Sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo: Pallio Kwa Maaskofu Wakuu Wapya 35 Wanne ni Kutoka Afrika
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV, katika Sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo Miamba wa imani, Jumatatu tarehe 29 Juni 2026, anatarajia kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu pamoja na kuwapatia Pallio Takatifu, Maaskofu wakuu 35 walioteuliwa katika kipindi cha Mwaka 2025-2026. Kati yao kuna Maaskofu wakuu wanne kutoka Barani Afrika nao ni: Askofu mkuu Sithembele SIPUKA: Jimbo kuu la Cape Town (Afrika ya Kusini); Askofu mkuu François SYLLA, Jimbo kuu la Conakry (Guinea); Askofu mkuu Isaac Jogues Kodjo Agbéménya GAGLO Jimbo kuu la Lomé (Togo) n hatimaye ni Askofu mkuu Dennis Kofi AGBENYADZI, S.M.A, Jimbo kuu la Berbérati (Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati.)
Pallio takatifu ni kitambaa cha sufi safi kinachotengenezwa kwa manyoya ya kondoo wachanga; na kinavaliwa na Baba Mtakatifu pamoja na Maaskofu wakuu wa majimbo makuu ya Kanisa Katoliki pamoja na Mapatriaki wa Makanisa ya Mashariki. Hii ni alama ya Kristo mchungaji mwema aliyesadaka maisha yake kwa ajili ya kumkomboa mwanadamu kutoka katika lindi la dhambi na mauti. Kama ilivyokuwa kwa Kristo Yesu, Mchungaji mwema, hata Maaskofu wakuu wanahamasishwa kuwabeba kondoo wao kama kielelezo cha wachungaji wema; wakumbuke kwamba, wameteuliwa si kwa ajili ya mafao yao binafsi, bali kwa ajili ya kondoo wa Kristo Yesu. Maaskofu wakuu wapya wanapaswa pia kusadaka maisha yao kwa ajili ya Kristo Yesu na Kanisa lake. Pallio takatifu ni alama ya umoja na mshikamano kati ya Maaskofu wakuu pamoja na Khalifa wa Mtakatifu Petro.
MAASKOFU WAKUU WANAOPOKEA PALLIO TAKATIFU 29 JUNI 2026
1. Kard. Grzegorz RYŚ
Askofu mkuu wa Jimbo kuu Kraków (Poland)
2. Kard. Konrad KRAJEWSKI
Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Łódź (Poland)
3. Askofu mkuu Shane Anthony MACKINLAY
Jimbo kuu la Brisbane (Australia)
4. Askofu mkuu Mark S. RIVITUSO
Jimbo kuu la Mobile (Marekani)
5. Askofu mkuu Antonysamy SAVARIMUTHU
Jimbo kuu la Madurai (India)
6. Askofu mkuu Alberto S. UY
Jimbo kuu la Cebu (Ufilipin)
7. Askofu mkuu Júlio Endi AKAMINE, S.A.C.
Jimbo kuu la Belém do Pará (Brazil)
8. Askofu mkuu Andrzej PRZYBYLSKI
Jimbo kuu la Katowice (Polond)
9. Askofu mkuu Charles DUVAL, C.Ss.R.
Jimbo kuu la Grouard-McLennan (Canada)
10. Askofu mkuu Charlie M. INZON, O.M.I.
Jimbo kuu la Cotabato (Ufilipin)
11. Askofu mkuu Elias FRANK
Jimbo kuu la Calcutta (India)
12. Askofu mkuu Josef GRÜNWIDL
Jimbo kuu la Wien (Austria)
13. Askofu mkuu David William V. ANTONIO
Jimbo kuu la Nueva Segovia (Ufilipin)
14. Askofu mkuu Susai JESU, O.M.I.
Jimbo kuu la Keewatin-Le Pas (Canada)
15. Askofu mkuu Stephen Andrew HERO
Jimbo kuu la Edmonton (Canada)
16. Askofu mkuu Luciano MAZA HUAMÁN
Jimbo kuu la Piura (Perú)
17. Askofu mkuu Ronald A. HICKS
Jimbo kuu la New York (Marekani)
18. Askofu mkuu Charles Phillip Richard MOTH
Jimbo kuu la Westminster (Uingereza)
19. Askofu mkuu Marco Aurélio GUBIOTTI
Jimbo kuu la Juiz de Fora (Brazil)
20. Askofu mkuu José Roberto FORTES PALAU
Jimbo kuu la Sorocaba (Brazil)
21. Askofu mkuu Sithembele SIPUKA
Jimbo kuu la Cape Town (Afrika ya Kusini)
22. Askofu mkuu José Armando ALVAREZ CANO
Jimbo kuu la Morelia (Mexico)
23. Askofu mkuu Stanislav PŘIBYL, C.Ss.R.
Jimbo kuu la Praha (Jamhuri ya Watu wa Czech)
24. Askofu mkuu James R. GOLKA
Jimbo kuu la Denver (Marekani)
25. Askofu mkuu James Francis CHECCHIO
Jimbo kuu la New Orleans (Marekani)
26. Askofu mkuu Francesco Antonio SODDU
Jimbo kuu la Sassari (Italia)
27. Askofu mkuu Luis Augusto CAMPOS FLÓREZ
Jimbo kuu la Bucaramanga (Colombia)
28. Askofu mkuu François SYLLA
Jimbo kuu la Conakry (Guinea)
29. Askofu mkuu Mário Antônio DA SILVA
Jimbo kuu la Aparecida (Brazil)
30. Askofu mkuu Khalid REHMAT, O.F.M. Cap.
Jimbo kuu la Lahore (Pakistan)
31. Askofu mkuu Isaac Jogues Kodjo Agbéménya GAGLO
Jimbo kuu la Lomé (Togo)
32. Askofu mkuu Guy BOULANGER
Jimbo kuu la Sherbrooke (Canada)
33. Askofu mkuu Dennis Kofi AGBENYADZI, S.M.A.
Jimbo kuu la Berbérati (Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati)
34. Askofu mkuu Michele AUTUORO
Jimbo kuu la Benevento (Italia)
35. Askofu mkuu Giampaolo DIANIN
Jimbo kuu la Gorizia (Italia).
