, Afrika ya Kusini. Tarehe 6 Februari 2016, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu msaidizi wa wa Jimbo kuu la Johannesburg na kuwekwa wakfu tarehe 30 Aprili 2016.
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu Msaidizi Duncan Theodore Tsoke kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Kimberley nchini Afrika ya Kusini. Itakumbukwa kwamba, Askofu Duncan Theodore Tsoke alizaliwa tarehe 15 Aprili 1964 huko Deveyton. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 2 Desemba 1995 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo kuu la Johannesburg, Afrika ya Kusini.
Tarehe 6 Februari 2016, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu msaidizi wa wa Jimbo kuu la Johannesburg na kuwekwa wakfu tarehe 30 Aprili 2016. Hatimaye, tarehe 3 Machi 2021 Baba Mtakatifu akamteuwa tena kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Kimberley, Afrika ya Kusini.
13 Machi 2021, 14:23