Tafuta

2026.20.07 Kitabu kipya cha Papa  Leo XIV. 2026.20.07 Kitabu kipya cha Papa Leo XIV. 

Amani inajengwa kwa kupunguzwa silaha na sio silaha za nyuklia

Jumba la Uchapishaji la Vatican limechapisha kitabu kipya cha Papa,chenye kichwa:"Kutokuwa na Silaha na Kupokonya Silaha.Amani ni Zawadi." Kimehaririwa na Alessandro Banfi.Huu ni mkusanyiko wa kwanza wa vitabu kutumia mbinu mbalimbali za Robert Francis Prevost kuhusu mada ya amani tangu kuchaguliwa kwake Mei 8, 2025, kilicho na utangulizi wa maandishi ya Papa ambayo hayajachapishwa.

PAPA LEO XIV

"Amani iwe nanyi!": hii ilikuwa salamu ya kwanza ambayo Yesu Mfufuka aliwapa mitume wake (Yh 20:19). Hii pia ni zawadi ya kwanza ambayo Kristo mfufuka aliwapa marafiki zake na ulimwengu mzima: amani. Hata hivyo, zawadi hiyo haikuja "kwa bei rahisi": mwili mtukufu wa Bwana wa Nazareti ulibeba majeraha ya Mateso. Alivumilia chuki, vurugu, na kusulubiwa kwa ulimwengu. Yesu Kristo aliteseka bila haki, bila kuwa na silaha na kutotumia silaha na akafufuka tena. Ujumbe wa Injili ulikuwa na unaendelea kuwa sehemu ya historia. Leo kama ilivyokuwa miaka elfu mbili iliyopita.

Amani ni hamu kubwa inayochochea mioyo ya watu wengi, lakini pia mara nyingi hutishiwa, kukanyagwa, na kudhihakiwa. Leo hii, Nchi 103 zinahusika kwa namna fulani katika vita duniani (1). Silaha hunguruma na kuua nchini Ukraine, Mashariki ya Kati, Sudan, Myanmar, Yemen, Congo, na katika hali nyingine nyingi.

Mtangulizi wangu mpendwa, Papa Francisko, alibuni usemi "Vita vya Tatu vya Dunia vilivyogawanyika vipande vipande" kuelezea hali ya migogoro iliyoenea, ambayo haijawahi kutokea tangu mwisho wa Vita vya Pili vya Dunia. Nikifuatilia hatua zangu kuhusu mada hii, ambayo sasa imekusanywa katika mkusanyiko huu, ningependa kusisitiza mambo kadhaa ambayo ni karibu na moyo wangu.

Kwanza, amani ni jukumu. Ikiwa silika yetu ya kwanza tunapokabiliwa na tatizo tunalokumbana nalo, mvutano tunaoupata, kosa tunalopata ni kuwahukumu wengine, kuwashutumu na hata kuwahukumu, itakuwa vigumu kwamba kutojali kwanza na kisha chuki itakua karibu nasi. Kuna njia ya kuona ukweli unaoharibu na haujengi. Badala yake, amani huanza na mimi. Inaanza nasi.

Mtakatifu Augustino alisema: "Hizi ni nyakati ngumu, na  ngumu, nyakati za bahati mbaya. Ishi vizuri na, ukiwa na maisha mazuri, badilisha nyakati: badilisha nyakati na hutakuwa na la kulalamika" (2). Hatuwezi kuwaomba wenye nguvu duniani amani ikiwa hatutaanza kuishi wenyewe, tukianza na mahusiano yetu ya kila siku: katika familia zetu, majumbani mwetu, katika miji yetu, katika maeneo tunayofanya kazi. Amani hujengwa kwa ishara ndogo za kila siku: tabasamu linalotolewa, tusi lililosamehewa, neno jema.

Zaidi ya hayo, amani hujengwa kwa ukweli. Hata wale wanaopigana vita wanadai kutenda "kwa jina" la amani. Hakuna mtu mwenye ujasiri wa kutangaza kwamba wanataka vita kwa ajili ya vita: hata wenye nguvu duniani wanajua kwamba kila mtu anatamani haki na anatamani kuishi kwa amani. Hasa baada ya matokeo mabaya ya matukio ya Hiroshima na Nagasaki, kukimbilia vitani kunazidi kuwa "matukio yasiyo na marejesho," kama Mtakatifu Yohane Paulo II alivyosisitiza (3).

Nimekumbusha mara kwa mara miito ya dhati ambayo Mtakatifu Paulo VI aliiambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa(UN). Kinachowaunganisha watu, mtangulizi wangu mtukufu alibainisha, ni mkataba uliofungwa "kwa kiapo ambacho lazima kibadilishe historia ya baadaye ya ulimwengu: hakuna vita tena, hakuna vita tena! Amani, amani lazima iongoze hatima ya watu na ya wanadamu wote!" (4).

 

Kifuniko cha Nne cha Kitabu "Disarmata e disarmante"
Kifuniko cha Nne cha Kitabu "Disarmata e disarmante"

Hasa katika enzi ya atomiki, ukweli lazima utetewe: Sio silaha za nyuklia zinazoleta amani, bali ni kupokonya silaha. Ukweli huu, ambao ulionekana wazi katika miongo ya hivi karibuni, ambapo tulishuhudia kupungua kwa nyuklia, umefichwa na mashindano ya silaha ambayo leo yanatisha na kutisha. Kama mwimbaji-mtunzi na mshairi Bob Dylan alivyoandika, akizungumzia kwa mfano bomu la atomiki katika moja ya shairi lake: "Ninakuchukia kwa sababu mwanadamu alikuumba, na mwanadamu anakumiliki, na mwanadamu anakushughulikia" (5).

Kanisa kwa unyenyekevu linauliza swali kwa wote leo: je, wanadamu wanapaswa kuendelea kuishi Duniani? Mchanganyiko wa utawala wa mtandao na upangaji silaha duniani unatufanya tufikirie swali hili kwa uzito.

Amani inatafuta mashahidi. Mkusanyiko huu unatuweka wazi kupitia nguvu ya nyuso nyingi. Watu waliojadiliwa hapa, akiwemo Mwenye Heri Floribert Bwana Chui, Watumishi wa Mungu Giorgio La Pira, na Dorothy Day, ni mfano wa wanaume na wanawake wengi ambao wamekuza amani, kushinda kishawishi cha ufisadi, kuwasaidia maskini, na kukuza diplomasia.

Pamoja na wanaume na wanawake wanaojulikana, amani inawakilishwa na "wahusika wakuu wasio maarufu" ambao wamefuata dhamiri zao. Kumekuwa na nyakati katika historia ambapo majanga ya nyuklia yamekaribia. Ripoti za habari zinatuambia kwamba uamuzi wa mtu mmoja, afisa wa Kisovieti Stanislav Petrov, ulisaidia kuzuia uwezekano wa vita vya nyuklia duniani: ilikuwa Septemba 26, 1983. Rada kutoka kwenye handaki karibu na Moscow, ambapo Petrov alikuwa kwenye zamu ya ulinzi, iligundua uzinduzi wa makombora kadhaa ya balestiki ya mabara kutoka Marekani yakielekea Umoja wa Kisovieti. Hata hivyo, hili lilikuwa kosa katika mfumo wa ufuatiliaji wa setilaiti wa Kisovieti. Petrov, akikaidi maagizo, aliamua kutoripoti shambulio linalodaiwa: chaguo lililofanywa kwa dhamiri ya mtu aliyejua kwamba kitendo hicho rahisi kingeweza kusababisha mamilioni ya vifo.

Ulimwengu ambapo mashine, haijalishi ni za kisasa na za kasi zaidi kuliko sisi, zinaamua kuwapiga mabomu watu wasio na ulinzi zingekuwa za kutisha kweli. Dhamiri ya mtu mmoja inaweza kuwa na thamani kwa ulimwengu mzima. Hatimaye, amani inahitaji tumaini. Kanisa litaendelea kuhubiri upendo kwa wanaume na wanawake wote.

Kama kuna kitu ambacho ulimwengu unatafuta leo, naamini ni ujumbe wa tumaini kwa wakati ujao. Tuangalie kesho kwa tumaini, tukiwa tumepata chanzo pekee katika ujumbe wa Yesu. Kwa sababu kiini cha mafundisho ya Kristo ni hiki: Upendo, upendo, na kutoa maisha ya mtu kwa ajili ya wengine kushinda kifo, kutengwa, na vurugu: "Nilikuja ili wawe na uzima, na wawe nao tele" (Yh 10:10).

Kwa wale wanaohatarisha kuanguka katika kishawishi cha kukata tamaa mbele ya vita vingi vinavyoendelea duniani, ninatoa mwaliko ambao Papa Pio XI alitoa kwa Kanisa zima: "Tumshukuru Mungu kwa kuturuhusu kuishi katika nyakati ngumu. Sasa, hakuna mtu anayeruhusiwa kuwa wa kawaida." Mungu atuongoze katika njia ya kutotumia vurugu. Waamini na watu wema hawataacha kufanya kazi kama wapatanishi. Kila mmoja wetu afanye amani iwe sababu ya maisha yake.

Vatican, Juni 19, 2026

[1]Taz.Orodha ya Amani Duniani 2026, Sydney 2026.

[2] Mtakatifu Augustino wa Hippo, Sermons, 311, 8.8.

[3] Mtakatifu Yohane Paulo II, Sala ya Amani, 2 Februari 1991.

[4] Mtakatifu Paulo VI,Hotuba wa Shirika la Umoja wa matafa,4 Oktoba1965.

[5] Bob Dylan, Go Away You Bomb, 1963.

KITABU CHA PAPA LEO XIV

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku:Just click here.

21 Julai 2026, 09:17