Tafuta

Papa Leo XIV wakati wa uwasilishaji wa Waraka wa Kitume wa "Magnifica Humanitas." Papa Leo XIV wakati wa uwasilishaji wa Waraka wa Kitume wa "Magnifica Humanitas."  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:Kujenga Amani,kuondoa silaha ya tekonolojia na Akili unde

Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu limetangaza kauli mbiu ya Ujumbe wa Papa Leo XIV kwa ajili ya Siku ya 60 ya Amani Duniani,ambayo itaadhimishwa Januari 1,2027:"Kuondoa silaha za kiteknolojia,kutumikia amani.Siasa kama uwajibikaji wa kuzuia".Ni Marejeo ya mada za Waraka wa "Magnifica Humanitas."

Vatican News

"Kuondoa silaha za kiteknolojia, kutumikia amani. Siasa kama uwajibikaji wa kuzuia,"  hii ndiyo kauli mbiu iliyochaguliwa na Baba Mtakatifu Leo XIV katika kuadhimisha Siku ya LX ya Amani itakayofikia kilele chake tarehe Mosi Januari 2027 na ambayo imechapishwa na Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu.

Katika taarifa iliyotolewa, tarehe 11 Agosti 2026 inabainisha kwamba, “Baba Mtakatifu anapenda kusisitiza wajibu wa kimaadili wa wale walioitwa kutenda katika nyanja ya kisiasa na anawahimiza wanadamu wote kukukuza utu wa mwanadamu na kuchangia katika ujenzi wa amani kuanzia na "teknolojia ya kuondoa silaha.”

Marejeo ya barua ya Magnifica Humanitas

Akirejea Waraka wake wa awali katika kukumbusha kuwa "hakuna mashine inayoweza kufanya vita ikubalike kimaadili” (Magnifica humanitas, n. 198), Papa anaonya kuhusu hatari zinazohusiana na kukabidhi maamuzi ya kijeshi kwa akili unde. Papa Leo XIV anatoa wito wa dhati kwa Jumuiya ya Kimataifa kuhamasisha makubaliano ya pamoja yenye uwezo wa kulinda uwajibikaji wa binadamu na kanuni za kibinadamu katika muktadha ambapo maisha ya watu na kuishi pamoja kati ya watu huathiriwa.

KAULI MBIU YA SIKU YA AMANI DUNIANI 2027

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

 

11 Agosti 2026, 12:10