Ziara ya Kitume ya Papa Leo XIV,Barcelona:Mtawa wa Kenya anatumaini upyaisho kupitia ziara ya Papa!
Na Paul Samasumo – Barcelona.
Hispania ilikuwa moja ya mataifa ya kwanza kutuma wamisionari ulimwenguni kote kutangaza Injili ya Kristo. Wengi wetu, hata pia mimi, tulipata kumjua Mungu kwa mara ya kwanza kupitia ushuhuda wao. Sr. Anne Ilia akizungumza na Vatican News alielezea furaha yake katika utume wake huko Barcelona, kuhusu utimilifu wake katika kufanya kazi na kushirikiana na Kanisa ambalo lilimpatia imani hiyo kwanza. “Sasa, katika kubadilishana imani nzuri, sisi ambao hapo awali tulihubiriwa injili na wamisionari hao tumekuja Ulaya kusaidia na kushirikiana katika misheni ile ile ya uinjilishaji hapa,” alisema.
“Ninaishi na kutumikia Kanisa na jamii hapa Barcelona kama mwalimu katika moja ya shule zetu, ambapo ninajitolea kuelimisha na kuwasaidia watoto na vijana. Pia ninasaidia na kufunza Katekisimu katika Parokia yetu. Kama mtaalamu mwalimu, utume wangu ni kuelimisha, na kuwaongoza vijana katika jamii yetu kwa upendo, upendo ulioongozwa na Kristo Mtumishi,” aliongeza. Shirika la Watumishi wa Moyo Mtakatifu wa Yesu ilianzishwa huko Vic (Barcelona) mnamo 1891 na Padre Juan Collell Cuatrecasas wa Hispania, na tunazingatia sana elimu, maendeleo ya vijana, na ustawi wa jamii. “Katika Shirika hili tumejitolea kuwahudumia wale wa mahitaji mbali mbali, tukifuata mfano wa Kristo wa upendo na huruma.”
Papa Leo anatukumbusha kwamba hatuko peke yetu
Alipoulizwa kuhusu matarajio yake kwa ziara ya Papa Leo XIV huko Barcelona, Sr. Anne alionesha matumaini kwamba ziara ya Baba Mtakatifu inawezakugusa na kufufua imani ya watu wote. Alitumaini kuwa uwepo wa Papa "utuwajaza matumaini zaidi, ujasiri, na hamu kubwa ya kumfanya Yesu awepo zaidi katika maisha yetu." Sr Anne aliendelea, "Natumaini kwamba baada ya ziara ya Papa Leo XIV hapa Barcelona, Kanisa litapyaishwa kwa kina wa moyo na kuimarishwa kwa imani. Ninatamani uongofu kwamba wale ambao wamekuwa mbali au hawajali Kanisa watagundua tena furaha ya kuwa sehemu ya Kanisa na kupata uzoefu wa maisha mapya na upendo usio na masharti wa Kristo.
Pia ninatumaini wakati huu kutawatia moyo vijana kuitikia wito wa Mungu kwa ujasiri na ukarimu, iwe ni maisha ya ndoa, maisha ya utawa, au huduma duniani. Ninaamini maneno na uwepo wa Papa yanaweza kukumbusha Kanisa zima kwamba hatuko peke yetu. Sisi ni sehemu ya familia moja ya ulimwengu wote, tumeungana katika sala, katika utume, na katika upendo kwa Kristo. Ziara yake na ifufue ushirika wa kiroho kati ya parokia za mahali hapo, jumuiya za kidini, harakati za walei, na vyama vya kisiasa, na kutusaidia sote kuinua macho yetu kwa Kristo, ambaye hutembea nasi kila siku. Ninaomba kwamba sauti yake iwe wito wazi wa haki na amani katika wakati wetu.”
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here
