Tafuta

2026.06.10 Papa anakaribishwa katika Kisima kikubwa cha Kanari. 2026.06.10 Papa anakaribishwa katika Kisima kikubwa cha Kanari. 

Visiwa vya Kanari:Kutoka bandari ya aibu hadi bandari ya matumaini

Huko Las Palmas de Gran Canaria,Papa Leo XIV anatembelea Bandari ya Arguineguín iliyopewa jina la Bandari ya Aibu mwaka 2020 baada ya maelfu ya wahamiaji kufika na kukosa vifaa vya kutosha. Sasa,Sekretarieti Kuu ya Huduma ya Kichungaji inatumaini ziara ya Papa itabadilisha Bandari hii kuwa mahali pa matumaini na kuwaruhusu wahamiaji "kuhisi wakisindikizwa na Baba Mtakatifu.”

Na Kielce Gussie - Las Palmas de Gran Canaria.

Akirudi kutoka ziara yake ndefu zaidi ya Kitume ya Asia na Oceania mnamo Septemba 2024, Papa Francisko alionesha hamu yake ya kutembelea Visiwa vya Kanari, kwani utunzaji wa wahamiaji ulikuwa mada kuu ya upapa wake. Haya yalisikika wakati akijibu moja ya swali la mwandishi wa habari, waliokuwa naye katika msafara huo ambapo alijibu: "Umesoma mawazo yangu, sivyo? Ninafikiria kwenda Visiwa vya Kanari, kwa sababu kuna hali ambapo wahamiaji wanawasili kwa njia ya baharini." Jimbo la Kanari lilikuwa limepokea barua iliyowekwa sahihi na Papa Francisko akielezea nia yake ya kutembea huko. Hata hivyo, Papa wa Argentina hakuweza kukamilisha safari hiyo.

Lakini mnamo Juni 11 mwaka mmoja na miezi minane baada ya ziara hiyo, Papa Leo XIV anatimiza hamu ya muda mrefu ya mtangulizi wake na kwenda visiwa vya Hispania vilivyoko pwani ya Morocco katika Bahari ya Altantiki. Hii inakuwa mara ya kwanza kwa Papa kutembelea Visiwa vya Kanari katika ziara rasmi ya Kitume. Baadhi wamekaribia kama vile Papa Yohane Paulo II na Papa Benedikto XVI  Papa Francisko akitembelea Morocco iliyo karibu.

Katika siku chache za mwisho kabla ya ziara ya Papa, Enélida Hernández Monzón, Katibu Mkuu wa Huduma ya Kichungaji na mratibu wa sehemu ya Visiwa vya Kisiwa Kikubwa cha Kanari katika Ziara ya Kitume, alielezea hisia zilizoongoza kwenye ziara hii ya kihistoria. "Kuna kazi nyingi, uratibu, na ushirikiano," alizungumza na Vatican News. Lakini pia kuna "wasiwasi" kwa sababu kuna maelezo mengi ambayo yanahitaji kukamilishwa. "Lakini kwa furaha, matumaini, na hamu ya kumkaribisha Baba Mtakatifu miongoni mwetu, kazi inakuwa ya kufurahisha zaidi."

Mshangao maradufu

Ingawa watu wa Visiwa vya Kanari walikuwa wametarajia ziara ya Papa, hawakutarajia hivi karibuni katika upapa wa Papa Leo XIV. Hernández alifichua kwamba walishangazwa na tangazo hilo licha ya matakwa ya mara kwa mara ya Papa Francisko ya kuja. Uamuzi wa Papa Leo XIV kutembelea visiwa hivyo mwaka mmoja tu baada ya  upapa wake ni "mshangao na furaha maradufu", alielezea. Kuwa na Mrithi wa Mtakatifu Petro kutembelea Visiwa vya Kanari ni "muhimu sana," mratibu alisema, kwa sababu Papa "anawaimarisha Wakristo wote katika imani yao." Anawathibitisha katika safari yao ya kiroho na kuwatia moyo kuendelea na dhamira yao ya kufanya kazi kwa ajili ya Injili. Ziara yake, Hernández alisisitiza, pia "inathibitisha kazi ambayo imefanywa kwa karne nyingi katika jimbo la Visiwa vya Kanari."

Mkutano wa matumaini

Ingawa Papa atakuwa na shughuli nyingi za kukutana na mapadre, watawa, na wafanyakazi wa kichungaji katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Anne na kuongoza Misa katika Uwanja wa Gran Canaria, labda tukio linalotarajiwa zaidi huko Las Palmas de Gran Canaria ni Mkutano wa Papa   na mashirika yanayotoa huduma  na wahamiaji katika Bandari ya Arguineguín.

Ilikuwa katika bandari hii mwaka 2020 ambapo zaidi ya wahamiaji 2,600 mara sita ya uwezo wa bandari hiyo walikuwa wamewekwa katika kambi ya wazi, wakilala kwenye blanketi na kuvumilia halijoto kali. Ongezeko la idadi ya wahamiaji waliofika kwenye visiwa hivyo lilikumbwa na ukosfu wa vifaa vya kutosha. Matokeo yake, mahali hapo pakajulikana kama "bandari ya aibu". Sasa, "bandari hiyo hiyo itakuwa uwepo wa Papa Leo XIV Hernández alisema, "bandari hiyo hiyo ambayo ilishuhudia mateso na maumivu makubwa baada ya boti nyingi kufika kwenye fukwe zetu wakati wa miaka hiyo. Kwa sababu hiyo, mkutano huu kati ya Papa na wahamiaji ni zaidi ya fursa ya mara moja tu maishani. Inaashiria mabadiliko. Kuna matumaini kwamba mkutano huu, "unaofanyika kwenye bandari ambayo ilikuwa ni lango la kuelekea mustakabali huo, utawaruhusu watu hao kuhisi wamesindikizwa na Baba Mtakatifu," Hernández alisema. Wahamiaji wenyewe walisaidia kupanga mkutano wa Papa pamoja na mashirika yanayowajali, Caritas ya Jimbo na Wizara ya Uhamiaji, na taasisi mbalimbali zilizojitolea kufanya kazi na jamii za wahamiaji.

Jumuiya moja ya Kanari

Kwa baadhi ya wahamiaji wanaofika kwenye Visiwa vya Kanari, imani ina jukumu katika safari yao kuelekea ujumuishaji na maisha yao mapya. Hernández alielezea kwamba baadhi yao ambao hapo awali hawakuwa Wakristo wamekubali imani hiyo "kwa undani zaidi. Wamepitia mchakato wa uongofu." Kwao na watu wengine 50,000 wanaotarajiwa kujaza Uwanja wa Gran Canaria, kuhudhuria Misa ya Papa Leo XIV jioni  tarehe 11 Juni 2026 itakuwa ni jambo maalum la imani. Katika muktadha wa leo hii, Hernández alitafakari ujumbe ambao Wakristo hutumaini kusikia kila wakati na ambao anaamini Papa ataugusia niwa kututia moyo kuendelea kusonga mbele katika ukuaji wetu wa kiroho, kuendelea kuimarisha imani yetu, matumaini, na upendo.

Tumeitwa kuunda ulimwengu bora kwa ajili yetu wenyewe na kwa vizazi vijavyo, kwa familia na marafiki zetu na kwa wale ambao hatuwezi kukutana nao. Misa ya Papa itakuwa ukumbusho wa wito huu wa ulimwengu wote, "kutenda mema, kuwahudumia wengine, kuwasaidia walio katika mazingira magumu na wale wanaohitaji." Lakini si kwa Wakristo pekee. Uwanja huo utajazwa na wasio Wakristo, Waislamu, na wawakilishi wa imani na tamaduni tofauti za kidini. Kama Hernández alivyosema, ziara ya Papa Leo XIV ni ya umoja, moja ya kuwaunganisha watu pamoja kwenye njia ya imani na matumaini bila kujali dini yao. Wahamiaji ambao wamesafiri kutoka nchi yao hadi Visiwa vya Canari “ni sehemu moja zaidi ya jumuiya ya Canari.”

Mfano kwa wengine

Akitazama hali  halisi ya uhamiaji katika visiwa kwa ujumla, Hernández alikiri kwamba ingawa rasilimali ni chache na sera zinahitaji kubadilishwa vyema kulingana na mahitaji ya sasa, "maendeleo yanafanywa, na watu wanapokea msaada." Visiwa vya Canari, alisema, vinaweza kuwa mfano kitaasisi na kupitia mashirika ya Kanisa wa jinsi ya kuwajumuisha wahamiaji katika jamii za wenyeji. Watoto waliofika peke yao wako katika kozi za lugha na wanashiriki katika mipango ya maendeleo. Wengine hata wamekaribishwa katika familia za wenyeji. Hernández alitoa mfano wa kijiji kilichokuwa ndani ya kisiwa cha Las Palmas ambacho kilikuwa kinakabiliwa na umaskini. Lakini wakati fulani, jamii nzima, pamoja na mamlaka zao za mitaa, walikusanyika na kuwakaribisha watoto wahamiaji wasio na wazazi.

Watoto hawa hawakufufua eneo hilo na kuunganishwa na kijiji tu,  lakini "muhimu zaidi, walipata familia zinazowasaidia kujifunza jinsi ya kuwa na furaha tena na kuwapa upendo na utunzaji ambao huenda wameuacha." Kwa hivyo, nyingi ya familia za watoto hawa "zilijitolea kwa uchungu kwa matumaini ya kuwapa maisha bora" Hernández alisisitiza. Katika visa vingi, watoto hawa wamepata nafasi hiyo kupitia familia za Kanari zilizowakaribisha.

Kisiwa cha Kanari
BANDARI YA AIBU HADI MATUMAINI

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

 

11 Juni 2026, 11:12