Tafuta

2026.06.22 Wanachama wa Mfuko wa Jerome Lejeune" 2026.06.22 Wanachama wa Mfuko wa Jerome Lejeune"  (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV:Uingiliaji wa kinabii wa Dk.Lejeune ulimfanya atetee maisha ya kila mwanadamu

Papa Leo XIV ametoa heshima kwa Mtumishi wa Mungu Jérôme Lejeune,mtetezi wa hadhi ya binadamu akikutana Juni 22 na wanachama wa Mfuko wa daktari huyo wa watoto wa Ufaransa na mwanzilishi wa jeni za kisasa.Alikuwa akisema:"ni chuki kwa magonjwa na upendo kwa wagonjwa."Alijua teknolojia inaweza kutumika dhidi ya dawa ambayo kwa asili ni huduma ya maisha kama inavyotokea wakati teknolojia inapoepuka udhibiti wowote muhimu wa kimaadili."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana na wanachama wa mfuko, wanafamilia wa Mtumishi wa Mungu Profesa Jérôme Lejeune Jumatatu tarehe 22 Juni 2026, mjini Vatican na kuwatakia amani wote. Akianza hotuba yake alisema “Ni furaha kusherehekea miaka mia moja ya kuzaliwa kwa Jérôme Lejeune pamoja nanyi, wanachama wa Mfuko  unaoitwa kwa jina lake na unaoendelea na kazi yake. Akisukumwa na mateso ya watoto walemavu, Profesa Lejeune alijitolea maisha yake kama mtafiti wa kisayansi kwao.  Ugunduzi wake maarufu zaidi, ule wa kromosomu inayosababisha trisomy 21, ulimfanya kuwa maarufu wa jeni za kisasa, zinazotambuliwa duniani kote; orodha ndefu ya majina yake ya heshima inathibitisha hili.” Lakini pia alikuwa daktari kwa wito na hakuacha kufanya kazi ili kupata tiba, ili kupunguza mateso ya wagonjwa wake, ambao aliwaita "maskini zaidi kati ya maskini."

Ulinzi wa uhai

 

Alitetea kwa bidii maisha na hadhi ya walio hatarini zaidi, hata kwa gharama ya kazi yake mwenyewe: "Dawa," alipenda kusema, "ni chuki kwa magonjwa na upendo kwa wagonjwa."Akijua ubora wa kitaaluma wa Profesa Lejeune na kujitolea kwake bila kuchoka kwa Kanisa, Papa Mtakatifu Paulo VI alimteua kuwa mwanachama wa Chuo cha Sayansi cha Kipapa. Baadaye, kama wanavyojua, urafiki wake wa kina na Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili na maono yao ya pamoja ya ulinzi wa uhai yalikuwa chanzo cha kuundwa kwa Chuo cha Kipapa cha Maisha, ambacho Profesa Lejeune alikiona kama taasisi muhimu katika kukabiliana na kuongezeka kwa vitisho kwa maisha. Mtu wa sayansi na hekima, Jérôme Lejeune aligundua haraka kwamba ugunduzi wake wa kisayansi ungetumika kuwaangamiza watu wenye trisomy 21 kabla ya kuzaliwa( ni hali ya kimaumbile inayosababishwa na nakala ya ziada ya kromosomu namba 21 mwilini).

Papa akutana na Chama  Mfuko wa Profesa Lejeune
Papa akutana na Chama Mfuko wa Profesa Lejeune   (@VATICAN MEDIA)

Kisha hakusita kuwatetea, akishutumu ukiukwaji wa Kiapo cha Hippocratic (Daktari wa Kale wa kigiriki aliyejulikana kama baba wa tiba) na eugenics (yaani Utafiti wa jinsi ya kupanga uzazi ndani ya idadi ya watu ili kuongeza kutokea kwa sifa zinazorithiwa zinazoonekana kuwa za kuhitajika)mpya aliyoiita "ubaguzi wa rangi wa kromosomu." Uingiliaji wake wa kinabii ulimfanya atetee maisha ya kila mwanadamu kwa jina la hadhi isiyoweza kuepukika ambayo ina asili yake katika tendo la ubunifu la Mungu. Katika suala hili, Papa aliendelea kusema kuwa “alishauri na kushauri taasisi na watawala ulimwenguni kote. Vita hivi vilimletea ukosoaji mkali katika kipindi fulani cha kisayansi. Profesa Lejeune alijua kwamba ingawa teknolojia inaweza kusaidia dawa, haiwezi kuibadilisha. Pia alijua kwamba teknolojia inaweza kutumika dhidi ya dawa ambayo kwa asili ni huduma ya maisha kama inavyotokea wakati teknolojia inapoepuka udhibiti wowote muhimu wa kimaadili na wakati hesabu za ufanisi, faida, au matumizi zinaposhinda.” Lakini thamani ya mtu haitegemei kile anachotimiza au kutoa. Hii ndiyo sababu daktari hapaswi kamwe kujiruhusu, kulingana na algoriti za maabara, kuamua maisha ya kiinitete fulani au mtu mzee! Dawa haiwezi kamwe kuwa mtumishi wa kifo kilichopangwa!

Utunzaji na ulinzi usio na masharti wa mwanadamu

Papa Leo XIV alisisitiza tena kwamba leo hii Mfuko wa Lejeune, ambao wao ni  wanachama hai, unaendelea na kazi iliyoanzishwa na Profesa Lejeune katika nyanja tatu za utafiti, utunzaji, na ulinzi usio na masharti wa mwanadamu. Kwa hiyo Papa alifurahishwa na nafasi wanayochukua duniani kote katika utafiti kuhusu ulemavu wa kiakili wa kijenetiki. Pia waliunda na kuunga mkono Taasisi ya Jérôme Lejeune, ambayo hutoa ushauri nasaha kwa maelfu ya wagonjwa wenye ulemavu mbalimbali wa akili. Katika hilo Papa alipenda “kutoa faraja yangu kwenu katika kujitolea kwenu kwa maisha na utu wa binadamu, hasa kwa mamlaka ya umma. Ninajua kwamba mnaingilia mara kwa mara mijadala ya kijamii ili kumlinda kila mtu katika hali zote za kuwepo kwake. Na najua pia mmejitolea kuhamasisha utamaduni wa maisha kupitia Mwenyekiti wa Kimataifa wa Maadili ya Kibiolojia, ambao hutoa mafunzo ya kitaaluma kwa wataalamu mbalimbali katika uwanja huu: wataalamu wa afya, wanasheria, na wanafalsafa.”

Wanachama wa Mfuko wa  Jerome Lejeune
Wanachama wa Mfuko wa Jerome Lejeune   (@VATICAN MEDIA)

Baba Mtakatifu Leo XIV alitoa shukrani kwa mafunzo hayo wanayowapa wanaume na wanawake ambao, kesho, wataweza kuchangia katika kuhakikisha maadili ya kimatibabu kwa ajili ya kuhudumia utu na uhai wa binadamu. Kwao, marafiki wapendwa wenye(trisomy 21 ) Wagonjwa wa Down (Down Syndrome) na familia zao, kwa watoto wa Mheshimiwa Profesa Lejeune waliopo hapa asubuhi ya leo, kwa ninyi nyote, wanachama wa Taasisi za Jérôme Lejeune nchini Hispania, Argentina, na Marekani, na hatimaye kwa, wanachama kutoka Ureno, Italia, Tunisia, Ivory Cost, na Korea, Papa Leo XIV alipenda “kuelezea kuridhika kwakwe na kazi ambayo, kama watu wa kawaida, wanayoiendeleza katika upendo wa ukweli, katika nyayo za Mtumishi wa Mung Jérôme Lejeune.”

Kwa maombezi ya Mama Yetu

Kama yeye, iweni mashahidi waliojitolea katika jamii, katika huduma ya kutafuta manufaa ya wote. Hii ndiyo kanuni kuu ya kwanza ya mafundisho ya kijamii ya Kanisa, na ya "umbo la kijamii" la hadhi inayotambuliwa kwa kila mtu (Magnifica Humanitas, n. 59). Manufaa ya wote hayawazuii hata mmoja wa wale walioumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.” Ujumbe na kazi ya Mtumishi wa Mungu Jérôme Lejeune imejengwa juu ya umoja wa akili na moyo ulioungana. Aweze kuwatia moyo vijana na wataalamu wengi wanaotamani uthabiti; awasaidie kuunganisha akili na imani, neno na tendo, kutokuwepo kwa hukumu kwa watu na kukataa uongo, bila ugumu. "Ninawakabidhi kwa maombezi ya Mama Yetu, nikimwomba aongoze hatua zenu, asaidie juhudi zenu, na kueneza huruma yake kwa wote wanaohitaji. Kwa nyote mliopo hapa, ninawapa kwa uchangamfu Baraka yangu ya Kitume, ambayo ninawapa wanachama wote wa Foundation, familia zao, na "wapenzi" wa Jérôme Lejeune.”

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

22 Juni 2026, 11:24