Tafuta

Ziara ya Papa Leo XIV inaanza Barcelona

Katika baadhi ya mitaa kuna vipeperushi katika ishara ya njiwa vikimkaribisha Papa Leo XIV na vinatangaza: “Benvingut!” hiyo ni lugha ya Kikatalani kwa maana ya “Karibu”.Neno jingine maarufu ni PAU la Kikatalani linamaanisha AMANI.Papa atatembelea Kito cha thamani cha Barcellona,ambacho ni Basilika ya Sagrada Familia.Ni alama maarufu duniani iliyoundwa na mbunifu Antoni Gaudí.Mwaka huu,Barcelona inafanya kumbu kumbu ya miaka 100 ya kifo chake.

Na Paul Samasumo - Barcelona.

Papa Leo XIV aliwasili Barcelona  Jumanne tarehe 9 Juni, ikiwa ni hatua yake ya pili kutembelea nchini Hispania, ikiwa ni katika Ziara yake ya Kitume tangu 6 Juni. Tukizunguka mjini siku chache kabla ya kuwasili kwa Papa, tulikutana na  shughuli nyingi. Mamlaka ya hapa imekuwa ikiendelea kusafisha mitaa na kurekebisha njia za kutembelea. Kuna timu za wafanyakazi kila mahali. Kanisa pia limekuwa likiandaa kumbi mbali mbali. Ingawa mazungumzo yalikuwa yakimhusu Papa Leo XIV mitaani na kwenye mikahawa, watu pia waliendelea na shughuli zao za kawaida kwa njia ya kawaida kama vile kuwapeleka watoto shuleni na kuendesha baiskeli zao na kukaa mezani mitaani. Hata hivyo, kuna uwepo wa usalama unaoonekana lakini kwa ujumla, kila kitu ni shwari.

Basilika ya Familia Takatifu huko Barcellona
Basilika ya Familia Takatifu huko Barcellona

Vipeperushi

Katika baadhi ya mitaa kuna vipeperushi katika ishara ya njiwa vikimkaribisha Papa Leo XIV na vinatangaza: “Benvingut!” neno hilo ni Kikatalani kwa maana ya “Karibu." Neno jingine maarufu ni PAU ambalo tuliambiwa kwa Kikatalani linamaanisha AMANI. Ni wazi kwamba Papa Leo XIV anaonekana kama mtu wa amani. Mtu anayeweza kuhimiza ulimwengu kuishi kwa amani. Ziara hii ni ya kiroho na ya kichungaji sana.

Kaburi la Antoni Gaudi,Mbunifu wa Basilika nzuri ya Familia Takatifu
Kaburi la Antoni Gaudi,Mbunifu wa Basilika nzuri ya Familia Takatifu

Historia ya Barcellona:umaarufu wa Familia Takarifu

Historia ya Barcelolna wakati mwingine inasemekana kuwa ni historia ya Hekalu na jiji. Barcelona imeteuliwa kuwa Mji Mkuu wa Dunia wa Usanifu wa Majengo kwa mwaka 2026 na Shirika la Sayansi Elimu na Utamaduni(UNESCO). Hii ni kwa kutambua historia yake tajiri katika upangaji wa mipango miji. Kito cha Barcelona, ​​bila shaka, ni Basilika ya Sagrada Familia, yaani Familia takatifu. Ni alama maarufu duniani iliyoundwa na mbunifu Antoni Gaudí. Na mwaka huu, Barcellona inasherehekea Mwaka wa Gaudí na kumbukumbu ya miaka mia moja ya kifo chake. Kanisa na jiji vyote  vinajivunia urithi wa Gaudí. Ilikuwa inafaa kwa hiyo kwamba Papa Leo ahudhurie sherehe hizo tatu.

Kito cha thamani huko Barcellona ni Basilika ya Familia Takatifu
Kito cha thamani huko Barcellona ni Basilika ya Familia Takatifu

Kudumisha huduma ya kichungaji kwa wahamiaji

Hata hivyo, akiwa Barcellona, ​​Papa Leo XIV, kama Mchungaji wa ulimwengu wote, atakabiliana ana kwa ana na changamoto za kichungaji za Kanisa mahalia.  Mojawapo ya hizi itakuwa ziara yake katika Parokia inayoendeshwa na Jumuiya ndogo ya Waagostinian yenye wachungaji wanne pekee katika Barcelona nzima - mapadre wawili kutoka Tanzania na wawili kutoka Ufilipino. Wanadumisha uwepo mkubwa wa kichungaji na huduma miongoni mwa wahamiaji.

Mwakilishi wa Vatican akielezea Ziara ya Papa Leo XIV huko Barcellona

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

09 Juni 2026, 13:08