Ziara ya Papa Leo XIV huko Rimini na San Marino:Ratiba rasmi imechapishwa!
Vatican News
Ziara ya kichungaji ya Papa Leo XIV katika Jamhuri ya San Marino na Rimini mnamo tarehe 22 Agosti 2026 ni fupi lakini imejaa matukio. Pia atasimama kwenye Mkutano wa Urafiki Miongoni mwa Watu, tukio la kiutamaduni linaloandaliwa kila mwaka na Harakati ya Communione e Libarazione yaani Umoja na Ukombozi katika mji wa Rimini, Mkoa wa Emilia Romagna kuanzia Agosti 21 hadi 26, 2026 lenye kaulimbiu: "Upendo Unaosonga Jua na Nyota Nyingine." Ofisi ya Habari ya Kiti Kitakatifu ilichapisha ratiba rasmi, Jumatano tarehe 12 Agosti 2026
San Marino, mikutano na mamlaka, ibada katika Basilika
Ndege itaruka saa 2.00 asubuhi kutoka kituo cha helikopta cha Vatican. Baada ya safari ya saa moja ya ndege, Papa atatua katika Uwanja wa Ndege wa Torraccia (Jamhuri ya San Marino) na kuhamia Piazza della Libertà yaani, Uwanja wa Uhuru. Katika Uwanja wa Jamhuri, Papa atakutana na Makatibu wa Nchi, kwa kufuatiwa na mkutano wa faragha na Kapteni anayeongoza nchi katika Ukumbi wa Baraza la Kumi na Wawili.
Kitabu cha Wageni mashuhuri kitasainiwa hapa. Saa 4:40 asubuhi, Mkutano umepangwa katika Ukumbi wa Baraza Kuu, baada ya hapo Papa atatokea kwenye uwanja kupitia dirisha la Ukumbi wa Jamhuri kwa salamu na baraka ya Kitume. Kisha ataelekea kwenye Basilika ya San Marino, ambapo atakaribishwa na Askofu Domenico Beneventi, wa San Marino-Montefeltro, na Gambera wa Basilika hiyo, Padre Marco Mazzant
Ibada ya Misa itafanyika, pamoja na kuheshimiwa kwa masalia ya Mtakatifu Marino, mbele ya mapadre, watu waliowekwa wakfu, na wawakilishi wa maisha ya kikanisa ya Jimbo. Saa 6:15 mchana, Papa atawasalimu waamini katika uwanja huo na kuwaaga wenye mamlaka.
Ziara ya Kibinafsi kwa Watawa wa Kiagostiniani wa Pennabilli
Papa Leo XIV pia atafanya ziara ya faraga kabisa kwa Jumuiya ya Monasteri ya Mtakatifu Anthoni wa Padua ya Watawa wa Kiagostiniani huko Pennabilli. Utawa huo ni mahali ambapo wakati wa Vita vya Pili vya Dunia watawa walijibu ukatili wa vita kwa kufungua milango yao kwa jumuiya mbili za watawa ambao Wajerumani walitaka kuwafukuza Ujerumani na kwa wasichana wa familia za watu waliohamishwa kutoka Rimini.
Leo hii jumuiya hiyo ina watawa 11 wenye nadhiri za daima na wawili wenye nadhiri za muda na Aspiranti mmoja. Alikuwa ni Padre Robert F. Prevost, wakati huo akiwa ni Mkuu wa Shirika la Waagostiniani ambaye mnamo Novemba 2012, aliidhinisha uhamisho wa watawa wanne kutoka Monasteri ya Kiagostino ya Lecceto (Siena) hadi kwenda Pennabilli, na hivyo kuongeza zaidi uwepo wa watawa hawa wa kutafakari katika eneo hilo.
Mkutano, maonyesho ya Agostino na Harmel, mkutano na maskini na Misa ufukwe wa Bandari
Kutua kwa helikopta ya Papa kwenye Maonyesho ya Rimini kumepangwa saa 8.45 mchana. Papa atatembelea maonyesho mawili: lile la Mtakatifu Agostino na lile la Leo Harmel. Pia kutakuwa na njia ya kwenda katika Kijiji cha Watoto: kutoka hapo kutakuwa na salamu kwa washiriki wa Mkutano ikifuatiwa na mkutano katika Ukumbi Mkuu saa 10.00 jioni.
Papa pia anatarajiwa kuwa katika Kanisa Kuu la Rimini, ambapo atawasili hapo saa 11.30 jioni: akiwa hapo atakutana na wagonjwa, walemavu na maskini wanaosaidiwa na Caritas Jimbo. Kwa hiyo, uhamisho hadi Uwanja wa Bandari ambapo Papa ataongoza Misa saa 12.30 jioni. Ziara hiyo itaisha saa 2.00 usiku na kurudi mjini Vatican, anatarajiwa kufika saa 3.00 usiku.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.
